Dk. Mwinyi akihutubia.
Waziri wa afya na ustawi wa jamii
Dk. Hussein Mwinyi amezindua kipimo cha malaria kinachotoa majibu ya haraka
katika vituo binafsi vya kutolea huduma za afya.
Kipimo hicho ambacho tayari
kinafanya kazi katika vituo vya afya vya serikali, kinatoa majibu kwa muda wa
dakika 15 tangu mgonjwa kuanza kutolewa damu.
Akiongea katika uzinduzi huo, Dk
Mwinyi amesema kuzinduliwa kwa kipimo hicho kinachojulikana kama MRDT wana
lengo la kupambana na Malaria na kusogeza huduma kwa wananchi wote kwa gharama
nafuu.
Dk. Mwinyi amewataka wananchi kuacha
tabia ya kutumia dawa za malaria bila kupima hata kama utakuwa na dalili za
homa badala yake mgonjwa afike katika kituo cha afya kilicho karibu yake kwa
uchunguzi zaidi.
Ameongeza kuwa gharama ya kupima kwa
kipimo hicho haitakiwi kuzidi shilingi 1,100 na kwamba serikali imejipanga
vizuri kuwadhibiti watoa huduma wa afya wa sekta binafsi watakaozidisha bei
kinyume na maelekezo ya serikali.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha
uchunguzi na tiba ya malaria katika mpango wa taifa wa kudhibiti malaria nchini
Dk. Sigsbert Mkude amesema kipimo hicho kimefanyiwa utafiti wa kina na
kuonekana kuwa kinafa japo kuna baadhi ya changamoto kwa baadhi ya wagonjwa.
Kutokana na taarifa ya utafiti
katika jamii THMIS katika kipindi cha miaka mitano, maambuki ya ugonjwa wa
malaria yamepungua kwa zaidi ya asilimia 50 kutoka asilimia 18 mwaka 2007/2008
hadi asilimia 9 mwaka 2011/2012.
0 comments:
Post a Comment