Meneja
wa zamani wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema David
Beckham alitakiwa kuondoka katika klabu hiyo kwasababu nahodha huyo wa zamani
wa timu ya taifa ya Uingereza alidhani yeye ni mkubwa kuliko meneja.
Katika
kitabu chake kipya kinachoelezea maisha yake ya ukocha, Ferguson amesema
aligombana na Beckham baada ya kumkosoa kwa kiwango chake alichokionyesha
katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Arsenal ambao walipoteza.
Katika
kitabu hicho Ferguson ameandika kuwa dakika ambayo mchezaji wa United
atakapodhani yeye ni mkubwa kuliko meneja ni lazima aondoke na Beckham alidhani
yeye ni mkubwa kuliko Ferguson ndio maana akamuuza.
Ferguson
pia alionyesha wasiwasi wake kuhusu mtindo wa maisha ya watu mashuhuri kufuatia
nyota huyo kumuoa Victoria Adams aliyekuwa nyota wa kundi la muziki la Spice
Girls nchini humo.
Kocha
huyo aliendelea kudai kuwa Beckham ndiye mchezaji pekee kati ya aliyowafundisha
kuchagua maisha ya umaarufu na kitendo hicho hakikumfurahisha ndio maana
akamuacha aondoke.
Lakini
Ferguson alimpongeza nyota huyo kwa mchango wake uliochangia mafanikio mengi ya
United na kumtaja kama kioo cha watoto wote duniani.
Katika
kipindi chote cha miaka 26 aliyofundisha United, Ferguson alishinda mataji 38
na kufanikiwa kuwafundisha nyota kadhaa wakiwemo Beckham, Eric Cantona,
Cristiano Ronaldo, Peter Schmeichel, Bryan Robson, Roy Kean, Jaap Stam na Ruud
Van Nistelrooy.
0 comments:
Post a Comment