Wawakilishi wa timu mbalimbali zinazoshiriki ligi
kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya
kukabidhiwa vifaa vya michezo na mdhamini wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom
tayari kwa ajili ya kuanza kwa msimu wa ligi kuu 2013/2014. Pamoja nao katika
picha ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na
Mawasiliano wa kampuni hiyo Kelvin
Twisa,(Aliyeshikilia mpira) na Mkurugenzi
wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba.
Wawakilishi wa timu mbalimbali zinazoshiriki ligi kuu
ya Vodacom Tanzania Bara, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya
kukabidhiwa vifaa vya michezo na mdhamini wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom
tayari kwa ajili ya kuanza kwa msimu wa ligi kuu 2013/2014. Pamoja nao katika
picha ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na
Mawasiliano wa kampuni hiyo Kelvin
Twisa, na Mkurugenzi wa Mashindano wa
TFF, Saad Kawemba.
*******
Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu Tanzania Bara Kampuni ya
Vodacom leo imekabidhi vifaa kwa timu 14 shiriki za ligi hiyo vikiwa na thamani
ya zaidi ya Sh 400 Milioni.
Akizungumza kabla ya zoezi la kukabidhi vifaa
hivyo kuanza, Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba pamoja na
kuishukuru Vodacom kwa kutekeleza majukumu yake ya kimkataba amevitaka vilabu
vya ligi kuu kuu ya Vodacom kuheshimu chapa ya mdhamini wakati wote wa mechu za
ligi.
“Ninatoa wito kwa vilabu vyote kutumia jezi zenye
nembo ya mdhamini kama kanuni zinavyo sema, pia ninawaomba viongozi wote tuwe
na Ushirikiano katika kuhakikisha ligi inafanikiwa kama inavyotakiwa,”
Kama mzazi tusingependa kutumia kanuni na sharia
kuadhibu klabu inayokwenda kinyume tunapenda kuona kila mmoja akimtendea haki
mdhamini kama ambavyo nay eye anavyotimiza haki yake ya kutupatia vifaa
hivi.”Aliongeza Saad
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano
wa Vodacom, Kelvin Twissa alisema kuwa vifaa hivyo viko tayari na anaamini timu
zote zimejiandaa vya kutosha na tayari kuingia katika mtanange wa ligi.
“Tunajisikia furaha sana kufikia hapa leo na
kukabidhi vifaa hivi tukitekeleza matakwa ya mkataba wa udhamini, ni imani yetu
kwamba timu zineshajiandaa vizuri na sasa tupo tayari kuanza msimu mpya wa
2013/2014.’Alisema Twissa
Twissa aliongeza kuwa vifaa vipya vilivyo
kabidhiwa ni pamoja na seti za jezi mbalimbali, viatu vya mazoezi na mechi,
soksi, vilinda ugoko (shin guards), nguo za mazoezi, nguo za kawaida, gloves na
vifaa vingine.
Aidha, Pamoja na kukabidhi vifaa hivyo wao kama
wadhamini wa ligi kuu pia wamefarijika kuona timu zote zimefanya maandalizi ya
kutosha.
“Hii
ni ishara tosha kuwa siku hadi siku ligi
yetu imeendelea kuimarika na kuwa na ushindani mkubwa zaidi hakika tunajivunia
kuwa sehemu ya mafanikio ya soka nchini,” alisema.
Twissa alihitimisha kwa kutoa wito kwa wadau
wengine wenye malengo ya kukuza soka la Tanzania kujitokeza na kuongeza
udhamini katika ligi ili kuleta tija zaidi huku akiendelea kuwakumbusha
wanahabari wajibu wao wa kuitangaza ligi hususan vipaji.
Hatudhamini kwa sababu ya viongozi wala jambo
jengine lolote, Vodacom inadhamini ligi kwa sababu soka ni mchezo unaopendwa na
ndio wenye washabiki wengi na hatimae kukuza vipaji.”Alisema Twissa na
kuongeza.
“Vyombo vya habari mnanafasi kubwa sana ya kutangaza vipaji na ligi
yetu na sio kuandika habari hasi ambazo hazijengi tungepeda kuona wachezaji
wetu wanakuwa maarufu kama wanavyojulikana kina Ronaldo, Rooney na wengine wa
nje.”
0 comments:
Post a Comment