Na Ezekiel Kamanga.
Wananchi wanaotumia kivuko cha
Daraja la Makaburi ya Sabasaba Mtaa wa Jakaranda wameiomba halmashauri ya Jiji
la Mbeya kuweka kipaumbele katika kuboresha huduma za kijamii hususani
miundombinu ya barabara, vivuko kwani vingi vimekuwa hatarishi katika
kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha Jijini hapa.
Wakizungumza na kituo hiki jana
kwa nyakati tofauti walisema kuwa kivuko hicho kimekuwa chakavu kwa
muda sasa licha ya kutoa taarifa kwa viongozi wa serikali za mitaa.
Athanas Amosy,Mkazi wa Forest
alisema ni vema halmashauri ikaliona hili na kulifanyia kazi kwani wananchi
wengi wamekuwa wakitegemea kivuko hichi ambacho ni muhimu kwetu kwa
shughuli mbalimbali za kiofisi na hata wafanyabishara kwani kimekuwa tishio
pindi mvua zinapokuwa zikinyesha.
Mkazi wa Magereza Salome Adamson
,alisema wanaiomba Serikali kuangalia namna ya kuboresha
miundombinu rafiki inayotumika na wananchi kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi
katika maeneo ya mijini .
Akizungumza na gazeti hili
,Mwenyekiti wa Mtaa wa sabasaba Aidan Ng'oma alikiri kuwepo kwa changamoto hizo
na kwamba alituma maombi halmashauri na kwamba uwenda ni miongoni
mwa miradi itakayoboreshwa kwa mwaka huu wa fedha .
"Kwani mkakati sio kuboresha
kivuko hiki pekee kipo kingine korofi katika eneo la ujenzi ambacho
ni miongoni vya vitakavyofanyiwa ukarabati"alisema.
Kwa upande wake ,Diwani wa kata ya
Mbalizi Road,Adam Hussein alipohojiwa kuhusiana na malalamiko ya wananchi
alisema kuwa alikwisha wasilisha kwenye vikao vya baraza la madiwani na
kwamba miongoni mwa miradi iliyoingizwa katika bajeti ya mwaka wa fedha
2016/17 .
0 comments:
Post a Comment