Mkuu wa Wilaya ya Kalonga, Nchini Malawi Rosemary Kalonga na Mkuu wa Wilaya ya Kyela Dk Thea Ntara.
Maafisa Usalama kutoka Wilaya ya Kyela nchini Tanzania.
Maafisa Usalama kutoka Wilaya ya Karonga nchini Malawi.
Maafisa Mifugo kutoka Wilaya za Kyela na Karonga
Kikao cha ujirani mwema baina ya Wilaya ya
Kyela nchini Tanzania na Karonga nchi ya Malawi kimefanyika katika ukumbi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Kyela kwa ajili ya kujadili changamoto zinazozikabili
Wilaya hizo.
Wilaya ya Kyela iliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya
Dakta Thea Ntara na kwa upande wa Wilaya ya Karonga iliwakilishwa na Rosemary
Moyo na baadhi ya changamoto kubwa zinazozikabili Wilaya hizo ni pamoja na
wahamiaji haramu,madawa ya kulevya,pombe kali na wizi wa pikipiki.
Baadhi ya wajumbe kutoka pande zote mbili
wamesema kuwa tatizo la wahamiaji haramu kutoka nchi za
Ethiopia,Somalia,Congo,Burundi,Rwanda na Nigeria kunachangiwa na ukoefu wa
umakini kutoka mipaka ya kaskazini ambapo huwaacha wahamiaji hao kuingia
kiholela.
Sababu nyingine inachangiwa na baadhi ya
watumishi wa umma wa pande hizo mbili wa
kutodhibiti vitendo hivyo kutokana wa baadhi ya wahamiaji kutumia pesa pindi
wanapokamatwa na baadhi ya maafisa usalama wasio waaminifu.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Karonga
Rosemary Moyo amesema kuwa Watanzania na Wamalawi ni ndugu wa damu ambao
wametenganishwa na wakoloni kwa njia ya mpaka wa mto Songwe kwani mpaka sasa
raia wa mpakani huvuka kutembeleana kila siku na wengi wao wameoleana kutoka
pande hizo mbili.
Hata hivyo kutokana na tatizo hilo kubwa kwa
nchi hizo Serkali zote huingia gharama kubwa kuwatunza na kuwasafirisha
wahamiaji haramu kuwarejesha nchi
walizotoka.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kyela Dakta
Thea Ntara amesema wilaya ya Kyela imeimarisha ulinzi mpakani kwa kushirikiana
na wananchi ndiyo maana wamefanikiwa kukamata wahamiaji wengi haramu
waliojaribu kuvuka mpaka kupitia wilaya hiyo hivyo juhudi kubwa zifanyike ili
kuhakikisha tatizo hilo linakomeshwa kabisa.
Hata hivyo elimu itolewe kwa raia wa pande
zote mbili ili watu wanaowatilia shaka watolewe taarifa katika vyombo vya
ulinzi na usalama vya nchi hizo.
0 comments:
Post a Comment