Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
*Wawili wauawa na kisha kuchomwa moto akiwemo Askari Magereza.
Askari
magereza Abel Mwakajonga(24) na nduguye Ezekiel Gambi(30) mkazi wa
Ukwile, Kata ya Mlangali Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya, wamefikwa na
mauti siku ya Jumamosi Desemba 8 mwaka huu baada ya kukodi bodaboda
kutoka Mlowo kuelekea Mlangali kwa ajili ya kumkamata mtuhumiwa wa
mauaji Bwana Laiton Ngonya.
Mtuhumiwa
huyo anadaiwa kumuua baba yao marehemu Salumu Gambi, mnamo Novemba 4
mwaka huu na kuzikwa siku inayofuata katika Kijiji cha Chizumbi mpakani
mwa Wilaya ya Ileje na Mbozi .
Kwa
mujibu wa maelezo ya mdogo wa marehemu Ezekia, bwana Godfrey Gambi(26)
amesema kulikuwepo na mawasiliano baina ya simu baina ya Zemu Kayila
ambaye ni dereva bodaboda iliyokodiwa na marehemu hao na Bwana Ngonya,
ambapo baada ya kufika kijijini hapo marehemu walipotaka kumkamata
mtuhumiwa alipiga yowe akidai watu hao(marehemu) ni wezi wa pikipiki
ndipo wananchi walianza kuwapiga kwa vitu vyenye ncha kali yakiwemo
mapanga na visu hadi kuwasababishia mauti.
Wananchi
hao hawakuishia hapo waliwavua nguo na kuwateketeza kwa moto na miili
kuachwa eneo la tukio, huku uongozi wa kijiji hicho kutokuwa na taarifa.
Aidha
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ukwile Bwana Osia Mtawa, amesema baada ya
mauaji hayo alipata taarifa na kisha kutoa taarifa Polisi Wilaya ya
Mbozi ambapo walifika majira ya saa 12:00 jioni na kuichukua miili ya
marehemu hadi Hospitali ya wilaya hiyo kwa ajili ya uchunguzi
uliofanywa na Daktai Makala siku ya Jumapili Desemba 9 mwaka huu.
Mwili
wa marehemu Ezekia Gambi ulifanyiwa uchunguzi majira ya saa 5:43 na
mwili wa Askari Abeli Mwakajonga saa 5:51 na taarifa kukabidhiwa Polisi.
Hata
hivyo ndugu wa marehemu walikabidhiwa miili ya marehemu hao saa nane
baada ya kupata kibali cha Polisi ambapo marehemu Mwakajonga amezikwa
katika Kijiji cha Mbebe wilaya ya Ileje na mwili wa marehemu Gambi
umezikwa Kijiji cha Ukwile wilaya ya Mbozi.
Wakati
huo huo mauaji haya yamekuja siku moja na tukio la kuuawa kikatili kwa
Afisa mstaafu wa Usalama wa Taifa Mzee Joseph Mwasokwa, aliyeuawa nje ya
nyumba yake eneo la Block T mkoani hapa kuwa mashakani licha ya Kamanda
wa Jeshi la polisi mkoani Diwani Athuman kufanya juhudi kubwa ya
kupambana na uhalifu .
Kamanda
huyo ametoa wito kwa yeyote atakayetoa taarifa za kupatikana watu
waliojichukulia sheria mkononi na waliohusika na mauaji ya Afisa Usalama
ili kufanya mkoa kuwa na hali ya amani na utulivu.
0 comments:
Post a Comment