Mashabiki wa soka nchini wametakiwa kuwa nyuma ya timu ya
taifa ya Tanzania Taifa Stars ambayo inakabiliwa na mchezo wa mwisho wa kuwani
nafasi ya kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia dhidi ya timu ya taifa ya
Gambia mwishoni mwa juma hili.
Rai hiyo kwa mashabiki wa soka, imetolewa na katibu mkuu wa
shirikisho la soka nchini TFF Angetille Osiah ambapo amesema kuna haja kwa
watanzania kuendelea kuwa nyuma ya Taifa Stars licha ya kukosa nafasi ya kufuzu
kucheza fainali hizo ambazo zitaunguruma mwakani nchini Brazil.
Amesema mchezo dhidi ya Gambia una umuhimu mkubwa kama
alivyosema kocha mkuu wa Taifa Stars Jan Poulsen wakati akizungumza na
waandishi wa habari hapo jana.
Wakati huo huo timu ya taifa ya Tanzania imeondoka hii leo
kuelekea mjini Banjul nchini Gambia tayari kwa mchezo dhidi ya wenyeji wao
ambao umepangwa kufanyika Septemba 07.
Kikosi kilichoondoka kinamjumuisha nahodha na mlindamlango
wa Taifa Stars Juma Kaseja, Mwadini Ali, Ali Mustafa,
Amri Kiemba, David Luhende, David Mwantika, Erasto Nyoni, Frank Domayo, Haruni
Chanongo, Henry Joseph, Jonas Mkude, Juma Liuzio, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa,
Nadir Haroub, Said Dilunga, Simon Msuva na Vincent Barnabas.
0 comments:
Post a Comment