Timu ya
wataalamu wa halmashauri ya Wilaya ya Momba, wamependekeza Mkoa mpya
utakaogawanywa na serikali upewe jina la Momba, ukijumuhisha Wilaya ya
Momba, Mbozi, Ileje na Chunya huku makao makuu yakiwa Vwawa.
Pendekezo
hili wamelitoa jana, kwenye kikao cha Kamati ya ushauri kilichofanyika katika
ukumbi wa mikutano uliopo eneo la Ukwile Wilayani Mbozi kutokana n kutokamilika
kwa baadhi ya miundombinu ya wilaya ya Momba.
Kikao
hicho kilichokuwa kikijadili maendeleo ya Wilaya kiliendeshwa na Mkuu wa Wilaya
ya Momba, Abiudi Saideya na kwamba Mkoa wa Mbeya utabaki kama ulivyo huku
ukiunganisha Wilaya ya Mbeya, Kyela, Rungwe na Mbarali.
Aidha,
mapendekezo hayo yamekuja ni baada ya Rais wa Jamuhuri ya Muunganano akiwa
Mkoani Mbeya kwenye sherehe za mei mosi kuridhia ombi la serikali kuugawa Mkoa
wa Mbeya kutokana na ukubwa wa eneo za mraba zilizopo.
Wakitoa
mapendekezo yao baadhi ya wajumbe, walisema kuwa Wilaya ya Momba inavivutio vya
kiutalii, idadi ya watu, mazao ya chakula na biashara kama vile ufuta, kahawa,
mahindi, mpunga pamoja na uoto wa asili.
“Momba
ndio kitovu cha barabara kuu iendayo nchi za kusini mwa Afrika endapo utapewa
hadhi ya Mkoa utaongeza kipato kupitia ushuru wa forodha kwa nchi za kusini mwa
afrika,”alisema Saideya
Pia,
kikao hicho kilitumia nafasi hiyo kutoa onyo kwa baadhi ya wananchi ambao
wamekuwa wakijichukulia sheria mkononi na kusababisha vifo vya watu kutokana na
vitendo vya kishirikina ambavyo vimetajwa kukithiri katika Wilaya hiyo.
Saideya,
aliwataka waganga wa kienyeji ambao wanashughulika na upigaji wa ramli kuacha
mara moja kwani wao ndio chanzo cha mauaji hayo.
Alisema,
waganga wanapopiga ramli huwataja baadhi ya watu kwamba ndio wamesababisha kifo
cha mgonjwa Fulani hivyo kupelekea watu kutengeneza uadui hadi kufika mahala
wananchi kujichukulia sheria mkononi kwa kuondoa uhai wa watu hao wanaotajwa na
waganga.
“Hivi
karibuni katika kijiji cha Msangano, watu watatu walizikwa wakiwa hai kutokana
na ramli hizi za waganga jambo linalotia dosari Wilaya ikiwa na kudumaza
maendeleo kwani watu wanaogopa kuwekeza biashara zao,”alisema
Hata
hivyo, Mkuu huyo aliwataka wakazi wa eneo hilo kujenga tabia ya kutunza chakula
hasa kwenye msimu huu wa mavuno kwani kumekuwepo na dalili za nje kutokana na
hali ya ukame inayoendelea Wilayani humo.
Picha na Ezekiel Kamanga
|