Pages


Home » » CCM MBARALI YACHARUKIA VIONGOZI WASIOWAJIBIKA.

CCM MBARALI YACHARUKIA VIONGOZI WASIOWAJIBIKA.

Kamanga na Matukio | 02:16 | 0 comments
Mwnyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya Bwana Mathayo Lauren Mwangomo, amesema kuwa wakati wakubezwa kwa chama hicho kwa sasa haupo  kutokana na kujisogeza kwa wananchi ili kupata changamoto zao.

 Ameyasema hayo katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Desemba 17 mwaka huu katika Kijiji cha Ruiwa wilayani humo.

Bwana Mwangomo amesema kuwa CCM imefanya mambo mazuri katika jamii ikiwa ni pamoja na kujenga shule za msingi na sekondari za kata, ambazo zimekuza kiwango cha elimu nchini ikiwa wapinzani wamekuwa wakibeza mafanikio hayo.

Pia amewataka wananchi kutokubali maneno ya uchochezi ambayo yamekuwa yakidhoofisha maendeleo  na juhudi za serikali  katika kutatua matatizo mbalimbali  na kwamba katika kuleta kasi hapakosi matatizo.

Katika Mkutano huyo Mwenyekiti huyo alipokea kero za wananchi wa kata ya Ruiwa ikiwa ni pamoja na ubadhilifu wa fedha zaidi ya shilingi milioni 60 zilizochangwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Gwili ambazo zinadaiwa kufunjwa na Diwani wa kata hiyo Bwana Alex Mdimilage ambapo alimtorosha mhasibu  wa shule hiyo  na kutoroka na fedha za wananchi zaidi ya milioni 27 na kuiacha shule hiyo ikiwa haina chochote.

Kwa upande mwingine pia wamedai kuwa diwani huyo amekuwa kikwazo cha maendeleo ya kata hiyo na kutokana na uwajibikaji wake mbovu umepelekea wananchi wengi kukihama chama hicho.

Hata hivyo Diwani Mdimilage amekanusha tuhuma hizo na kudai kuwa mambo yote yanayozungumzwa dhidi yake ni chuki  za kisiasa na kwamba kwa kipindi chake hiki amesimamia miradi mbalimbali kijijini hapo na kata kwa ujumla.

Bwana Mwangomo amekiri kuwepo kwa viongozi wazembe katika  maeneo wilayani humo, hivyo amewataka viongozi wanaohusika  na tuhuma hizo kujiengua  mapema na hawatasubiri TAKUKURU na Polisi na kero zote zilizowasilishwa na wananchi atazifanyia kazi.

Katika ziara hiyo Mwenyekiti wa wilaya aliongozana na Geofrey Mwangulu  Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa, Patrick Mwaisomba(Mchumi wa Wilaya), Frank Mwashikumbulu ambaye ni mjumbe wa Halmashauri ya wilaya.


Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger