Mgombea nafasi ya
uraisi wa shirikisho la soka nchini TFF Jamal Malinzi hii jana amezindua rasmi
kampeni za kuwani nafasi hiyo huku akitoa ahadi ambazo ana hakika atazitekeleza
endapo atapewa nafasi na wajumbe wa
mkutano mkuu mwishoni mwa juma hili.
Jamali
Malinzi ambae anaiwani nafasi hiyo kwa mara ya pili,
baada ya mwaka 2008 kushindwa na raisi anaemaliza muda wake Leodger Chilla
Tenga, amesema soka la Tanzania linahitaji msaada mkubwa ili liweze kufikia
malengo yake pamoja na kuwafurahisha watanzania ambao wana uchu wa mafanikio.
Malinzi
amesema mzizi mkubwa wa maendeleo ya soka nchini unatakia kujikita katika idara
ya ufundi ya shirikisho la soka nchini na kama atapata nafasi ya kuwa raisi wa
TFF atahakikisha idara hiyo inaboreshwa kwa lengo la kuufufua upya mkakati wa
soka kuanzia kwa vijana wenye umri mdogo.
Katika hatua nyingine
Jamali Malinzi akaguzia suala la
mikataba kwa kusema endapo atapewa fursa ya kuliongoza shirikisho la soka
nchini kwa ridhaa ya wapiga kura, atahakikisha kuwa muwazi katika hatua za
kuingia mikataba na makampuni ambayo kwa sasa yanatumia kivuli cha soka
kujinufaisha binafsi pamoja na baadhi ya watu wasiolitakia mema soka la
Tanzania.
0 comments:
Post a Comment