Kamishina
Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja wa kwanza kutoka kulia,
akizungumza na viongozi wa Tone Multimedia Group ambao ni wamiliki wa
Mtandao wa Mbeya yetu Blog, Kushoto ni Joseph Mwaisango, Fredy njeje na
Venance Matinya kutoka Gazeti la Jambo leo na Ezekiel Kamanga ambaye
alikuwa amepiga Picha.
Kamishna
wa wa Magereza Gaston Sanga (Aliye vaa Tai) ambaye pia Mkuu wa kitengo
cha Fedha na Utawala wa Jeshi Hilo,akiwa sambamba na afisa Habari wa
Jeshi la Magereza Mkaguzi Lukas A.Mboje wa pili kutoka kulia ,
Akizungumza na waandishi wa Habari.
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja kutoka kulia akizunguza na SACP C. A Keenja
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja kutoka kushoto akiwa na Mkuu wa uhamiaji Mkoa wa Mbeya Wilson Bambaganya.
Mkuu
wa kitengo cha Usafirishaji Makao makuu Jeshi la Magereza (wapili
kutoka Kulia) Mratibu Mwandamizi wa Magereza Lazaro Nyanga akiwa na
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza pamoja na waandishi wa Habari
Kamishina
Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja katikati akiwa katika na picha
ya pamoja na Kamishna wa wa Magereza Gaston (kushoto) ambaye pia Mkuu
wa kitengo cha Fedha na Utawala wa Jeshi na Mkuu wa uhamiaji Mkoa wa
Mbeya Wilson Bambaganya (kulia)
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja akizungumza na baadhi ya Askari wa Jeshi la Magereza .
JESHI la Magereza
Nchini limeomba ushirikiano na Vyombo vya Habari ili kusaidia kufikia malengo
ya kulisaidia Jeshi hilo kujitegemea na
kujiendesha lenyewe pasipo kutegemea misaada.
Kauli hiyo imetolewa na
Kamishina Jenerali wa Magereza Nchini, CGP John C. Minja wakati wa hafla fupi
ya kuwatunuku Nishani Maaskari wa Jeshi hilo iliyofanyika katika ukumbi wa
Gereza la Ruanda Jijini Mbeya alipokuwa
akizungumza na baadhi ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya wakiwemo viongozi
Waandamizi wa Mtandao wa www.mbeyayetu.blogspot.com.
Minja amesema ili kufikia
malengo waliyojiwekea ni lazima pawepo na ushirikiano baina ya Jeshi hilo na
Waandishi wa Habari kwa kuwa ndiyo wenye dhamana ya kuwaambia wananchi
Changamoto zinazolikumba Jeshi hilo.
Pia ametoa wito kwa Viongozi
kutoogopa kuzungumza na Vyombo vya Habari kwa kile alichodai kushindwa kufanya
hivyo ni kuficha maovu ambayo wanaogopa
kuonwa na kujulikana kwa jamii.
Aidha amewaagiza Viongozi wa
Jeshi hilo kuhakikisha wanaandaa Barua mapema kwa Maaskari wanaopandishwa Vyeo
na siyo kusubiri na kusotea kwa muda mrefu wakisubiri barua za uthibitisho.
0 comments:
Post a Comment