Mwandishi wa habari kutoka Kituo cha redio kinachofahamika kutoka Nyanda za Juu Kusini Bomba FM na Blogu ya Kamanga na Matukio Ndg. Ezekiel Kamanga akishuka katika ndege katika uzinduzi wa uwanja huo wa Ndege wa kimataifa uliopo Songwe Mkoani Mbeya. |
Brandy Nelson,Mbeya
HATIMAYE Ndege ya kwanza ya abiria imetua
katika Uwanja wa kimataifa wa Songwe rasmi leo baada ya miaka 11 ujenzi
wake ambao tayari umekamilika na
kugharimu kiasi cha sh.100 bilioni.
Akizungumza baada ya
kutua ndege hiyo Kaimu Mkurugenzi wa
malamalaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA) Seleman Seleman alisema kuwa tayari uwanja wa
kimataifa wa Songwe umekamilika na dunia nzima inataarifa ya kukamilika kwa uwanja huo.
Alisema kuwa kutokana na kukamilika kwa uwanja huo tayari
ofisi za mamalaka hiyo imeshahamia katika uwanja huo na kuanza shughuli zake
rasmi leo ambapo uwanja wa zamani
umefungwa rasmi hakuna ndege yoyote itakayoweza kutua katika uwanja huo.
“Kimeanzisha historia mpya kwani dunia inafahamau kwa asasa
kwamba uwanja wa kimataiafa wa Songwe upo wazi umekamilika na umeanza kutumika
rasmi leo”alisema
Alisema kuwa Uwanja wa songwe wa kimataifa ni kati ya
viwanja vikubwa viwili kujengwa baada ya uhuru ukitanguliwa na uwanja wa mkoa wa Kilimanjaro kwani viwanja vingine
vimekuwa vikifanyiwa marekebisho.
Kwa upande wake kaimu mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mkuu wa Wilaya
ya Chunya Deodatus Kinawiro alisema aliwataka wananachi wa Mkoa wa Mbeya
kujiandaa kutumia uwanja huo kwa kuongeza kipato chao na kuinua uchumi wa Mkoa.
Alisema kuwa Wakazi wa Mbeya wanaopaswa kuzalisha kwa wingi maua na matunda ili
kutumia vizuri uwanja huo ili uchumi wa mkoa uweze kukua “tusiutumie uwanja huu
kwa lengo la kusafiria pekee”alisema
“Uwanja wa Songwe ni fulsa muhimu kwa wakazi wa mkoa wa Mbeya na mikoa jirani
kwani utaweza kuwasaidia katika kuongeza pato la mtu mmoja mmoja na taiafa kwa
ujumla kutokana na uwanja huo kuwa wa kimataifa ambapo shughuli mbali mbali za kiuchumi zitafanyika kutokana na uwanja huo”alisema
0 comments:
Post a Comment