NAIBU Waziri wa Fedha Janeth Mbene ametoa msaada
wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya Shilingi Mlioni 7 kwa timu 16 za Wilaya
ya Momba Mkoani Mbeya.
Vifaa hivyo ni pamoja na jezi za mpira wa
miguu jozi 16 ambazo zilizawiwa kwa timu zote zilizoshiriki Michuano ya Ligi ya
Mpira wa Miguu iliyofanyika katika Mji Mdogo wa Tunduma iliyojulikana kwa
jina la CCM Super Cup.
Mbali na vifaa hivyo vya michezo Naibu Waziri
alitoa pia kitita cha Fedha Shilingi Milioni Moja kwa ajili ya washindi watatu
wa Mwanzo ambapo Mshindi wa Kwanza alijinyakulia Shilingi Laki tano(500,000/=),
Mshindi wa pili Shilingi Laki tatu(300,000/=) na mshindi wa tatu alijinyakulia
Shilingi Laki mbili(200,000/=).
Timu zilizoibuka kidedea katika michuano hiyo ni
pamoja na Timu ya Nasele Fc ambayo ilikuwa mshindi wa Kwanza na
mshindi wa Pili ikiwa ni Timu ya Super Rangers zote za Mpemba huku Mshindi wa
Tatu ikichukuliwa na Timu ya Eagle Fc kutoka katika Mji mdogo wa Tunduma.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Naibu Waziri
wa Fedha, Mkuu wa Wilaya ya Ileje Rosemary Senyamule alisema lengo la michuano
hiyo ni kuleta Umoja kwa vijana wa Wilaya ya Momba ikiwa ni pamoja na kukuza
vipaji ili kupata Wachezaji wa Timu ya Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla
kutokana na Mji wa Tunduma kutoa Wachezaji wengi wazuri.
Alisema katika Michuano hiyo ilipata mafanikio
makubwa kutokana na kukusanya watu wengi bila kujali itikadi za Vyama vya
Siasa ambapo pia aliwaomba wadau mbalimbali wa michezo kujitokeza
kudhamini michezo ili kuinua viwango na kutoa ajira kwa vijana.
Aidha kabla ya kuwa mgeni rasmi katika Fainali ya
Michuano hiyoiliyokamilika Mwishoni mwa Wiki iliyopita Mkuu huyo wa Wilaya
alipata fursa ya kutembelea vikundi mbali mbali vya uzalishaji mali na
Wafanyabiashara wa Tunduma.
Senyamule aliwaahidi wafanyabiashara na
wajasiliamali hao kuwasaidia kutoa elimu ya ujasiliamali ili kukuza vipato vyao
kutokana nay eye kuanzisha mpango wa kutoa elimu kwa wajasiliamali Wilayani
Ileje ambao wameonekana kunufaika na mpango huo.
Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
|
0 comments:
Post a Comment