MHESHIMIWA RAISI AKIHUTUBIA MAELFU YA WANANCHI NA WAFANYAKAZI WALIOKUSANYIKA UWANJANI. |
Rais
Jakaya Kikwete amelitaka shirikisho la vyama vya wafanyakzi nchini
(Tucta) kutambua kuwa suala la kutoongeza mishahara kwa wafanyakazi
serikali hailifanyii makusudi suala hilo .
Amesema uongezaji wa mishahara kwa wafanyakazi linaendana ukubwa wa bajeti yenye hasa katika ukusanyaji wa kodi .
Raisi
Kikwet amesema hayo leo jijini Mbeya katika kilele cha maadhimisho ya
siku ya wafanyakzi Duniani Mei Mosi ambapo kitifa imefanyika mkoanui
humo katika uwanja wa kumbukumbu ya sokoine na kuhudhuliwa na baadhi ya
viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri na mabarozi.
Katika
hotuba yake Rais Kikwete ameelezea niya ya serikali katika kukabiliana
na changamoto mbalimbali zinazo wakabili wafanyakazi nchi likiwepo suala
la mishahara na tozo kubwa ya kodi.
Rais
Kikwete amesema kuwa nivema shirikisho hilo liktambua kuwa serikali
imekuwa ikifanya kila jitihada katika kuendelea ku boresha maisha ya
wafanyakzi nchini.
Amesema
katika mwaka ujao wa fedha serikali itaongeza kima cha chii cha
mishahara hasa kutokana kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato kutoka
zaidi ya shilingi bilioni 5 kwa mwaka hadi bilioni 6 ambazo kwa
asilimia kubwa zimetengwa katika kuongeza mishahara ya wafanyakazi kwa
asailimia 44.
Hata hivyo Kikwete amesema tamko
rasmi la kuongeka kwa kima hicho cha chini cha mishahara ya wafanyakazi
kitatolewa na waziri wa fedha wakati akiwasilisha bajeti yake katika vikao vya bunge Dodoma .
Katika
suala la punguzo la kodi kwa wafanyakazi hao Rais Kikweta amesema kuwa
katika mwaka 2009/2010 serikali ilipunguza tozo ya kodi kutoka asilimia
18 hadi 15 ambapo kwa mwaka 2011/2012 punguzo la kodi lilikiwa asilimia 14 hivyo bado serikali inaendelea kulipunguza tatizo hilo.
Hata hivyo Kikwete amesema anatambua kuwa zipo changamoto nyingi zinazo wakabili wafanyakazi hao lakini ameahidi kuendelea kuzifanyia kazi pamoja na kukaa na viongozi wao katika kuzungumzia mbalimbali yanayo lihusu shiriksho hilo .
Wakati huo Mheshimiwa Raisi
amewatoa kwa wafanayakzi watakao staafu kuwa suala la kupata fao lao la
kustaafu litatolewa licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali
zinazoukabili mfuko huo wa hifadhi ya jamii (SPF)
Amesema serikali
imejiwekea mkakati wa kuhakisha inaweka kiasi cha shilingi bilioni 50
kila mwaka ili kuhakikisha kila atakye staafu anapatiwa haki yake bila
kuchelewa.
Pia ametoa wito wa
mifuko ya hifadhi ya kijamii njini kucha tabia ya kuwalazimisha
wafanyakazi hao kujiunga na mifuko hiyo kwani kinyume cha taratibu na
sheria ya mifuko hiyo.
Katika
saula la amani Raisi Jakaya Kikwte Pia amewataka wananchi Mkoani humo
na watanzania kwa ujumla kuendelea kuilinda amani iliyopo kwani madahara
ya kutokewaka kwa amani ni makubwa hivyo amewataka kungana kwa pamoja
kuilinda amani hiyo.
0 comments:
Post a Comment