Msafara
wa Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja ukiwasili katika
viwanja vya Chuo cha ufundi Ruanda Jijini Mbeya kwa ajili ya kuwatunuku
nishani Maaskari wa Jeshi la Magereza
Kamishina
Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja Akikagua Gwaride maalum
lililoandaliwa na maaskari wa Jeshi la Magereza kwa ajili yake mara
baada ya kuwasili katika viwanja hivyo kwa ajili ya kuwatunuku nishani
Maaskari.
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja akipokea Salam za heshima kutoka kwa Askari wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Mbeya
Baadhi ya Maaskari wa Jeshi la Magereza wakitoa heshima kwa Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja (ambaye haonekani pichani) wakati wa hafla ya kuwatunuku nishani.
Brass band ya Jeshi la Magereza kutoka Kiwira Rungwe wakitumbuiza katika Sherehe hizo
Baadhi ya Maofisa wa Jeshi la Magereza wakiwa wamesimama kwa ukakamavu kutoa heshima kwa Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja
Baadhi ya Maaskari wastaafu wa Jeshi la Magereza pamoja na maofisa wakifuatilia kwa umakini Sherehe za kutunuku nishani
Baadhi ya Maaskari wakisubiri kutunukiwa nishani kutoka kwa Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja
SACP
C. A Keenja akitaja majina 29 ya Maaskari wanaotakiwa kutunukiwa
Nishani ya Utumishi uliotukukuka Tanzania, Utumishi Muda Mrefu Tanzania,
Utumishi mrefu na tabia njema na Mwenge wa Uhuru daraja la nne.
Askari Mwanamke akitembea kwa ukakamavu kuelekea eneo linalotumika kutunukia Nishani kwa Maaskari wa Jeshi la Magereza
Kamishina
Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja (kulia) akimvisha nishani ya
utumishi ulio Tukuka Tanzania ACP Hawa M. Simon ambaye pia ni Mkuu wa
Magereza Mkoa wa Rukwa.
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja Akimvalisha Nishani SGT ambaye Jina lake halikupatikana Mara Moja.
Kamishina
Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja akimvisha Nishani ya utumishi
mrefu na tabia njema SGT Yusufu F. Nzunda kutoka chuo cha Magereza
Kiwira
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja Akimvalisha Nishani SGT ambaye Jina lake halikupatikana Mara Moja.
Kamishina
Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja Akimpongeza Askari mara baada ya
kutunukiwa nishani ya utumishi mrefu na Tabia njema.
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja Akiwa katika picha ya pamoja na Maaskari 29 waliotunukiwa Nishani mbalimbali
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maofisa wa Jeshi la Magereza wastaafu.
Kamishina
Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja akiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Mbeya
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanawake waliotunukiwa Nishani
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja akibadilishana jambo na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Barakael Masaki
Kamishina
Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja akiwa katika picha ya Pamoja na
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza Makao Makuu Insp. Lucas Mbonje
wakizungumza na waandishi wa Habari mbalimbali wa Mkoa wa Mbeya.
**********************
RAISI
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewatunuku Nishani
mbali mbali Askari 29 kwa Askari wa Jeshi la Magereza kutoka Nyanda za
juu kusini.
Mbali
na Nishani hizo pia Jeshi hilo limesema limejipanga kuhakikisha
linaanza kujitegemea na kuepukana na Bajeti za Serikali katika
kujiendesha kutokana na uwepo wa Rasilimali nyingi zinazoweza kuzisaidia
hususani Wafungwa na Ardhi kwa ajili ya kuzalisha Chakula.
Kauli
hiyo imetolewa Leo na Kamishina Jenerali wa Magereza Nchini, CGP John
C. Minja wakati wa hafla fupi ya kuwatunuku Nishani Maaskari wa Jeshi
hiyo iliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Magereza Ruanda Jijini
Mbeya.
CGP
Minja amesema Jeshi la Magereza linauwezo wa kujiendesha kutokana na
kuwa na rasilimali na nguvu kazi ambazo zitatumika katika kuzalisha
chakula ili kuepuka kusubili Fedha kutoka Serikalini ambazo huchukua muda mrefu kupatikana na milolongo kuwa mingi.
Ameongeza
kuwa hata baada ya kuanza kujitegemea kwa Jeshi hilo kutawapunguzia
gharama walipa kodi ambao wamekuwa wakikatwa fedha zao kila siku ili
kufanikisha upatikanaji wa Chakula kwa Wafungwa na Shughuli nzima za
Jeshi la Magereza Nchini ikiwemo upungufu wa Majengo.
Kamishina
huyo pia ameiomba Serikali kuunga mkono juhudi hizo na mikakati ya
kutaka kujitegemea ili kuzipunguzia Taasisi Mbali mbali kama Wabunge
ambao kila mara wamekuwa wakijadili suala la uboreshaji wa Jeshi la
Magereza Nchini.
“
Tangu niingie madarakani lengo langu na ajenda kuu ni kuboresha jeshi
la Magereza ili liweze kujitegemea ikiwa ni pamoja na kuwapunguzia
gharama zisizokuwa za ulazima kwa wanaokatwa fedha katika vipato vyao” alisema CGP Minja.
Katika Hafla hiyo Jumla ya Askari 29 walitunukiwa Nishani Kutoka kwa Kamishina
Jenerali wa Magereza ambaye alitumia Mamlaka aliyokasimiwa na Raisi wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Kifungu cha 34(4) Cha katiba ya
Jamhuri ya Muungano ya kuwavisha Nishani Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza ambao walitunukiwa Nishani mbali mbali lakini hawakuvishwa na Raisi Aprili 26, Mwaka huu.
SACP Keenja ambaye ndiye alikuwa akitaja majina ya Askari waliotunukiwa Nishani hizo alisema Orodha
ya majina ya Maafisa na Askari pamoja na Nishani zao yameelezwa na
kuainishwa katika Taarifa ya Kawaida na kutangazwa kwenye Gazeti la
Serikali namba 84/2013 la April 26, Mwaka huu.
Alizitaja
Nishani hizo kuwa ni pamoja na Nishani ya Utumishi uliotukuka ambayo
hutunukiwa Maafisa waliokwenye Utumishi wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania
ambapo kwa Jeshi la Magereza hutunikiwa wenye Cheo cha Mrakibu au wa
juu ya Cheo hicho waliotumikia jeshi hilo kwa Miaka 20 Mfululizo ambayo
alitunukiwa Askari mmoja ambaye ni ACP Hawa Mollel Simon ambaye pia ni
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Rukwa.
Nishani
ya Pili hutunukiwa kwa Askari kuanzia Nyota Moja ambao wametimiza
utumishi wa miaka isiyopungua 15 mfululizo akiwa na tabia njema ya
kuweza kusifiwa, Nishani ambayo alitunukiwa Askari mmoja ambaye ni ACP
Ally Abdalah Kaherewa ambaye pia ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Ruvuma.
Nishani
ya Tatu ni kwa ajili ya askari wenye Cheo cha Wakaguzi, Wakaguzi
wasaidizi, Stesheni Sajini, Sajini na Koplo waliotumikia jeshi la
Magereza miaka 15 Mfululizo ambayo huitwa Nishani ya Utumishi Mrefu
Tanzani ambayo walitunukiwa Askari 18.
SACP
Keenja ameitaja Nishani ya nne waliotunukiwa asakari hao kuwa ni kwa
wale wanajeshi waliohai ambao walizaliwa Disemba 9, 1961 au kabla ya
hapo na mbao wamefanya kazi katika katika Majeshi ya Ulinzi na Usalama
kwa muda wa Miaka 35 au zaidi wakiwa Jeshini wenye sifa na tabia njema
ambayo huitwa Nishani ya Mwenge wa Uhuru daraja la Nne waliyotunukiwa
askari 9.
Na Mbeya yetu Blog.
0 comments:
Post a Comment