Na Esther Macha, Mbeya
WATANZANIA
wametakiwa kuacha kumtafuta mchawi wa hali duni ya maisha yao na
kulalamika hali duni ya maisha na badala yake wawe wabunifu,wajitathmini
na kufanyakazi kwa bidii na maarifa ili waweze kujipatia kipato na
maendeleo ya familia,jamii na taifa kwa ujumla.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw.Abbas Kandoro wakati
akifungua mkutano wa mashauriano juu ya malengo nane ya melania katika
ukumbi wa paradise,jijini Mbeya ambapo wadau kutoka mikoa ya
Ruvuma,Rukwa,Njombe,Katavi na Mbeya walishiriki mkutano huo.
Aidha
Bw. Kandoro ametoa maoni yake kuwa endapo kila mtanzania atajituma
katika kutafuta maisha na kuzitumia fursa zinazomzunguka,akaacha kuwa
mnung’unikaji wa hali ngumu ya maisha huku amekaa kijiweni,akaacha
kumtafuta mchawi kwa kila linalomsibu,akawa mchangiaji katika
kuhakikisha hali ya utulivu na amani inadumishwa kwa kuheshimu misingi
ya utawala bora,kasi ya kuliendeleza taifa itakuwa kubwa.
"Kwa
sasa bado tunaongea sana, ‘we are talking a lot,’ninaamini mkusanyiko
huu utasaidia sana kufanya tathmini ya pamoja kujuwa tulikotoka,tulipo
na tunakokwenda,ninaipongeza serikali kuteuwa Taasisi ya utafiti katika
Nyanja za uchumi na jamii (ESRF) ifanye kazi ya kukusanya maoni ya wadau
mbalimbali,"alisema .
Alisema
utekelezaji wa malengo ya millennia kwa Tanzania unatofautiana kila
Mkoa na Wilaya na ametolea mfano kwenye eneo la Ukimwi,Mkoa wa Mbeya una
asilimia 9.2 kwa takwimu za mwaka 2008 wakati kitaifa ni asilimia
5.7,kupunguza umaskini kitaifa imetokea asilimia 39 kwa mujibu wa
takwimu za mwaka 1990 hadi asilimia 33.6 kwa takwimu za mwaka 2007.
Mkuu
huyo wa Mkoa pato la mkazi wa Mbeya kwa siku ni dola 1 hadi 1.5 kwa
mujibu wa takwimu za mwaka 2010 ambapo katika elimu ya msingi na
Sekondari ukiangalia katika uwiano wa Ke na Me wamevuka lengo kama nchi
kwa asilimia 101 na 205 na kwa Mkoa wa Mbeya ni asilimia 102 na 88
ambayo kwa ujumla haijavuka lengo.
Aidha
alisema lazima kukiri kuwa bado kuna changamoto katika kutokomeza
umaskini wa kipato,njaa,kuboresha afya ya uzazi na huduma za maji salama
pamoja na elimu.
Mkuu
wa Mkoa huyo alisema kupitia warsha kutoka katika mikoa yote Tanzania,
anao uhakika,ushauri na mapendekeo ya washiriki kuhusu kuamua nini
kifanyike kwa siku zijazo baada ya 2015 ni muhimu sana.
Naye
Dkt.John Mduma mwezeshaji ambaye ni Mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Dar
es salaam alisema lengo la mashauriano hayo ni kutoa kichocheo cha
mjadala wa wadau mbalimbali,kujenga taswira ya kimataifa ya hali ya
baadaye kwa mapendekezo madhubuti,kuhakikisha na kusikika sauti za
maskini na wasio sikika,kutambua na kuchambua masuala yatakayoathiri
maendeleo,kushawishi mchakato ndani ya serikali kuu ioane na taasisi na
matokeo yanayotarajiwa.
Bw.John
kajiba ,Mtafiti kutoka taasisi ya utafiti wa mambo ya uchumi na jamii
(ESRF-Economic and Social Research Foundation) alisema taasisi hiyo
imeombwa kusimamia majadiliano hayo kwa kushirikiana na Ofisi ya rais
tume ya mipango katika kanda saba na hasa katika maeneo ya Serikali za
mitaa,Asasi za kiraia,watoto,wazee na wanawake wadogo.
Disemba,4,2012
kumefanyika tukio muhimu na la kihistoria kwa taifa la Tanzania
kutokana na kuwa miongoni mwa nchi 50 kati ya 189 zilizochaguliwa
kujadili,malengo hayo nane ya millennia katika kanda saba ambazo mahali
yalipofanyika katikamabano ni kanda ya Ziwa (Mwanza),kanda ya kaskazini
(Arusha),Kanda ya kati(Dodoma),kanda ya nyanda za juu (Mbeya),kanda ya
kusini(Mtwara),kanda ya magharibi (Shinyanga) na kanda ya mashariki
(Morogoro).