Siku
moja
baada ya uongozi wa klabu ya Dar es salaam Young Africans kudaiwa
kumuajiri
katibu mkuu mpya badala ya Lawrence Mwalusako, kamati ya wazee wa klabu
hiyo wameibuka na kudai hawamtambui katibu huyo ambae ni raia kutoka
nchini
Kenya.
Katibu wa
kamati ya wazee wa klabu hiyo Ibrahim Akilimali amesema kama ni kweli viongozi
wa ngazi za juu wameamua kufanya maamuzi ya kumuajiri katibu huyo anaejulikana
kwa jina la Patrick Nagi wanatakia kutambua wamekiuka kanuni na taratibu
zilizoainishwa kwenye katiba inayowaongoza.
Uongozi wa
klabu ya Simba umeendelea kutoa tahadhari kwa wafanyabiashara nchini
wanaoendelea kukiuka taratibu za kuuza bidhaa zenye nembo ya klabu hiyo
inayotambulika kisheria.
Mwenyekiti wa
baraza la wadhamini la klabu ya Simba Khamisi Kilomoni kwa muda mrefu wamekua
wakitoa tahadhari hiyo kwa wafanyabiashara wakubwa na wale wadogo lakini
imeonekana wanadharaulika, hivyo kwa sasa wameamua kutumia nguvu za kisheria
kwa lengo la kukomesha biashara hiyo haramu.
Naye Insepekta
wa Jeshi la Polisi Mohamed Manyae amesema baada ya kufuatwa na uongozi wa klabu
ya Simba na kulalamikia juu ya biashara inayoendelea kufanywa na
wafanyabiashara nchini ya bidhaa za klabu hiyo, wameamua kuwa bega kwa bega na
uongozi huo kwa lengo la kumaliza tatizo hilo.
0 comments:
Post a Comment