Pages


Home » » KADA WA CHADEMA AUAWA NYUMBANI KWAKE.

KADA WA CHADEMA AUAWA NYUMBANI KWAKE.

Kamanga na Matukio | 01:51 | 0 comments
Kada wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mtaa wa Sogea, Makambini mji mdogo wa Tunduma, Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya ameuawa na mtu au watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jumapili ya Desemba 16 mwaka huu nyumbani kwake.

Uchunguzi wa awali unadai kuwa kuma mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Meneck Kisunga, alienda nyumbani kwa marehemu, ambaye ni balozi wa mtaa huo akidai nyumbani kwake kuna ugomvi na mkewe hivyo kumtaka marehemu kwenda kusuluhisha ndipo marehemu alipofungua mlango alishambuliwa mpaka kuuawa.

Aidha Afisa  Mtendaji wa mtaa huo Bwana Osea Kabula amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na baadae alimtaarifu Mwenyekiti wa Mtaa huo Bwana Ally Mwafongo na hatimae kutoa taarifa kwa Jeshi la polisi Tunduma ambao walifika eneo la tukio kwa uchunguzi zaidi.

Mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hili na mazishi yamefanyika Desemba 17 mwaka huu katika makaburi ya Tunduma.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger