JESHI la Polisi Mkoani Mbeya
linamshikilia Steven Julias mkazi wa Jakaranda kata ya Iyela Jijini Mbeya
akituhumiwa kutelekeza familia kwa miezi mitano bila huduma za msingi ikiwemo
chakula na sare za shule.
Kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo
kumethibitishwa na mwenyekiti wa dawati la Jinsia Mkoa wa Mbeya, Mary Gumbo
ambaye alisema walimkamata Oktoba 11, mwaka huu eneo la nyumbani kwake
alikokuwa amewatelekeza watoto hao.
Aliongeza kuwa mtuhumiwa huyo alikutwa
akiwa anafanya maandalizi ya kuwatorosha watoto hao ili kukwepa mkono wa sheria
dhidi yake baada ya kusikia kwenye vyombo vya habari kuwa anatafutwa kukabili
kesi iliyombele yake.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo alisema
hivi sasa uchunguzi unafanyika ili kesi iweze kufunguliwa na hatimaye
kufikishwa mahakamani ili sheria iweze kuchukua mkondo wake ili vitendo vya
unyanyasaji dhidi ya watoto vikomeshwe.
Wakati huo huo maisha wanayoishi kwa
sasa watoto hao Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) ambao ni wanafunzi
wa darasa la kwanza shule ya msingi Mapambano iliyopo Kata ya Iyela
Jijini Mbeya maisha ya kujipikia bila huduma za msingi wasamaria wema wameombwa
msaada wao wa hali na mali.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti watoto
hao wamesema hivi sasa wanaishi kwa misaada kutoka kwa walimu na baadhi ya watu
ambao huwapa unga na maharage na wao hulazimika kutafuta fedha za kununulia
mahitaji mengine kama mafuta ya kula na taa.
Wametaja baadhi ya mahitaji yao muhimu
kwa sasa kuwa ni pamoja na Sare za shule kutokana na kuchakaa kwa sare
wanazotumia ikiwemo Madaftari, kalamu,Masweta, Viatu, mafuta ya kupikia, mafuta
ya kupaka, sabuni, chumvi, mkaa, Unga, Mchele na maharage.
Aidha
imeshauriwa kuwa kutokana na mazingira wanayoishi watoto hao kutokuwa mazuri
kwa utunzaji wa vyakula ambapo nyumba wanayoishi kutokuwa na mlango vitu hivyo
vihifadhiwe Ofisini Kwa Mwalim Mkuu kama vitapatikana.
Kwa
yeyote atakayekuwa ameguswa na hali ya watoto hao awasiliane na Mbeya Yetu
kupitia namba 0754 374 408
au Bomba Fm redio kupitia 0754 490 752.
Na Mbeya yetu
|
0 comments:
Post a Comment