Home »
» MJANE WA MIAKA 60 ANAOMBA MSAADA WA KUTIBIWA MKONO WAKE ULIYOANZA KUHARIBIKA BAADA YA KUJERUHIWA NA NYOKA.
MJANE WA MIAKA 60 ANAOMBA MSAADA WA KUTIBIWA MKONO WAKE ULIYOANZA KUHARIBIKA BAADA YA KUJERUHIWA NA NYOKA.
|
Mwanamke
Mjane FAINES NAMBEYE KAONGA [60] Mkazi wa kijiji cha IGUNDU Kata ya
SANGAMBI Wilaya ya CHUNYA Mkoani MBEYA anawaomba wasamaria kumchangia
pesa kwa ajili ya kupata matibabu baada ya kujeruhiwa na nyoka alipokuwa amelala chumbani kwake. |
|
Hivi ndivyo mkono wake ulivyo kwa sasa |
|
Mwanamke mmoja Mjane aliyefahamika kwa jina la FAINES
NAMBEYE KAONGA [60] Mkazi wa kijiji cha IGUNDU Kata ya SANGAMBI Wilaya ya
CHUNYA Mkoani MBEYA anawaomba wasamaria kumchangia pesa kwa ajili ya kupata
matibabu baada ya kujeruhiwa na
nyoka alipokuwa amelala chumbani
kwake.
Mjane huyo alijeruhiwa mkono wa kushoto na nyoka alipokuwa
amelala chumbani kwake hivi karibuni na kusababisha ngozi kutoka hali
iliyomsababishia maumivu makali ambapo alikimbizwa Hospitali ya Wilaya ya
CHUNYA na kupatiwa matibabu lakini mpaka sasa hali inazidi kuwa mbaya.
FAINES amesema
pamoja na kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya na kuruhusiwa kurudi
nyumbani mkono umezidi kuliwa na sumu na kusababisha ngozi kutoka hadi mfupa
kutokeza nje ya ngozi hali inayomtia hofu siku hadi siku.
Mama huyo hana pesa za kuweza kupata matibabu zaidi kutokana
nayeye kufiwa na mumewe na wanawe hawana uwezo wa kugharamia matibabu katika
Hospitali nyingine hivyo kuwaomba wasamaria wema kumsaidia ili aweze kuokoa
maisha.
Baadhi ya majirani wamesema mama huyo ameumwa na nyoka siku
za hivi karibuni akiwa amelala chumbani kwake na alipopelekwa kupatiwa matibabu
hajapata ahueni na afya yake imezidi kuzorota siku hadi siku hali akishindwa
kufanya kufanya shughuli za kiuchumi
Picha na Ezekiel Kamanga
Kwa atakaeguswa kumsaidia mjane huyu wasiliana
na
0754 49 07 52
AU
0754 37 44 08
|
0 comments:
Post a Comment