Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa
na Luteni Mstaafu Chiku Gallawa baada ya kumuapisha kuwa mkuu wa mkoa
mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016.
Na Ezekiel Kamanga, Songwe
Mkuu
wa Mkoa wa Songwe Luten Mstaafu Chiku Galawa ameanza ziara ya
kutembelea Wilaya zote tano za Mbozi Songwe,Ileje,Momba na Songwe ambazo
zinaunda Mkoa wa Songwe ili kujitambulisha kwa wananchi na kupokea
changamoto mbalimbali zinazozikabili wilaya hizo.
Galawa
ameanza ziara katika Wilaya ya Songwe ambapo alipokelewa katika Kijiji
cha Kaloleni Kata ya Mkwajuni na Vijana waendesha Bodaboda walioambatana
na Mbunge wa Jimbo la Songwe Philip Mulugo ambaye ni mlezi wa Vikundi
mbalimbali vya waendesha pikipiki Wilaya ya Songwe.
Mkuu
wa Mkoa Chiku Galawa alipokea changamoto mbalimbali za Jimbo la Songwe
kutoka kwa Mbunge wa Jimbo hilo ikiwa ni pamoja maji,barabara,umeme na
Afya.
Mulugo
amesema kuwa wilaya hiyo mpya ina eneo la kutosha kujenga nyumba za
watumishi wa wilaya hiyo na ofisi mbalimbali pia Asasi ikiwa ni pamoja
na ujenzi wa Benki ya NMB ili kuwaondolea adha wakazi wa Mkwajuni
kutokana na kutokuwepo kwa Taasisi za kifedha.
Kwa
upande wa Mkuu wa Mkoa kabla ya kuwawahutubia wananchi katika uwanja wa
michezo wa Mkwajuni alivikwa uchifu na wazee wa kimila wa kabila la
Kibungu wakiongezwa na Chifu Kazumba ambaye pia alimkabidhi mbuzi mnyama
kama ishara ya upendo na ukaribisho wilayani humo.
Akiwahutubia
mamia ya wakazi wa Mkwajuni Galawa amweshukuru wakazi wa Mkwajuni kwa
maaribisho mazuri na kusema kuwa changamoto zilizopo katika Mkoa wake
mpya zitumikke kama fursa ya kuleta maendeleo katika wilaya hiyo na Mkoa
kwa ujumla.
Amesema
Wilaya ya Songwe ina ardhi nzuri,Ziwa Rukwa na madini mbalimbali ambayo
yatakuwa chachu ya maendeleo kama Dhahabu,makaa ya mawe na madini adimu
duniani yanayotumika kutengezea vifaa vya elekroniki ambayo
yanapatikana katika Kata ya Ngwala.
Galawa
ataendelea na ziara yake katika wilaya za Mbozi Momba,Ileje na Mbozi
ambapo atakuwa na kazi ya kupokea kero kutoka kwa wananchi na kuzipatia
ufumbuzi ili kuleta maendeleo katika Mkoa wa Songwe.
0 comments:
Post a Comment