Na Ezekiel Kamanga,Chunya.
Wanawake wa halmashauri ya wilaya ya Chunya Mkoani
Mbeya wametakiwa kujihusisha na ujasirimali ili waweze kufikia malengo ya hamsini
kwa hamsini na kuachana na dhana ya
kutegemea wanaume pekee kama ndio
wazalishaji wakuu katika familia.
Haya yameelezwa na mwenyekiti wa UWT wilaya ya
Chunya Mboka Konzo wakati akizungumza na mwandishi wa habari kuhusiana na
mwamko wa wanawake wa halmashauri ya Chunya kujihusisha na shughuli za
ujasirimali ukilinganisha na miaka ya nyuma.
Konzo alisema mwamko wa wanawake kwa halmashauri ya
Chunya kwasasa umekuwa mkubwa ukilinganisha miaka ya nyuma walikuwa wakitegemea wanaume kwa kila kitu
huku wao wakibaki nyumbani waletewe chochote lakini kwasasa wanawake
wanajishughulisha na ujasirimali mdogo
mdogo kama kuuza mboga mboga,mamamntilie na hata kuzungusha matunda.
Aliendelea kueleza kuwa mbali na kuwa na kasi ya
kujihusisha na ujasiriamali wanawake wamekuwa wakiungana katika vikundi vya kukopa
na kurejesha (upatu)ambavyo vimekuwa vikiwawezesha wanawake wengi kujikwamua
kiuchumi.
Aidha wakizungumzia suala la ujasiliamali baadhi ya
wajasirimali wadogo wadogo Esta George na Rehema Charles wanaojihusisha na
uuzaji wa matunda katika stend ya chunya mjini walisema kuwa kwasasa
wanajitambua na kwamba wameamua kujihusisha na ujasiriamali kama njia ya
kusaidiana katika majukumu.
Ambapo waliongeza kuwa licha ya kusaidiana katika
majukumu wanafanya hivyo ili kesho na kesho kutwa mwanaume asipokuwepo waweze
kusimama wenyewe na kuendesha familia zao bila kuteteleza kwani wamekuwa
wakiona wanawake wenzao ambao wamekuwa wakitegemea wanaume jinsi
wanavyohangaika wanapoondokewa na waume zao.
0 comments:
Post a Comment