Hivi ndivyo Barabara ilivyokuwa kabla
Waandishi
wa Jiji wakiwa wamefika kuwashangaa wenzao wakiwa wanafanya kazi ya
kutejenga Taifa , wa pili kutoka kushoto ni Mwandishi wa Habari wa Bomba
Fm Radio Richard Kamanga aliyekuwa akifanya kazi ya kutengeneza
Barabara hiyo akiongea nao.
Baadhi
ya wamachinga na wananchi wa eneo hilo aibu zikiwa zimewashuka na
kuamua kushirikiana na Waandishi wa Habari kutoka Bomba Fm Radio na
Mbeya yetu Blog kuendelea kutengeneza njia hiyo
Waandishi wa Jiji wakiahidi kuleta kifusi kwa ajili ya kurekebisha Barabara hiyo
Wachina wakiwa wamefika eneo la tukio na kuahidi kuwa nao wataongeza nguvu katika ujenzi wa Barabara hiyo
Mchina akipata maelekezo juu ya Barabara hiyo
Hii ndio kazi kubwa inayoendelea kufanywa na Mbeya yetu Blog sambamba na Bomba Fm Radio .
Picha na Mbeya yetu
********************
Wakati
kazi ikiendelea baada ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya kuingia Mitini,
na tukio hili kuripotiwa muda mchache uliopita kupitia Mtandao huu na
Bomba Fm Radio huku waandishi hao wakiendelea ya kujenga Taifa ndipo
Ghafla waandishi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya walipoweza kufika na
kuwashangaa wenzao wakiendelea kupiga kazi na baada ya kuona aibu
waliamua kuahidi kuleta kifusi kwa ajili ya matengenezo ya Barabara
hiyo.
Nao
Baadhi ya wamachinga wapenda maendeleo waliweza kujitokeza kwa ajili ya
kuwaunga mkono waandishi wa habari walioanzisha kazi hiyo na kuwasaidia
kazi inayo endelea ya ukarabati wa kipande hicho cha barabara.
Wachina nao hawakuwa mbali baada ya kusikia ripoti ya tukio hili wakaamua kufika kujionea wenyewe, na wao kuahidi kutoa mchango wao wa kuweza kutengeneza barabara hiyo.
Wachina nao hawakuwa mbali baada ya kusikia ripoti ya tukio hili wakaamua kufika kujionea wenyewe, na wao kuahidi kutoa mchango wao wa kuweza kutengeneza barabara hiyo.
Hii
ndio Hali halisi ya Barabara ya Block T ambapo imeharibika na
kusababisha Dala dala kutaka kugomea kupita katika Eneo hilo kuhofia
kukwama.
Hii
ni sinto Fahamu ambapo wakati waandishi wa Habari waliojitolea
kurekebisha Barabara hiyo wakiendelea na kazi ya kuziba mashimo hayo ,
watumishi wa Jiji wenyewe walikuwa ndani ya Gari lao wamefunga vioo na
kushangaa kinacho endelea bila kuonesha ushirikiano wowote na Baadae
waliondoka, Jambo ambalo limewashangaza watu wengi, Huku wakiwa
wameahidi wangerekebisha Muundombinu huo.
Mmoja ya Gari dogo likiwa limesimama baada ya kuona kuwa Njia ni mbaya
Baadhi
ya Waandishi wa Habari Kutoka Bomba Fm wakishirikiana na Mbeya yetu
Blog wakianza kuchukua Kifusi na Kuziba Barabara hiyo.
Msimamizi Mkuu na Mwandishi wa Mbeya yetu Blog Joseph Mwaisango akiwa anaendelea na kazi ya kuziba eneo hilo lililoharibika
Hali halisi ya Njia hiyo
Mmoja
wa wasukuma Mkokoteni akiwa amejitosa kupita katika tope na kuendelea
na safari , kutokana na kwamba alikuwa hana Njia nyengine zaidi ya hiyo
Baadhi ya Waandishi wa Habari kutoka Bomba Fm Radio wakiendelea na Kazi
Kazi
imepamba moto ambapo waandishi wa Habari kutoka Bomba FM wakiwa
wamekomaa kuendelea kuziba mashimo katika barabara hiyo iliyo haribika
kwa kiwango kikubwa huku wakazi na wafanya biashara wa eneo hilo wakiwa
wanatazama bila kufanya juhudi zozote za kutengeneza, lakini wakisikia
kuna mgomo wanakuwa wakwanza kwenda andamana na shughuli za kijamii kama
hizi kuzisusia
Kazi
ikiwa inaendelea kwa kasi ili kupisha Magari yaanze kutumia Njia hiyo
huku Wakazi na wafanyabiashara wa eneo hilo wakiwa wanapaangalia tu, na
Jiji kufika hapo na gari lao bila kufanya kitu chochote
Kazi ikiwa inaendelea kwa kasi kubwa
Kila mmoja yupo bize
Kazi inaendelea kusonga mbele
Picha na Mbeya yetu
********************************
Mbeya
yetu Blog kwa ushirikiano mkubwa kabisa na Bomba Fm Radio (elimisha
burudisha) waamua kurekebisha kipande cha barabara inayo tumika
kupitia daladala zinazo toka uyole kuelekea s/kuu kipande hicho
kilichopo Block
'T'
Ushirikiano huo wa
vyombo hivyo viwili vya habari umekuja baada ya madereva wa daladala kutaka
kuweka mgomo kwaajiri ya kipande hicho cha barabara kuwa kibovu kinachokuwa ni tatizo kwa daladala hizo.
Wakati tukio hilo la ukarabati likiendelea Halimashauri ya Jiji la Mbeya
wamefika na kuwashangaa tu bila hata kuchukua hatua yoyote na hatimaye kuondoka
vivyo hivyo, wamachinga wa maeneo hayo pia wamegoma kutoa ushirikiano wakati
wakiambiwa kuhusu masuala ya mgomo huwa mbele kwaajiri ya kuchafua amani.
Bomba Fm Radio na mbeya yetu Blog wamechukua hatua hiyo ili
kuepusha migomo isiyo kuwa yalazima kutokana na kupenda amani na kuwajali
watanzania ambapo Halimashauri ya Jiji ilitoa ahadi ya kutengeneza lakini mpaka
sasa haijaweza kufanya jambo lolote kuhusiana na sehemu hiyo.
Mtazamo : Halimashauri
ya Jiji la Mbeya mnapo wahamisha watu kutoka sehemu moja kuelekea sehemu
nyingine tunaomba muhakikishe mmewawekea miundombinu ya kutosha ili kuepusha
mambo machache yanayo weza kuwa ni tatizo kwa wananchi
0 comments:
Post a Comment