Pages


Home » » Theo Walcott ameshangazwa na jeraha la kichwa alilopata mchezaji mwenzake Wayne Rooney.

Theo Walcott ameshangazwa na jeraha la kichwa alilopata mchezaji mwenzake Wayne Rooney.

Kamanga na Matukio | 02:03 | 0 comments
Mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza, Theo Walcott ameshangazwa na jeraha la kichwa alilopata mchezaji mwenzake Wayne Rooney na kusababisha kumuweka nje ya kikosi cha timu ya taifa ya nchi kitakachopambana na Moldova na Ukraine katika kutafuta tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia.



Rooney aliondolewa katika kikosi cha Manchester United ambacho kilichapwa bao 1-0 na Liverpool katika Uwanja wa Anfield baada ya jeraha hilo kwa bahati mbaya wakati wa mazoezi.



Meneja wa United David Moyes alithibitisha nyota huyo kukosekana kwa kipindi cha wiki tatu au zaidi hivyo kumuacha kocha wa Uingereza Roy Hodgson kukosa huduma ya mchezaji huyo.



Akihojiwa Walcott amesema aliona picha ya sehemu alipoumia Rooney na kustushwa huku akidai kuwa sio kitu kizuri kukitazama akifananisha na sinema za kutisha.

Hata Hivyo Walcott ana imani kuwa wapo wachezaji wengine imara wanaoweza kuisadia nchi hiyo kushinda mechi zake zote mbili muhimu kwa ajili ya kufuzu.



Wakati huohuo, mabingwa wa soka barani Ulaya na Ujerumani, klabu ya Bayern Munich wametangaza kuwa kiungo wake nyota Javi Martinez amefanyiwa upasuaji wa kinena wenye mafanikio.



Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa hiyo imedai kulikuwa na ulazima wa kiungo wa kimataifa wa Hispania kufanyiwa upasuaji huo baada ya mara kwa mara kulalamika kuwa na tatizo hilo.



Martinez ambaye aliingia uwanjani akitokea benchi na kufunga bao la kusawazisha katika dakika za majeruhi katika muda wa nyongeza wiki iliyopita katika mchezo wa Supercup dhidi ya Chelsea kabla ya Bayern kushinda mechi hiyo kwa changamoto ya mikwaju ya penati.



Kocha wa Hispania Vicente del Bosque hakumjumuisha kiungo huyo katika kikosi chake ambacho kinakabiliwa na mechi ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Finland na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Chile.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger