Pages


Home » » TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYAHABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 14/12/2012.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYAHABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 14/12/2012.

Kamanga na Matukio | 02:33 | 0 comments



WILAYA YA CHUNYA - TAARIFA KUOKOTWA KWA SILAHA [BASTOLA].
MNAMO TAREHE 12.12.2012 MAJIRA YA SAA 09:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA IFUMBO WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. WATOTO WADOGO WALIOKUWA WAKICHEZA MPIRA WA MIGUU KATIKA UWANJA WA S/MSINGI IFUMBO WALIOKOTA BASTOLA MOJA ILIYOTENGENEZWA KIENYEJI INAYOTUMIA RISASI ZA S/GUN IKIWA NA RISASI MOJA YA S/GUN . MBINU NI KUHIFADHI SILAHA HIYO KATIKA MFUKO WA RAMBO NA KUIWEKA KANDO YA UWANJA HUO . KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOMILIKI SILAHA BILA YA KIBALI KWANI NI KOSA LA JINAI. AIDHA ANATOA RAI KWA WAZAZI/WALEZI KUWAELIMISHA WATOTO KUACHA TABIA YA KUOKOTA NA KUCHEZEA VITU AMBAVYO HAWAVIFAHAMU KWANI VINGINE VINAWEZA KUWA  NI VITU VYA HATARI/MILIPUKO NA BADALA YAKE WATOE TAARIFA KWA WAZAZI/WALEZI AU MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA HARAKA ZICHUKULIWE KUEPUSHA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA.KAMANDA PIA ANARUDIA KUTOA WITO KUWA KIPINDI HIKI NI CHA ‘”OFFER “ YA KUSALIMISHA SILAHA BILA KUCHUKULIWA HATUA NA KINAMALIZIKA TAREHE 05.01.2013. ANATAHADHARISHA USALIMISHAJI UYALENGE MAENEO YALIYOSALAMA ZAIDI TOFAUTI NA ILIVYO KUWA KWA SILAHA HII KWA KUWA SILAHA INAWEZA KUANGUKIA KWA WATU WASIOWEMA.

WILAYA YA CHUNYA - TAARIFA YA KUPATIKANA KWA RISASI ZA SMG
MNAMO TAREHE 12.12.2012 MAJIRA YA SAA 15:00HRS HUKO KATIKA HIFADHI YA LUKWATI ILIYOPO KATIKA KIJIJI CHA BITIMANYANGA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA . DAIMON S/O JOHN, MIAKA 32, MNYAMWEZI, ASKARI MGAMBO MKAZI WA BITIMANYAGA AKIWA KWENYE DORIA YA KUDHIBITI MAJANGIRI KATIKA PORI HILO NA ASKARI MGAMBO WENZAKE WAWILI WALIMUONA MTU MMOJA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE JINSIA MWANAUME AMBAYE ALIWAKIMBIA NA KUTOKOMEA PORINI BAADA YA KUTUPA KIFURUSHI KIMOJA AMBACHO NDANI YAKE KULIKUTWA RISASI 114 ZA SMG, NGUO NA REDIO MOJA NDOGO AINA YA AITKENSON AMBAYO JUU IMEANDIKWA JINA LA MBOGE. MBINU NI KUKIMBIA NA KUTELEKEZA KIFURUSHI HICHO BAADA YA KUWAONA ASKARI MGAMBO HAO. MTUHUMIWA ANADHANIWA KUWA NI MUWINDAJI HARAMU.KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOMILIKI SILAHA BILA YA KIBALI KWANI NI KOSA LA JINAI.AIDHA ANATOA RAI KWA MTU/WATU WENYE TAARIFA JUU YA ALIKOJIFICHA MTUHUMIWA HUYO AZITOE KWA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.

Signed By,
[  DIWANI ATHUMANI – ACP  ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger