Pages


WANANDOA WAWILI WAKAZI WA MTAA WA BLOCK T JIJINI MBEYA WASABABISHA KUVURUGIKA IBADA.

Kamanga na Matukio | 06:22 | 0 comments
*Ampiga Mke wake, Mke akimbilia Kanisani.
*Mchungaji aacha Mahubiri na kuamulia Ugomvi,
*Waumini wamfikisha Mume Kituo cha Polisi Mwanjelwa afunguliwa RB na jalada.i.

Imetokea katika Kanisa la Tanzania Assemblies Of God (T.A.G) Mtaa wa Block T jijini Mbeya. Ambapo sakata hilo lilianza nyumbani pale Mme anayejulikana kwa jina la Lusekelo muumini wa Dini ya Kiislamu alipo Mkewe anayefahamika kwa jina la Bahati avae vazi la Khanga ndipo Mwanamke huyo alivyo kaidi na kuvaa Kitenge kitendo kilicho muudhi Mmewe na kuanza kumpiga.

Baada ya kuona kichapo kikizidi Mwanamke huyo aliamua kukimbilia katika Kanisa hilo la Mchungaji Angolwisye Mwasunda akiwa Madhabahuni, hali iliyofanya ibada kuvurugika baada ya Mchungaji na waumini kuamulia ugomvi huondani ya Kanisa hilo takatifu.

Waumini walikuwa na zoezi nzito la kumdhibiti Lusekelo na hivyo kutoa taarifa Kituo kidogo cha Polisi kilichopo Mwanjelwa ambapo alifunguliwa RB hii MWNJ/RB/2630/2011. Haikuishia hapo, Mtuhumiwa aliendelea kuporomosha matusi mazito hali iliyopelekea Mkuu wa kituo cha Polisi hicho kumpeleka mtuhumiwa Lusekelo Kiruo Kikuu cha Ktai kilichopo Jijini Mbeya na kufungualia jalada/faili lenye namba MB/IR/7561/2011 kwa kosa la kufanya fujo kanisani.

MADUKA HAYA NDIO YALIYOVUNJWA ENEO LA INYALA NA KUPELEKEA MWANANCHI WA NNE KUSHIKILIWA NA JESHI LA POLIS KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA MTU MMOJA.I

Kamanga na Matukio | 05:29 | 0 comments
 Duka hili lina milikiwa na Bwana Musa Mwanabeya ambaye ni mmoaja kati ya watu wa nne waliomuuaji kijana moja hakufahamika jina lakini ni mkazi wa Uyole jijini Mbeya.
Hali kadharika na hili linamilikiwa na Bwana Musa Philemon ambaye naye ni Muuaji.
 Na hili linamilikiwa na Bwana Japhet Walenjela ambaye naye ni muuaji
*Watu wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mbeya.
*Hali hiyo ndio iliyopelekea wananchi 11 kati ya 1200 wanashikiliwa na Jeshi la polisi  kufanya maandamano bila kibali siku ya Jumapili asubuhi na Polisi kufanikiwa kuwatawanya watu wengine kwa kutumia Mabomu ya machozi  

SERIKALI JIJINI MBEYA TAZAMENI HILI JAMANI KUNUSURU MAGONJWA YA MLIPUKO NA AMBUKIZI

Kamanga na Matukio | 05:10 | 0 comments
Dampo hili ni hatari kwa wanafunzi kwani lipo jirani na Shule ya Msingi Mwenge, eneo la Soweto jijini Mbeya kwani watoto wamekuwa wakikusanyika na kuokote mazagazaga kibao kama Nyembe ambazo huokota kwa ajili ya kukatia kucha na kuchongea Penseli, Nywele na Masalia ya vyakula.

Eneo hili ki ukweli limekithiri kwa uchafu haifahamiki takataka huzolewa saa ngapi kwani wakati wowote ukipita hakuna unafuu.

BREAKINGNEWSSSSSS....... AMPIGA MKE WAKE. NA MKE KUKIMBILIA KANISANI NA KUSABABISHA IBADA KUVURUGIKA

Kamanga na Matukio | 05:30 | 0 comments
Imetokea katika Kanisa la Tanzania Assemblies Of God (T.A.G) Mtaa wa Block T jijini Mbeya, Mchungaji aacha Mahubiri aamulia ugomvi. Washarika waamua kumpeleka Kituo cha Kati cha Polisi Mwanamke awashukuru waumini kwa kumuokoa.

UNYAMA HUU MBEYA MPAKA...................??

Kamanga na Matukio | 05:24 | 0 comments
 Marehemu NASIB EXZAVERY maalufu kama Mkemia akiwa amechomwa moto eneo la viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge Jijini Mbeya kwa kosa la wizi wa kuku ambaye Mwenye Kuku huyo hajafahamika.

 Marehemu NASIB pamoja na Kuku waliodaiwa kuwaiba na kumsababishia kifo.
 Inasikitisha sana
 Jeshi la Polisi likiwa limefika eneo la Tukio kuuchukua Mwili wa marehemu na kuupeleka katika hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya
 Gari hili ndilo linalodaiwa kuwa marehemu alikuwa akifanya kazi kama Utingo.
Watoto wa shule ya Msingi Mwenge wakiwa eneo la Tukio.

ALIYEIBA SIMU ATOZWA FIDIA NA SIMU YAACHA KULIA TUMBONI

Kamanga na Matukio | 05:08 | 0 comments
 Simu iliyoibiwa
 Mama mzazi Bi CHRISTINA MWAKALONGE
 Mwenyekiti wa Mtaa Bwana ASIFIWE MWAKALONGE
Kaka wa muhanga wa tukio hili Bwana DANIEL MWASYOGE
Mwenye simu aliyejulikana kawa jina la Japhet Muhabe mkazi wa Mbalizi amepokea fidia ya shilingi elfu 60,000/= kutoka kwenye familia ya Mwasyoge na kuichukua simu yake  aina ya HUAWEI yenye thamani ya shilingi 25,000/= hivyo simu kuacha kulia tumboni kwa mtuhumiwa wa wizi wa simu hiyo RICHARD GODSON mwenye umri wa miaka 27, mkazi wa Pipe Line na tumbo lake limerejea katika hali ya kawaida.  

WATU 11 WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA KWA KOSA LA KUFANYAMAANDAMANO BILA KIBALI

Kamanga na Matukio | 04:54 | 0 comments
 Wananchi wa kijiji cha Inyara wilaya ya Mbeya vijijini walifunga njia baada ya Maandamano siku ya jumapili kushinikiza Jeshi la polisi kuwaachia huru wananchi nne wanaotuhumiwa kwa mauaji ambao ni Musa Mwanabeya, Musa Philemon, Japhet Walenjela na Mwashinga Lazima,
Jeshi la Polisi katika Maandamano hayo linawashikilia watu Kumi na mmoja wakiongozwa na Bwana SAMWELI TARIANI mwenye umri wa miaka 50 kwa kosa la kufanya maandamano bila kibali.

BREAKING NEWSSSSS:- BAADA YA KUIBA SIMU, IKIPINGWA SIMU YAITA TUMBONI

Kamanga na Matukio | 06:01 | 0 comments
 Kijana mmoja mkazi wa kitongoji cha DDC Mji mdogo wa Mbalizi wilaya ya Mbeya, Mkoani Mbeya Bwana GOODSON MWASYOGE amejikuta yupo katika wakati mgumu baada ya kuiba simu ya mfanyabiashara eneo hilo baada ya wiki moja simu hiyo imekuwa ikilia tumboni baada ya kupigwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa Bwana ASIFIWE MWAKALONGE amethibitisha kwa tukio hilo akiwa sambamba na mjumbe Bwana MOHAMMED SAID.

Wakati huo huo Kaka wa muhanga wa tukio hili Bwana DANIEL MWASYOGE akiwa na Mama mzazi Bi CHRISTINA MWAKALONGE amemtaka aliyeibiwa simu kumsamehe kijana wao kwa kosa alilolifanya naye amekiri kutenda tukio hilo na anaomba msamaha kuwa abilisi alimpitia tuu hakuwa na tabia ya wizi na baadhi ra wananchi wa mtaa huo wanashangaa.

Kijana GOODSON ni mmoja wa wafanyakazi wa Machinjioni maarufu kama Butchery Mbalizi na simu ikiita basi tumbo hilo huvimba baada ya dakika kumi mara baada ya kuita.

WAKULIMA WA PARETO NA KAHAWA WILAYA YA MBEYA WAUONA UONGOZI WA WILAYA NA MKOA KUTAFUTIWA UFUMBUZI WA KIABIASHARA

Kamanga na Matukio | 05:50 | 0 comments
 Wananchi kutoka vijiji vya Ilembo, Pashungu , Italazia, Masoko Shola Izuo na Igale kutoka wilaya ya Mbeya vijiji wakiwa mbele ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wakiwa wamekodo Lori picha ya chini kufikisha Kero zinazowakabili.
 Gari hili walilikodi kwa shilingi Laki tatu kusafiri mpaka kwa Mkuu wa wilaya kupinga  Serikali kumteua mnunuzi mmoja tu kununua pareto, kuuzwa kwa bei ya chini ambayo inaunzwa kwa shilingi 1,800/= za Kitanzania  kwa kilo, hali wengine wakiwa tayari kununua kwa shilingi 2,500/= za Kitanzania.
 Wananchi wakiwa ndani ya Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya tayari kuwasilisha Kero zao kwa Mkuu wa wilaya hiyo.
Mkutugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mbeya Bi Juliana Malange 
 Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Bwana Evans Balama(kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbeya maarufu kama Ndomboro.
 Mkuu wa Wilaya akizisikiliza kero za wananchi hao
Hawa ni baadhi ya Wanunuzi wa Pareto waliozuiliwa kununua Mazao hayo. Nao hawakuwa nyuma kufuatilia sakata hilo.
Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mbeya Vijijini akiwa na Mwakilishi wa bodi ya Pareto Bwana Mbeyela 

 Hata hivyo Mkuu wa Wilaya Bwana Balama amezipokea kero zao na kuwaahidi kuzifikisha katika ngazi za juu na amewataka wananchi hao kuwa na subira, huku serikali ikiendelea kuufanyia uchambuzi maombi yao.

(Picha zote na Kamanga na Matukio, Mbeya Yetu, Chimbuko Letu na Latest News Tz) 

UCHAGUZI WA AWALI WA KUWAPATA WACOMBEA WA UDIWANI CCM KATA YA NZOVWE WAKAMILIKA

Kamanga na Matukio | 05:12 | 0 comments
Harakati za awali kuelekea kupata wagombea wa udiwani katika uchaguzi mdogo katika Kata ya Majengo na Nzovwe jijini Mbeya kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) zinaendelea vizuri baada ya chama hicho kukamilisha uchaguzi wa awali wa wagombea.

Akizungumza na mwandishi wetu Katibu wa CCM Wilaya ya Mbeya Mjini Bi.Bahati Makalanzi amesema kura za maoni za Kata zimeshafanyika na kwamba wagombea wote watajadiliwa ili kupitishwa katika vikao vya halmashauri ya mkoa.

Ameongeza kuwa kata ya Majengo ilikuwa na wagombea 6 ambao walikuwa wakiwania nafasi ya kukiwakilisha chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi mdogo ambapo SAMUEL MWAMBONA alipata kura 188 DAUSEN MSHILU kura 48 HASSAN MWALUKINDI kura 28 JOSEPPH MWAMBAPA kura 28 FILIMON MWAISOLEKA kura 12 na RAISON MWASEMBO kura 7.

Kwa upande wa kata ya Nzovwe wagombea walikuwa watano ambapo ISAAC SINTUFYA alipata kura 127 GENNER MWAIJANDE kura 96 LUCIUS LUOGA kura 60 FRED MWAKATENYA kura 41 na KELLY SICHONE kura 3.

Kampeni za uchaguzi mdogo kwa ajili ya kuziba nafasi ya madiwani wa kata hizo zitafanyika kwa muda wa siku 21 ambapo zitaanza septemba kumi na uchaguzi kufanyika octoba pili mwaka huu.

SHILINGI 10,000/= ZA KITANZANIA FAINI KWA MWANANCHI ATAKAYE ACHA MAENEO YAKE KATIKA HALI YA UCHAFU ILOMBA JIJINI MBEYA.

Kamanga na Matukio | 05:11 | 0 comments
Maafisa mazingira jiji la Mbeya kesho watafanya ukaguzi wa maeneo ya kata ya Ilomba ambapo faini isiyopungua shilingi elfu kumi itatozwa kwa mwananchi ambaye atabainika kuacha maeneo yake katika hali ya uchafu.

Akiongea na mwandishi wetu mmoja wa wafanyabiashara wa maeneo ya Mama John Geofrey Muhema amesema kitendo cha wafanya biashara kufanya usafi katika maeneo yao kinatokana na agizo lilotolewa na uongozi wa halmashauri la kumtaka kila mtu kufanya usafi katika maeneo yao kabla ya agosti 27 ambayo ndiyo itakuwa siku ya ukaguzi.

Hata hivyo amewataka wakazi wa eneo hilo kujenga mazoea ya kufanya usafi katika maeneo yao badala ya kusubiri amri kutoka kwa viongozi wa Serikali.

WATU WATATU WAKAMATWA NA KETE 180 ZA BANGI TUNDUMA

Kamanga na Matukio | 06:17 | 0 comments
Watu watatu wakamatwa na kete 108 za bangi mtaa wa tukuyu wilayani Mbozi, walikamatwa na askari mwenye namba E3843 Kikosi cha upelelezi anayeitwa Greyson na wenzake  wakiwa doria.

Waliokamatwa ni Joshua Mwanange(25) mkazi wa Tukuyu, Frank Simfukwe (19) Mkazi wa Tukuyu Tunduma na Juma  Charles (20) mkazi wa Tukuyu Tunduma wote kwa pamoja wamekamatwa na kete hizo zenye uzito wa kilo gramu 500.

Watuhumiwa wapo mahabusu wilayani Mbozi watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezoi kumilika.

HUU NDIO UKARABATI WA BARABARA ZETU MBEYA BWANA

Kamanga na Matukio | 05:52 | 0 comments
Huku Serikali ikipiga kelele ukosefu wa Pesa baadhi ya wayendaji wametafuta mianya ya kufuja pesa, kwa kukarabati barabara jijini Mbeya Isanga na Meta kwa kumwaga kokoto za milimita 5 bila lami wala saruji hivyo kuhatarisha wananchi wanaoishi eneo hilo kuvunjwa vioo vya nyumba zao baada ya magari kupita kwa kasi kutokana na madhara ya mawe hayo kuruka ambapo yamemwangwa na halmashauri ya jiji.

UTITILI WA MAKANISA MKOANI MBEYA HAYAKATI KIU YA MATUKIO YA UOVU

Kamanga na Matukio | 05:46 | 0 comments
Makanisa kibao kila mtaa Mbeya lakini Vituko vya maavo ni kibao, Kanisa hili lipo karibu na eneo la tukio ambapo KIKONGWE ALALA NA MAITI SIKU 6 AKIDAI ALIKUWA HAJUI LOLOTE, ARIPOTI MSIKITINI KUWA ANADHANI KUNA MAITI NYUMBANI MWAKE!  

Picha kamili hapo angali habari zinazofuata hapo Chini. 

GARI LAINGIA DUKANI WAKATI WAKIFUKUZWA NA TRA MBEYA.

Kamanga na Matukio | 05:41 | 0 comments

Na Ezekiel Kamanga.

Binti Oliva Myamba (20) akipewa pole na wananchi waliokuwepo eneo la tukio baada ya gari hilo hapo juu kupoteza mwelekeo na kuingia katika duka alilokuwa akiuza eneo la Magege Darajani Jijini Mbeya.

Katika ajali hiyo watu watatu wamenusurika kufa huku wawili wakikimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya matibabu zaidi akiwemo Imelda Alex (22).

Gari lililohusika na ajali hiyo lilikuwa likiendeshwa na dreva wake Edward Seme lenye namba T 978 BAC Canter ambapo mmiliki wa gari hilo anaitwa Baraka Songera (32) na dereva wa gari hilo amekimbia huku akimwacha utingo wake Tito Mwangoka(23)

Mmiliki wa nyumba iliyogongwa ametajwa kwa jina la Zawadi Kawena (53) mkazi wa eneo hilo la Magege ambapo Meneja wa TRA mkoa wa Mbeya alipotafutwa na mtandao huu wa www.kalulunga.blogspot.com alisema yupo safarini.


Namba ya gari ya TRA iliyokuwa ikiikimbiza gari hiyo iliyopata ajali iligeza chapchap baada ya kuona dili limekufa..

KIKONGWE ALALA NA MAITI SIKU 6 AKIDAI ALIKUWA HAJUI LOLOTE, ARIPOTI MSIKITINI KUWA ANADHANI KUNA MAITI NYUMBANI MWAKE!

Kamanga na Matukio | 05:36 | 0 comments
 MAANDALIZI YA KUUTOA MWILI WA MAREHEMU



 MASHUHUDA WA TUKIO HILO KATIKA MTAA WA ILOLOMAANDALIZI YA KUUZIKA MWILI WA MAREHEMU
 MAANDALIZI YA KUUZIKA MWILI WA MAREHEMU

 IBADA YA MAZISHI YA MAREHEMU SALEHE
 BAADHI YA WAUMINI WA MSIKITI WA SOWETO WAKINAWA BAADA YA MAZISHI

IMAMU ELIASA SELEMANI WA MSIKITI WA SOWETO JIJINI MBEYA AKIMWOMBEA DUA MAREHEMU KWA MWENYEZI MUNGU 
* Yasemekena aliwahi kumuua mkewe na kufungwa jela miaka 8
· * Wanakijiji wamtaka ahame, Polisi yaingilia kati

KIKONGWE mwenye umri wa miaka 85 aliyefahamika kwa jina la Sadiki Salehe mkazi wa Ilolo kata ya Ruanda Jijini Mbeya amejikuta matatani kufuatia kulala na maiti ya mtoto wake pekee kwa siku sita.

Habari za kuaminika kutoka kijijini hapo zimesema kuwa wakati harufu hiyo ikiendelea kuzagaa eneo la nyumba yake na majirani, Kikongwe huyo alikuwa akiendelea kuandaa futari karibu na mlango wa chumba cha marehemu hasa ukizingatia huu ni mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Mtoto wa kikongwe huyo alijulikana kwa jina la Salehe Sadiki(38) kwa mara ya mwisho alionekana Jumatano ya wiki liliopita(Agosti 17, 2011).

Kikongwe huyo alipohojiwa alisema kuwa Jumatano ya Agosti 24 mwaka huu akiwa nyumbani kwake alikuwa anahitaji dishi la kuogea ambalo lilikuwa katika chumba cha marehemu ambaye alikuwa akiishi nje ya nyumba ambayo ilikuwa ikitizama na ya baba yake umbali wa meta 1.5.
Na mara baada ya kuchukua hatua ya kutaka dishi hilo ndipo alipoenda na kugonga mlango wa chumba cha marehemu na kukuta mlango ukiwa umefungwa huku harufu ikitoka kwa mbali.

Harufu hiyo ilimshtua kikongwe huyo ambaye aliamua kwenda msikiti wa Soweto uliopo Jijini Mbeya kwa Imamu Eliasa Selemani ambaye naye alimtaarifu balozi wa mtaa huo Iddi Malole kuhusu tukio hilo.

Imamu Eliasa na Balozi Malole kwa pamoja walimtaarifu Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilolo Benson Mbwana kuhusu tukio hilo la kushangaza ambaye alimua kutoa taarifa katika kituo cha Polisi Mwanjelwa.

Kituo cha Polisi cha Mwanjelwa kilishindwa kushughulikia suala hilo ambalo lilipelekwa katika kituo cha Polisi cha Kati (CENTRAL POLICE) ambacho kiliruhusu kuzikwa kwa mwili huo ambao ulikuwa umeharibika vibaya kwa kupasuka huku Polisi ikiendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Wakati Polisi wakitoa amri ya kuzikwa kwa mwili huo wakazi wa mtaa huo walipandwa na hasira kufuatia tukio hilo na walisikika wakisema kuwa sio mara ya kwanza kwa mzee huyo ambaye hapo awali alimuua mkewe na kumweka uvunguni mwa kitanda kwa zaidi ya siku nne hali iliyomfanya atumikie kifungo cha zaidi ya miaka 8 jela kutokana sakata hilo.

Polisi walipoona hayo ilimuondoa mzee huyo eneo la tukio kwa nguvu ili kunusuru maisha yake.

Wakati polisi ikiondoka na mzee huyo wakazi hao walisikika wakisema mzee huyu hatakiwi kurudi tena kijijini hapo kutokana na vitendo hivyo licha ya sura yake ya upole aliyonayo na kushinda msikitini.

Aidha Mwenyekiti wa mtaa huo alisema sula hilo sasa limo mikononi mwa Jeshi la Polisi hivyo watalishughulikia ipasavyo.

MGOGORO WA KAPUNGA UNATATULIKA KI URAHISI, SERIKALI INAPASWA KUFANYA JITIHADA ZA HARAKA ILI KULETA MAENDELEO.

Kamanga na Matukio | 05:56 | 0 comments


Meneja uzalishaji wa Kapunga Rice Project Bwana SERGEI BEKKER akielezea ramani ya Mashamba ya Kapunga.

Mpunga unapoanzia.
Na hizi ni Baadhi ya mashine zinazotumika kukoboa Mpunga.
Mashine ambayo hupanga Madaraja matatu tofauti, Daraja I, II na III
Eneo la wazi ambalo halijalimwa na Mwekezaji
Sehemu ya mashamba ya Mpunga yakionekana kwa juu
Sehemu ya shamba ambalo limelimwa na hukodishwa na Mwekezaji kwa Wananchi
Mashine za kuhifanzia Mpunga ambazo zimetoka Ujerumani lakini zimekuwa zikifanya chini ya kiwango ambapo kilitegemewa licha ya kuwa ni msimu wa mavuno ya zao la Mpunga.
Tanki za kuhifadhia Mpunga
Jenereta linalotumika kuendeshea mitambo endapo umeme ukikatika.

Mashine za kuchambua Mpunga kwa madaraja.
Uwanja wa Ndege uliojengwa na Muwekezaji wa Kapunga, ambao unalalamikiwa na wananchi kijiji cha Mapogoro Kapunga wilayani Mbarali mkoani Mbeyakwa madai kuwa umejengwa pasipo ridhaa ya wananchi.
Mwenyekiti wa kijiji hicho cha Mapogoro Kapunga Bwana Ramadhani Nyoni akiwa na mjumbe wa kijiji bwana Bryton Ngela wakionesha ambapo Shule ilivyunjwa na Mwekezaji huyo.
Baadhi ya Masalia ya Majengo ya Shule yaliyobomolewa
Mawe yaliyokuwa yamekusanywa na Wananchi kwa ajili ya Ujenzi washule lakini wameshindwa kuendelea kutokana na Mwekezaji kudai uwanja huo ni mali yake.

Nyumba ya Walimu iliyojengwa na kwa sasa wameshindwa kuendelea kutokana na sakata hilo.
Masalia  ya majengo yaliyobomolewa
Fomula inayotumika kutambua sababu zinazosababisha Nchi nyingi za Kiafrika zisiendelee ambapo kuna Uvivu, Wizi, nidhamu ya kazi, Miundombinu mibovu, Utawala bora, Pia ametoa ufafanuzi kuwa ni bora kutumia ndege ili kuepuka wizi katika zoezi la upandaji wa mbegu na hupunguza gharama badala ya kutumia watu 150 kwa shughuli hizo basi hutumia watu 10.

ZIADA:- Mgogoro huu umechangia kwa kiasi kikubwa Pande zote mbili kuyumba kiuchumi na hivyo serikali inapaswa kutatua tatizo hili kani pande zote mbili zinaitupia lawama serikali. 
 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger