Na Ezekiel Kamanga, Mbozi.
Simon Mwambene(45) Mkazi wa Kijiji cha Matula, Mbozi Mission Kata ya Magamba Wilaya ya Mbozi, Mkoani Mbeya, ameuawa na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi alipokuwa lindo.
Marehemu ambaye alikuwa ni mlinzi wa binafsi na alikuwa analiza maduka 9 yaliyopo kijijini hapo na aliuawa na watu hao Desemba 13 mwaka huu majira ya saa 8:15 usiku.
Maduka hayo yaliyokuwa yakilindwa na marehemu yalikuwa yanamilikiwa na Bwqana Frank Tenson, Mgala, Tweve, Sosten Kibona, Raphael Kisunga, Kamika Simbeye, Crispin Ndabila, Gody Mahenge, Anthon Mwazembe na Samwel Ndabila.
Marehemu Mwambene alianza kulinda maduka hayo kwa mkataba kuanzia Desemba 3 mwaka 2011 ambapo hadi mauti yanmkuta alikuwa amefanya kazi kwa miezi 22, lakini kabla ya mauti hayo marehemu inadaiwa kuwa Desemba 12 mwaka huu majira ya saa mbili usiku alikuwa na ugomvi baina yake na mkazi mmoja Bwana Ezekia Sindwani. Ugomvi huo ulidumu kwa dakika sita na bwana Sindwani kudai hadharani kuwa atamfanyizia marehemu.
Aidha Bwana Sindwani akiwa na wenzake wanne Desemba 13 mwaka huu, majira ya saa 8:15 usiku walimvamia marehemu wakiwa na vitu vyenye ncha kali walimpiga hadi kusababisha kifo chake papo hapo.
Baada ya kutenda tukio hilo la kikatili walivunja maduka hayo na kuiba mablanketi matano yenye thamani ya shilingi 37,500, vocha mia moja zenye thamani ya shilingi 100,000, mashuka matatu yenye thamani ya shilingi 20,000, Bia tatu za shilingi 6,000 vyote hivyo vikiwa na thamani ya shilingi 243,500.
Hata hivyo katika uchunguzi wa awali unaonesha kuwa Bwana Sindwani ni mzoefu katika vitendo vya kihalifu kama vile mwaka 2011 alituhumiwa kumuua Richard Nyemba, na mwaka 2000 alimuua Emmanuel Msongole.
Mpaka sasa Polisi Mkoani Mbeya wamefanikiwa kumtia nguvuni mshukiwa huyo na watu wanne wametoroka kusikojulikana.
0 comments:
Post a Comment