Pages


KIPINDUPINDU;- Watu 17 wakamatwa kwa kukosa vyoo na uchafu wa mazingira Mkoani Mbeya.

Chimbuko Letu | 08:58 | 0 comments


 Mkuu wa Wilaya ya Kalonga, Nchini Malawi Rosemary Kalonga na Mkuu wa Wilaya ya Kyela Dk Thea Ntara.

Na Ezekiel Kamanga.
Watu 17 wakazi wa Kijiji cha Lusungo Kata ya Lusungo Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya wamekamatwa kwa kutokuwa na vyoo na uchafu wa mazingira hivyo kuzorotesha juhudi za kupambana na ugonjwa wa kipindupindu Wilayani humo.


Ugonjwa huo umedumu kwa kipindi cha miezi mitatu sasa na Kata ya Lusungo na Ndobo ndizo pekee bado zina wagonjwa wa kipindupindu hali iliyomfanya Mkuu wa Wilaya ya Kyela Dakta Thea Ntara kupiga kambi Kata ya Lusungo ili kufanya ukaguzi wa vyoo na usafi wa mazingira.


Hata hivyo juhudi za Mkuu wa Wilaya zinakwamishwa na Diwani wa Kata ya Lusungo Veronica Kanyanyila na Mwenyekiti wa Kijiji Zawadi Lugano Mwangojola ambao wamekuwa wakidai ugonjwa huo umesababishwa na imani za kishirikina na si uchafu au ukosefu wa vyoo.


Katika oparesheni hiyo maalumu iliyofanywa na Mkuu wa Wilaya aliyeambatana na Maafisa wa Afya pia iliyakumba maeneo mbalimbali kama Kata ya Ikama na Kijiji cha Tenende ambapo alilazimika kuvunja Kilabu cha pombe Kata ya Ikama baada ya kuwakuta wakazi wa eneo hilo wakinywa pombe za kienyeji katika mazingira machafu.


Mbali ya ukaguzi huo pia Mkuu wa Wilaya alishuhudia baadhi ya wananchi wakinywa pombe ya moshi na pombe zilizopigwa marufuku kutoka nchi jirani na kulazimika kuwakamata wahusika ambao wamefikishwa kituo kikuu cha Polisi Wilaya ambapo pindi uchunguzi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.


Dakta Thea aliteketeza sindano zinazodhaniwa kutumika kwa ajili ya kujidunga wakati wa matumizi ya madawa ya kulevya katika Kata ya Ikama na ametoa agizo la kuwasaka wauzaji wa madawa hayo na wanaouza pombe zilizopigwa marufuku kutoka nchi jirani.


Kwa upande wake Afisa Afya Geophrey Baroshi amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu na watahakikisha kila kaya ina choo na kuwa na mazingira safi kwa muda wote ili kuutokomeza kabisa ugonjwa huo Wilayani Kyela na kwamba waliokamatwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.


Mtendaji wa Kijiji cha Lusungo Fadhili Sade amesema kuwa wamefanya ukaguzi katika kaya 681 za kijiji hicho na zote hazina vyoo hali inayofanya mapambano ya kipindupindu kuwa magumu mno kwani wengi wao wamekuwa wakiamini ugonjwa huo unatokana na ushirikina.


Aidha Mtendaji wa Kata ya Lusungo Stephen John amesema wamekuwa wakipokea vitisho kutoka kwa Diwani wa Kata na Mwenyekiti wa kijiji kuwa aache kutangaza kuwa Kata hiyo inakabiliwa na ugonjwa wa kipindupindu kwani ndiyo kunachochea kuongezeka kwa ugonjwa huo ambao unatokana na ushikina na si uchafu au ukosefu wa vyoo.

Raia wa nchi ya Somalia anashikiliwa na jeshi la polisi Mkoani Mbeya kwa tuhuma za ubakaji.

Chimbuko Letu | 08:54 | 0 comments
Na Ezekiel Kamanga.
Raia wa nchi ya Somalia  Mohamed Ahmed (31) anashikiliwa na jeshi la polisi Mkoani Mbeya kwa tuhuma za kumbaka mtoto  mweye umri wa miaka miwili jina limehifadhiwa.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Ahmed Msangi alisema kuwa  lilitokea jumapili ya pasaka majira ya saa nne asubuhi katika eneo la Kambi katoto wilayani Chunya.

Alisema kuwa Mtuhumiwa Ahmed akiwa na nia ovu alimchukua mtoto nyumbani kwao na kisha kwenda kumbaka na kumsababishia maumivu makali sehemu za siri.

“Inadaiwa kuwa mtuhumiwa alienda kumchukua mtoto nyumbani kwao na kwenda nae sehemu isiyojulikana kisha kumbaka, bado tunafanya upepelezi ikithibitika ni kweli mtuhumiwa amehusika tutamfikisha mahakani kwa ajili ya hatua zaidi”alisema.

Katika tukio jingine alisema Mwanamke, Mwanashija Teru aliuwawa na watu wasiofahamika baada ya kukatwa na kitu chenye kali sehemu mbalimbali za mwili wake usiku wakati akiwa amelala.

Alisema kuwa tukio hilo lilitokea Machi 23 mwaka huu eneo la Kipambawe wilayani Chunya na kuripotiwa polisi Jumapili ya pasaka kutokana na umbali mrefu uliopo kati ya kituo cha polisi na eneo la tukio.

“Mwanamke huyo alikatwa na kitu chenye ncha kali sehemu za kichwani, Shingoni na mikononi wakati akiwa amelala usiku wa manane na watu wasiofahamika kwa hiyo tu nachunguza tukio hilo pamoja na kuwasaka wahusika ili wafikishwe mahakamani.”alisema

Halmashauri ya Jiji la Mbeya yaombwa kuweka kipaumbele katika kuboresha huduma za kijamii.

Chimbuko Letu | 08:50 | 0 comments
Na Ezekiel Kamanga.
Wananchi wanaotumia kivuko cha Daraja la Makaburi ya Sabasaba Mtaa wa Jakaranda wameiomba halmashauri ya Jiji la Mbeya kuweka kipaumbele katika kuboresha huduma za kijamii  hususani miundombinu ya barabara, vivuko  kwani vingi vimekuwa hatarishi katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha Jijini hapa.

Wakizungumza na kituo hiki jana  kwa nyakati tofauti  walisema kuwa kivuko hicho kimekuwa chakavu kwa muda sasa licha ya kutoa taarifa  kwa viongozi wa serikali za mitaa.

Athanas Amosy,Mkazi wa Forest alisema ni vema halmashauri ikaliona hili na kulifanyia kazi kwani wananchi wengi  wamekuwa wakitegemea kivuko  hichi ambacho ni muhimu kwetu kwa shughuli mbalimbali za kiofisi na hata wafanyabishara kwani kimekuwa tishio pindi mvua zinapokuwa zikinyesha.

Mkazi wa Magereza Salome Adamson ,alisema wanaiomba  Serikali kuangalia namna ya kuboresha  miundombinu rafiki inayotumika na wananchi kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi katika maeneo ya mijini .

Akizungumza na gazeti hili ,Mwenyekiti wa Mtaa wa sabasaba Aidan Ng'oma alikiri kuwepo kwa changamoto hizo na kwamba alituma maombi   halmashauri  na kwamba uwenda ni miongoni mwa  miradi itakayoboreshwa kwa mwaka huu wa fedha .

"Kwani mkakati sio kuboresha kivuko hiki pekee  kipo kingine korofi katika eneo la ujenzi ambacho  ni miongoni vya vitakavyofanyiwa ukarabati"alisema.

Kwa upande wake ,Diwani wa kata ya Mbalizi Road,Adam Hussein alipohojiwa kuhusiana na malalamiko ya wananchi alisema kuwa  alikwisha wasilisha kwenye vikao vya baraza la madiwani na kwamba miongoni mwa  miradi iliyoingizwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/17 .

"Tayari halmashauri imetenga  fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata yangu ikiwa ni pamoja na kuboresha vivuko,miundombinu ya barabara korofi "alisema.
 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger