WATU watano wamefariki dunia na wengine
22 kujeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka na
kuharibika, baada ya dereva kushindwa kulimudu kutokana na mwendokasi.
Ajali hiyo ilitokea majira ya saa sita mchana katika
Mtelemko wa Mlima Senjele katika Mpaka wa Halmashauri ya Mbeya na Wilaya ya
Mbozi eneo la Songwe Mkoani hapa, wakati gari hilo likitokea Tunduma kwenda
Jijini Mbeya.
Gari hilo lenye namba za usajili T 378
ADR aina ya Toyota Costa lilikuwa likiendeshwa na Dereva Semu Mwakajwanga
anayekadiliwa kuwa na umri kati ya miaka 60 na 70 ambaye alitoweka baada ya
tukio.
Muuguzi mkuu wa Hospitali Teule ya Ifisi
ambako majeruhi wote walipelekwa, Sikitu Mbilinyi alikiri kupokea majeruhi 22
na kusema kati yao Wanaume 8 ambao hali zao zinaendelea vizuri kutokana na
kutoumia sana ingawa wanamichubuko usoni na sehemu za mikono na miguu.
Aliongeza kuwa kati ya majeruhi hao
wanawake 10 walipokelewa wakiwa katika hali ya kuumia sana na kupatiwa matibabu
ambapo kati yao Wanne walipewa Rufaa kutokana na hali zao kutokuwa katika hali
nzuri, wengi wao wakiwa wameumia vichwa na kuvunjika miguu.
Alisema pia kati ya majeruhi hao watoto
ni wanne ambao hali zao zinaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu na
kuongeza kuwa taarifa za eneo la tukio kwamba watu wanne walikufa papo hapo na
mtoto mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka mitano.
Kwa upande wake Kondakta wa basi hilo,
Ulimboka Noah (26) alisema sababu ya kutokea kwa ajali hiyo ni kutokana na
gari kugoma kubalisha gia ambapo dereva alivyojaribui kubadili ilishindikana
ndipo alipojaribu kushuka nalo hivyo hivyo lakini kabla ya kufika darajani
ilikuwa kama kitu kimelichota gari na kupinduka.
Alisema kutokana na jinsi lilivyopinduka
gari hilo inasemekana ni kutokana na kukatika kwa Propela Shafti ambayo
ilijikita chini kasha kupindua gari au U- Bolt inaweza ikawa imeachia kwa kile
alichosema eneo lilikuwa zuri na hukuna kitu kilicholigusa gari hadi
likapinduka.
Bado miili ya marehemu haijatambuliwa na
imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya
Mbeya Ifisi.
Picha na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
|
0 comments:
Post a Comment