Pages


Home » » GARI LAINGIA DUKANI WAKATI WAKIFUKUZWA NA TRA MBEYA.

GARI LAINGIA DUKANI WAKATI WAKIFUKUZWA NA TRA MBEYA.

Kamanga na Matukio | 05:41 | 0 comments

Na Ezekiel Kamanga.

Binti Oliva Myamba (20) akipewa pole na wananchi waliokuwepo eneo la tukio baada ya gari hilo hapo juu kupoteza mwelekeo na kuingia katika duka alilokuwa akiuza eneo la Magege Darajani Jijini Mbeya.

Katika ajali hiyo watu watatu wamenusurika kufa huku wawili wakikimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya matibabu zaidi akiwemo Imelda Alex (22).

Gari lililohusika na ajali hiyo lilikuwa likiendeshwa na dreva wake Edward Seme lenye namba T 978 BAC Canter ambapo mmiliki wa gari hilo anaitwa Baraka Songera (32) na dereva wa gari hilo amekimbia huku akimwacha utingo wake Tito Mwangoka(23)

Mmiliki wa nyumba iliyogongwa ametajwa kwa jina la Zawadi Kawena (53) mkazi wa eneo hilo la Magege ambapo Meneja wa TRA mkoa wa Mbeya alipotafutwa na mtandao huu wa www.kalulunga.blogspot.com alisema yupo safarini.


Namba ya gari ya TRA iliyokuwa ikiikimbiza gari hiyo iliyopata ajali iligeza chapchap baada ya kuona dili limekufa..
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger