Na Ester Macha.
WANAWAKE Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya wametakiwa kuwa na
daftari la kumbu kumbu la biashara
ambazo wanazifanya kila siku ili liweze
kuwapa tathimini ya biashara wanazofanya
ambayo itawasaidia kusonga mbele kimaisha na kuachana na dhana ya kuwa tegemezi kwa waume zao.
Imeelezwa kuwa baadhi ya wanawake wamekuwa wakishindwa kuwa
na tathimini nzuri nzuri ya fedha zao za biashara kutokana na kuwa na nidhamu
mbaya ya matumizi ya fedha wanazozipata katika biashara zao.
Kauli hiyo imetolewa jana wakati wa Kongamano la mwanamke
jitambue lilofanyika katika ukumbi wa Chinga Wilayani
Mbarali ,na Mwakilishi wa Shirika la Elimisha ambalo linajishughulisha na masuala
ya watoto yatima,wanawake, pamoja na watoto wanaoishi katika mazingira magumu
Bw. Festo Sikagonamo wakati wa
kuwasilisha mada ya ujasiliamali kwa wanawake.
Bw. Sikagonamo alisema kuwa kitendo cha wanawake
wajasilimali waliopo mijini na vijijini kuwa na daftari la kumbu kumbu la bidhaa mbali mbali wanazouza kutasaidia
kukuza bishara zao na hatimae kuwa na nidhamu nzuri ya matumizi fedha zao .
“Kwa utaratibu huu ikifika mwisho wa mwezi au mwaka mwanamke ataweza kujua hesabu zake kwa
uhakika kuwa fedha hiyo afanyie kitu
gani cha msingi kwasababu tayari atakuwa kwenye msingi mzuri wa biashara na
atakuwa amepata faida kubwa, na nyie wanawake mliofanikiwa kupata elimu hii ya
ujasiliamali jitahidini kufika maeneo vijijini kuwapa elimu hiyo “alisema Mwakilishi huyo wa Shirika la
Elimisha.
Hata hivyo alisema kuwa Tofauti ya miongoni mwa wanawake nchini wamekuwa hawana kanuni nzuri
za kibiashara kwani katika
matumizi yao ambayo wameweka yanakuwa
hayatoshi hivyo ni jukumu kwa kila
mwanamke kuongeza juhudi ili kufanikisha
kile alichoshindwa lakini si kutoa fedha ambayo hajapangia matumizi.
Kwa upande wa Mratibu wa Kongamano hilo Bibi.Groly Komba
alisema kuwa lengo la kongamano hilo
ni ni kutoa ufahamu kwa wanawake kuhusiana na
masuala ya kijamii na kiuchumi, malezi bora kwa watoto, sheria ya ndoa na mirathi,pamoja
na masuala ya ukimwi ambayo ni maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Hata Hivyo Bibi. Komba alisema kuwa kitu kingine ambacho kilizungumziwa katika kongamano hilo ni suala la uchumi ambalo ni ujasiliamali ,vikoba,
kwa kuweka akiba ikwa kutumia
vikoba hivyo kwa wanawake .
“Lakini pia tumeanza mkakati wa na
mtandao wa wanawake wilayani
Mbarali kwa kuwaweka wanawake pamoja ili kutafuta wanawake wenye taaluma mbali mbali ambao
wataweza kutoa elimu za ujasiliamali kwa wanawake”alisema Mratibu huyo.
Mmoja
baadhi ya wanawake walioshiriki Kongamano hilo Bi . Elizabeth Saro
alisema kuwa kongamano hilo lilikuwa zuri kwani wamejifunza mambo
mengi hasa ujasiliamali, matumizi ya fedha, malezi ya watoto wao.
Aidha alisema kuwa
kongamano hilo limeweza kuwatoa walipo na kufika sehemu fulani kwani
pia wameweza kujifunza suala la maambukizi kutoka mama kwenda kwa mtoto
jinsi ya kijizuia ili mtoto asiweze kuambukizwa na ugonjwa huo.
0 comments:
Post a Comment