Raisi wa Shirikisho la Vyama vya Soka vya Nchi za Amerika Kaskazini, Kati na Caribbean-Concacaf, Jeffrey Webb amekanusha tetesi kuwa anataka kuchukua kugombea nafasi ya rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA inayoshikiliwa na Sepp Blatter.
Webb
amehusishwa kugombea nafasi hiyo mwaka 2015, huku Blatter akipendekeza katika
mkutano uliofanyika Caribbean Jumatatu iliyopita kuwa Webb anaweza kuchukua
nafasi kuchukua nafasi yake siku zijazo.
Lakini
Webb mwenyewe alikanusha suala hilo akidai kuwa hana mpango wa kugombea nafasi
hiyo katika siku za karibuni.
Blatter
ambaye aiongoza FIFA toka mwaka 1998 alikuwa akizungumza kufungua mkutano wa
mwaka wa Concacaf.
Mwaka
2011 Blatter aliwaambia viongozi wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA kwamba
kipindi hiki kitakuwa cha mwisho kwake kukalia ofisi hiyo lakini mwaka huu
ameonekana kubadili uamuzi baada ya kuonyesha ishara kama anaweza kugombea kwa
kipindi kingine.
0 comments:
Post a Comment