Pages


Home » » Wandishi wa Habari Mkoani Mbeya wametakiwa kuisaidia jamii kupinga vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na Watoto.

Wandishi wa Habari Mkoani Mbeya wametakiwa kuisaidia jamii kupinga vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na Watoto.

Kamanga na Matukio | 05:03 | 0 comments

Mwezeshaji kutoka Walter Reed Program Hijja Wazee wakati akitoa Semina kwa waandishi wa Habari 20 iliyofanyika katika ukumbi wa Youth Centre wa Kanisa Katoliki uliopo Jijini Mbeya.

Mwezeshaji kutoka Walter Reed Program Mergitu Ebba akiwanoa waandishi wahabari waliohudhuria semina hiyo



Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa makini kumsikiliza mwezeshaji






Wandishi wa Habari Mkoani Mbeya wametakiwa kuisaidia jamii kupinga vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na Watoto  uliokithiri vitendo ambvyo hupelekea kuwa na ongezeko la maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Kauli hiyo imetolewa na Mwezeshaji kutoka Walter Reed Program Hijja Wazee wakati akitoa Semina kwa waandishi wa Habari 20 iliyofanyika katika ukumbi wa Youth Centre wa Kanisa Katoliki uliopo Jijini Mbeya.
Mkufunzi huyo amesema kukithiri kwa vitendo vya unyanyasaji wa Kijinsia ndani ya jamii vinaweza kumalizwa endapo Wanahabari watafanya kazi ya kujitolea ya kuibua na kuiambia jamii madhara ya vitendo hivyo.
Ameongeza kuwa zaidi ya asilimia 56 ya jamii ya Mbeya inasadikika kujihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia na kwamba Mfuko wa raisi wa Marekani umetoa fedha kwa ajili ya kuhakikisha Vitendo hivyo vinaisha ambapo msaada huo utalenga Nchi tatu ikiwemo Tanzania.
Amesema Nchini Tanzania ni Mikoa minne  itakayohusika  ambayo ni Mbeya, Iringa, Mara na Dar Es Salaam ambapo kwa Mkoa wa Mbeya ni Wilaya Sita zitakazohusika ambazo ni Mbeya Jiji, Ileje, Kyela, Rungwe, Busokelo na Mbeya Vijijini.
Na Mbeya yetu
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger