Na Ezekiel Kamanga.
Jeshi la
Polisi Mkoani Mbeya linawashikilia Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nsalala Stephano
Mshani(CHADEMA)na Mtendaji Lwitiko Mwaibindi kwa tuhuma za kuuza ardhi ya
Kijiji na fedha kujimilikisha kwenye akaunti mbili za Mwenyekiti.
Tukio hilo
limetokea katika mkutano wa hadhara baada ya wananchi kuwatuhumu viongozi hao
kwa kuuza mali ya umma kisha kujimilikisha jumla ya shilingi milioni nane laki
sita na elfu hamsini bila ridhaa ya wananchi wa kitongoji cha Nsalala.
Katika
mkutano iliofanyika machi 26 mwaka huu wananchi hao walimwandikia Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Upendo Atu Sanga wakitaka kuundwa kwa Tume ya
uchunguzi ili kubaini fedha zinazodaiwa kuhodhiwa na viongozi hao bila ridhaa
ya wananchi.
Baada ya
kupokea malalamiko hayo Mkurugenzi alituma Tume ya uchunguzi ambapo ilibaini
tuhuma mbalimbali dhidi ya viongozi hao na kuyasoma maagizo mbele ya mkutano wa
hadhara uliofanyika April mosi mwaka huu katika uwanja wa shule ya msingi
Nsalala.
Barua hiyo
kutoka kwa Mkurugenzi ilisomwa mbele ya wananchi na Mwanasheria wa Halmashauri
ya Wilaya ya Mbeya Prosper Msivala amabayo ilibaini kuwa :-
(a)Mwenyekiti
Stephano Mshani anatuhumiwa kwa makosa yafuatayo:-
(i)Kushiriki
kuuza mali ya Umma kinyume cha sheria ya manunuzi ya Umma ya mwaka 2011.
(ii)Kutunza
fedha zilizotokana na mauzo hayo kwenye akaunti zake binafsi mbili zilizopo
Benki ya NMB Mbalizi Road zenya namba 6251000804 na 62510009 zote zikimilikiwa
na Stephano Mshani.
(b)Mtendaji
wa Kitongoji(Lwitiko Mwaibindi)anatuhumiwa kwa:-
(i)Matumizi
mabaya ya madaraka kwa kushindwa kusimamia Kitongoji na kuwapotosha wananchi.
(ii)Kughushi
nyaraka na mikhutasari ya vikao
(iii)Kukodisha
eneo la maziko kwa shughuli za kilimo bila kufuata taratibu.
(iv)Kuuza
mali ya Umma kinyume na taratibu ya manunuzi ya Umma ya mwaka 2011.
(v)Matumizi
mabaya ya muhuri ambao siyo halali.
(vi)Kumdanganya
Mwajiri kwa kuficha ardhi ya Mamlaka na kutokabidhi kwa mamlaka.
Hivyo
kutokana na makosa hayo Mkurugennzi Mtendaji wa Wilaya ameagiza mosi eneo
lililouzwa kurudishwa mara moja kwenye Maml;aka ya Mji mdogo kuanzia April mosi
mwaka huu.
Pili
Mtendaji wa Kitongoji(Lwitiko Mwaibindi)anasimamishwa kazi kuanzia April mosi
mwaka huu ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.
Tatu Polisi
na vyombo vya Dola vimchukulie hatua stahiki Mwenyekiti wa Kitongoji cha
Nsalala Stephano Mshani.
Uchunguzi
umebaini kabla ya mkutano huo viongozi hao walikuwa na taarifa mbili za mapato
na matumizi yenye kuonesha kuwa baadhi ya wadau walichanga jumla ya shilingi
milioni tatu laki nane arobaini na tatu elfu(3,843,000/=) ambazo zilitumika
zote kununua vifaa vya ujenzi,malipo ya mafundi na kusafirishia vifaa vya
ujenzi kwa ajili ya shule ya msingi Nsalala.
Taarifa ya
mauzo ya shamba shilingi 8,650,000/= ambazo zinaonesha kununulia vifaa vya ujenzi
fedha ambazo zilitunzwa kwenye akaunti binafsi za Stephano Mshani kuwa akaunti
ya Kitongoji ilikuwa haifanyi kazi kwa muda mrefu.
Baada ya
Mwanasheria kuisoma barua hiyo kutoka kwa Mkurugenzi Stephano Mshani na Lwitiko
Mwaibindi walichukuliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano na Diwani wa Kata ya
Nsalala Kissman Ngomale alifunga mkutano kwa kuwataka wananchi kuwa wavumilivu
ili kusubiri hatua stahiki dhidi ya viongozi hao ikiwa ni pamoja na kufikishwa
mahakamani.
0 comments:
Post a Comment