Home »
» ALIYEUAWA MBEYA JK AMTUMA KAKA YAKE MAZISHI YA OFISA USALAMA ALIYEUAWA MBEYA
ALIYEUAWA MBEYA JK AMTUMA KAKA YAKE MAZISHI YA OFISA USALAMA ALIYEUAWA MBEYA
|
MAZISHI ya aliyekuwa ofisa Usalama wa
Taifa (mstaafu) mkoa wa Mbeya RSO Joseph Nelson Mwasokwa, aliyeuwawa usiku wa
kuamkia Desemba 9, mwaka huu Jijini Mbeya, yamefanyika katika Kijiji cha Ibungu
wilayani Kyela mkoani Mbeya.
Marehemu pia alikuwa mwanachama wa Timu ya soka ya Yanga.
Mbunge
wa Jimbo la Mbeya Mjini Ndg. Joseph Mbilinyi(kushoto) na Mwenyekiti wa
Mtaa wa Block T Ndg. Majembe(kulia). Mtaa wa Block T ndiko alikokuwa
akiishi marehemu.
|
|
Kaka wa rais Kikwete Selemani Kikwete akinigia wilayani kyela kwenye mazishi ya marahamu mzee mwasokwa |
|
Aliyekuwa mkuu wa mkoa mbeya Mwakipesile akiongea na mzee Mwambulukutu kwenye mazishi ya marehemu Mwasokwa |
|
Waombolezaji
Katika mazishi hayo, Rais Jakaya Kikwete aliwakilishwa na kaka
yake Selemen Kikwete ambaye pia alipata nafasi ya kutoa pole kwa waombolezaji
ambao hawakuruhusiwa kuuona mwili wa marehemu bali kilichoruhusiwa kuangaliwa
ni picha yake iliyokuwa juu ya jeneza.
Mbali na Seleman Kikwete, viongozi mbalimbali nwalihudhuria
msiba huo akiwemo Mkurugenzi mkuu wa idara ya usalama wa Taifa Tanzania Ndugu
Othuman, aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Mbeya mstaafu John Mwakipesile na viongozi
kadhaa waandamizi wa Serikali.
Marehemu Mwasokwa akatwa na kitu chenye ncha kali kisogoni
ambako wauaji ambao hawajajulikana walifanya kitendo hicho kisha kuulaza mwili
wake kifudifudi nje ya geti la nyumba yake eneo la Block T jijini Mbeya.
Taarifa za Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, zimesema kuwa wauaji
wanaonekana kuwa walitumia panga ambapo marehemu alikutwa na majereha makubwa
sehemu za shingoni, kichwani, mabegani na mkono wa kushoto.
Kwa hisani ya Kalulunga
|
0 comments:
Post a Comment