Wananchi kutoka vijiji vya Ilembo, Pashungu , Italazia, Masoko Shola Izuo na Igale kutoka wilaya ya Mbeya vijiji wakiwa mbele ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wakiwa wamekodo Lori picha ya chini kufikisha Kero zinazowakabili.
Gari hili walilikodi kwa shilingi Laki tatu kusafiri mpaka kwa Mkuu wa wilaya kupinga Serikali kumteua mnunuzi mmoja tu kununua pareto, kuuzwa kwa bei ya chini ambayo inaunzwa kwa shilingi 1,800/= za Kitanzania kwa kilo, hali wengine wakiwa tayari kununua kwa shilingi 2,500/= za Kitanzania.
Wananchi wakiwa ndani ya Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya tayari kuwasilisha Kero zao kwa Mkuu wa wilaya hiyo.
Mkutugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mbeya Bi Juliana Malange
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Bwana Evans Balama(kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbeya maarufu kama Ndomboro.
Mkuu wa Wilaya akizisikiliza kero za wananchi hao
Hawa ni baadhi ya Wanunuzi wa Pareto waliozuiliwa kununua Mazao hayo. Nao hawakuwa nyuma kufuatilia sakata hilo.
Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mbeya Vijijini akiwa na Mwakilishi wa bodi ya Pareto Bwana Mbeyela
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya Bwana Balama amezipokea kero zao na kuwaahidi kuzifikisha katika ngazi za juu na amewataka wananchi hao kuwa na subira, huku serikali ikiendelea kuufanyia uchambuzi maombi yao.
(Picha zote na Kamanga na Matukio, Mbeya Yetu, Chimbuko Letu na Latest News Tz)
0 comments:
Post a Comment