Wachina nao hawakuwa mbali baada ya kusikia ripoti ya tukio hili wakaamua kufika kujionea wenyewe, na wao kuahidi kutoa mchango wao wa kuweza kutengeneza barabara hiyo.
BREAKING NEWS: LIVE MUDA HUU, WAANDISHI WA HABARI WA JIJI WAHAMASIKA BAADA YA MBEYA YETU BLOG PAMOJA NA BOMBA FM RADIO KUKARABATI KIPANDE CHA BARABARA BLOCK T
Wachina nao hawakuwa mbali baada ya kusikia ripoti ya tukio hili wakaamua kufika kujionea wenyewe, na wao kuahidi kutoa mchango wao wa kuweza kutengeneza barabara hiyo.
MAMA WANNE APELEKWA KATIKA KITUO MAALUMU NA WATOTO WAKE WAWILI WALIOBAKI KWA AJILI YA UANGALIZI.
UONGOZI wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kupitia kitengo cha Ustawi wa jamii umemtafutia kituo cha kulelea watoto wa mitaani cha Nuru Ophans Centre Mama aliyejifungua mapacha wanne na kubakia wawili baada ya kuugua Nimonia kwa ajili ya uangalizi wa karibu.
Hatua hiyo imekuja baada ya uongozi wa Hospitali hiyo kumfuata mama mwenye watoto hao Aida Nakawala(25) pamoja na mapacha wake waliobaki kutoka kijijini kwao Chiwanda Wilaya ya Momba mkoani hapa na kuwalaza hospitalini hapo kwa uangalizi wa karibu kwa muda wa zaidi ya wiki moja.
Aidha baada ya afya za watoto hao kuimarika kwa kiwango kikubwa pia Uongozi wa Hospitali hiyo imemtafutia hifadhi katika kituo cha kulelea watoto wa mitaani cha Nuru kilichopo Uyole jijini Mbeya kwa ajili ya uangalizi wa karibu kutoka kwa wauguzi na maafisa wa ustawi wa Jamii kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati akiwakabidhi watoto hao pamoja na mama yao kwenye uongozi wa kituo cha Nuru Orphans centre, Katibu wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Aisha Mtanda, alisema wameguswa na mazingira anayoishi mama huyo na kuamua kumpa uangalizi kwa miezi sita zaidi.
Alisema jukumu hilo halipaswi kufanywa na Hospitali kwa kuwa tayari walikuwa wamemaliza jukumu lao la kumhudumia alipokuwa ana matatizo lakini wamelazimika kubeba jukumu hilo baada ya kuguswa na mazingira na hali ya makazi ya familia hiyo.
Alisema Hospitali imekubaliana na uongozi wa Kituo cha Nuru kwamba apewe hifadhi mama huyo na watoto wake ili apate uangalizi wa karibu ikiwa na lengo la kunusuru maisha ya watoto waliobaki kutokana na wengine kupoteza maisha kiuzembe kwa ugonjwa wa Nimonia.
Aliongeza kuwa Hali ya hewa ya Mkoa wa Mbeya kwa siku zijazo kunakuwa na baridi kali sana hivyo watoto wasipokuwa kwenye uangalizi wa karibu wanaweza kupatwa na ugonjwa wa Nimonia tena kwa kukosa matunzo kama ya awali.
Kwa upande wake, Meneja wa Kituo cha Nuru, Amanda Fihavango alisema alikubali jukumu la kuwapokea watoto hao pamoja na mama yao kutokana na kuguswa na hali iliyowakuta ya kupotea kwa watoto wawili kati ya wanne.
Aliongeza kuwa ingawa anakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za kiuchumi atajitahidi kwahudumia kadri ya uwezo wake na kuomba wasamaria wema watakaoguswa na jambo hilo kujitolea kwa hali na mali kufanikisha kuokoa uhai wa watoto hao pamoja na wengine anaowalea.
Alisema kituo chake hupokea watoto waliookotwa baada ya kutupwa na wazazi wao au mama zao kufariki mara baada ya kutoka kujifungua ambao hupelekwa na Serikali kupitia Ustawi wa Jamii ingawa haichangii fedha zozote baada ya kuwapeleka.
Mtu yoyote mwenye kuguswa anaweza kuwasilisha mchango wake kituoni hapo au kuwasiliana na Meneja wa Kituo cha Nuru kupitia namba za Simu 0754 043004 kwa ajili ya kusaidia watoto hao pamoja na mama yao kuishi hapo kwa muda wa miezi sita.
TIMBWILI LAZUKA BAADA YA VIONGOZI WA SERIKALI KULA PESA ZA WANACHI.
MTENDAJI WA KIJIJI NA HALMASHAURI YA KIJIJI WATIMULIWA KIJIJI CHA IWIJI KWA UFUJAJI WA MBOLEA ZA RUZUKU
Kushoto Afisa tarafa Aaron Sote akipokea funguo toka kwa mtendaji Anton Ndisa |
Wananchi wakifuatilia mkutano huo kwa makini |
Saimoni Kasebele moja kati ya wajumbe kamati ya mbolea ambayo haikufanya kazi kijijini |
Moja kati ya wananchi ambao waliwekwa mahabusu na mtendaji baada ya kufuatilia mgao wa mbolea |
Wajumbe waliotimuliwa |
Mbolea inayosadikiwa kuibwa |
Kwa picha zaidi tazama hapa PICHA ZAIDI
Wananchi wa
kijiji cha Iwiji Kata ya Iwiji wilaya ya Mbeya wamemtimua Mtendaji wa Kijiji
hicho ambaye pia ni Kaimu Mtendaji Kata aliyefahamika kwa jina la Anthon Ndisa
kwa tuhuma za ubadhilifu wa Mbolea za ruzuku mifuko 189 iliyotolewa na serikali
kwa kipindi cha msimu wa 2013/2014.
Hatua hiyo
imechukuliwa na wananchi hao katika mkutatano wa hadhara uliofanyika kijijni
hapo ambapo Afisa Kilimo wilaya Marselin Mlelwa atitoa takwimu za mgao wa mbolea iliyotolewa Octoba 10
mwaka jana kwa kijiji hicho baada ya kupitishwa na Kamati ya Mbolea ya Wilaya
ambayo mwenyekiti wake ni Mkuu wa Wilaya.
Afisa Tarafa
ya Isangati Aaron Sote ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ndiye alisimamia
mkutano huo amesema kuwa Afisa kilimo ndiye mwenye jukumu la kutoa taarifa ya
mgao wa mbolea kama kamati ilivyopitisha.
Baada ya
kufunguliwa mkutano na Mwenyekiti
wa kijiji Patson Ngao Afisa Tarafa alimkaribisha Afisa Kilimo kusoma jinsi mgao
wa mbolea ulivyokwenda ambapo alisema Kitongoji cha Mabula kilipata mbolea ya
Dap mifuko 20 Urea 20, Kitongoji cha Iwiji Dap mifuko 8 Urea 20,Kitongoji cha
Soweto mifuko 6 Dap na Urea mifuko 16.
Kitongoji
cha Magole kilipata Dap mifuko 6 na Urea mifuko 16,Kitongojo cha Mtukula Dap
mifuko 6 na Urea mifuko 16 wakati Kitongoji cha Ntinga kilipata Dap mifuko 8 na
Urea mifuko 20 wakati Kitongoji cha Vimetu kikipata Dap mifuko 7 na Urea mifuko
20.
Katika mgao
huo kulikuwa na upungufu wa mifuko 50 ya Dap na Urea mifuko 36 ambayo wakulima
hawajapatiwa na kwamba ikifika wananchi wagawiwe ili kukamilisha idadi ya
mifuko 189 kwani hivi sasa mifuko iliyogawiwa ni mifuko 139 tu.
Baada ya
kusomwa taarifa hiyo wananchi walitaharuki wakidai kuwa hesabu hizo
zimetengezwa na Mtendaji Anthon Ndisa kwa manufaa yake kwani wananchi
hawajapata mbolea hiyo licha ya kutoa taarifa kwa uongozi wa Wilaya kupitia
Afisa Pembejeo Lupakisyo Masuba.
Kutokana na
kutoridhishwa na taarifa hiyo na kwamba wananchi wamehujumiwa na uongozi wa
kijiji kupitia viongozi wa vitongoji ambao walikiri kupokea mbolea hiyo na
kuigawa wakati kuna kamati mbolea ya kijiji ambayo ndiyo ilikuwa na jukumu la
kugawa ambapo uongozi wa kijiji ukidai kamati hiyo ilivunjwa.
Mmoja wa
wajumbe wa Kamati ya pembejeo Simon Kasebele amesema kuwa kati iliyokuwa na
wajumbe sita ambao ni Mwenyekit Venance Lwinga,Lucia Mose,Sara Kasalama,Patson
Kayelewe na Eva Makanika haikufanya kazi kutokana na agizo la Mtendaji aliyedai
kuwa kamati imevunjwa wakati siyo kweli bali ilikuwa ni njama za kuwahujumu
wananchi kwa manufaa yao.
Baada ya
majadiliano marefu wananchi waliamua kuirudisha Kamati ya Mbolea huku wakimtaka
Mtendaji kuondolewa haraka ili kuepusha ufujwaji wa mali za kijiji na kuwatimua
wenyeviti wote wa vitongoji na kumwacha Mwenyekiti wa kijiji pekee Patson Ngao
wakidai hahusiki na ubadhilifu kwani alizungukwa na Mtendaji kupitia wenyeviti
wa vitongoji.
Kwa upande
wake Afisa Kilimo Marselin Mlelwa amesema taarifa ataifikisha kwa Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ili kutoa maamuzi kwa vile Mtendaji ni Mwajiriwa hivyo
lazima taratibu za utumishi lazima zifuatwe.
Ili
kuhakikisha hakuna nyaraka zozote zinachukuliwa Ofisi Mwenyekiti na Kamati ya
Mbolea watafanyia shughuli zao katika ghala la Kijiji wakati Mtendaji aliagizwa
kubaki na funguo hadi hapo Halmashauri itakapotoa taarifa zake baada ya
ukaguzi.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Upendo Sanga amekiri kupokea taafa za
malamiko ya wananchi wa Iwiji na kuwataka kuwa na subira kwani serikali ina
utaratibu wake ambao lazima ufuatwe pindi mtumishi anapotuhumiwa kwa jambo
lolote ikiwa na pamoja na kuunda Tume ya Uchunguzi na Wakaguzi ili kupata
Ushahidi.
Uchunguzi
uliofanywa baada wananchi kulalamikia utaratibu uliotumika kugawa mbolea hiyo
Mtendaji wa Kijiji alirejesha mifuko 50 ya Dap ambayo imehifadhiwa kwa mmoja wa
Mawakala kijijini hapo ili kuficha ushahidi na kuonekana mbolea hiyo ilikuwepo
wakat ukweli ni kwamba mbolea hiyo tangu itolewe mwezi Octoba wananchi
hatanufaika nayo kwa kuwa msimu wa kilimo umepita na kijiji kukabiliwa na
hatari ya njaa.
Mbali ya
tuhuma ya Mbolea Mtendaji anatuhumiwa kufuja fedha za serikali na michango ya
wananchi kwa ajili ya kituo cha Afya hivyo wamemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri
anapofanya uchunguzi wa Mbolea afanye ukaguzi pia mradi wa Kituo cha Afya na
kama ikibainika Mtendaji na Halmashauri ya Kijiji wafikishwe kwenye vyombo vya
sheria.
Na Ezekiel Kamanga
|
Tuzo ya mwalimu bora duniani yazinduliwa
WANYANYASAJI WA WATOTO WAANZA KUCHUKULIWA HATUA MKOANI MBEYA.
|
Mwanahawa Nassoro(32) mkazi wa mtaa wa Airport Kata ya Iyela, ambaye anatuhumiwa kumtesa mtoto John Msumba |
Na Ezekiel Kamanga.
WATOTO WAWILI KATI YA MAPACHA WANNE WAMEFARIKI DUNIA, RAMBIRAMBI KUTOKA USWISI ZAPOKELEWA KIJIJINI KWAO.
Jeneza likiwa na mwili wa Marehemu tayari kwa Ibada ya Mazishi iliyofanyikia Nyumbani kwao Chiwanda. |
Mchungaji wa Kanisa la Africa Mission Church wanakosali wazazi wa Marehemu akiongoza ibada ya Mazishi. |
baadhi ya Waombolezaji wakielekea Makaburini. |
Joseph Mwaisango akiwa amebeba Jeneza lenye mwili ya marehemu kuelekea Makaburini tayari kwa safari ya mwisho |
Mwili wa Marehemu ukishushwa kaburini. |
Kaburi likifukiwa baada kukamilika kwa taratibu zote ambapo mwili wa marehemu ulizikwa katika makaburi ya Kijiji wanakozikwa Wananchi wengine. |
Kwa mujibu wa mila za kabila la Wanyamwanga vijana hawa walikuwa wakisiliba kaburi baada ya kumaliza mazishi. |
KATIKA hali ya kusikitisha Watoto wawili kati ya Wanne ambao ni mapacha waliozaliwa kwa pamoja na mwanamke Aida Nakawala Mkazi wa Kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya wamefariki dunia kwa ugonjwa wa Nimonia.
Watoto hao wamefariki kwa mida tofauti ambapo Mtoto wa Kwanza alifariki Nyumbani kwao baada ya kuugua ghafla ndipo hali za wengine zilipoanza kutia shaka na kulazimu Waandishi wa Habari wa Mtandao wa Mbeya Yetu, Gazeti la Jambo Leo na Redio ya Bomba Fm waliohudhuria mazishi ya Mtoto huyo kulazimika kuwakimbiza katika Hospitali ya Wazazi Meta kwa matibabu zaidi.
Hata hivyo baada ya kupokelewa kwa watoto hao Watatu mtoto mmoja aliaga dunia baada ya kuchelewa kupata matibabu kutokana na kubanwa na kifua na kusababisha kushindwa kupumua vizuri.
Hali za watoto wawili waliobaki wanaendelea vizuri na matibabu na kwa mujibu wa Daktari anayewatibu amesema taratibu za Hospitali hiyo ni kupokea watoto waliochini ya Miezi miwili lakini hao wamezidi umri huo hivyo badala ya kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya wataendelea kuwepo Meta hadi hapo hali zao zitakapoimarika.
Baadhi ya wananchi na wauguzi katika Hospitali ya Wazazi Meta wamesema sababu ya watoto hao kuugua ni kutokana na kukosekana kwa uangalifu wa karibu katika malezi ya watoto hao ukilinganisha na maisha ya vijijini kukosa watu wenye uelewa wa afya za watoto.
Wengine wameitupia lawama moja kwa moja Serikali kwa kushindwa kuchukua hatua za haraka tangu watoto walipozaliwa ili kujiridhisha na mazingira wanayopaswa watoto hao kuishi kwa kuwapatia msaada wa karibu na ushauri wa kitaalamu.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Mbeya, Thobias Mwalwego, alikiri kuwepo kwa urasimu katika Idara yao kwa madai kuwa tangu watoto hao walipokuwa wamezaliwa walipata taarifa na kuchukua hatua kwa afisa mmoja kufika kijijini na kuchukua picha zao.
Alisema urasimu unakuja kutokana na Ofisi ya Wilaya na Mkoa kukosa fungu la dharula ambapo barua za maombi zote hupelekwa makao makuu kwa Kamishna wa Ustawi wa Jamii ambapo Ofisi yake huchukua muda mrefu kurudisha majibu kutokana na waombaji kuwa wengi.
Alisema kila ofisi katika Ngazi ya Mkoa ingekuwa na fungu la Dharula kama ilivyo katika Ofisi zingine hali ambayo ingeweza kusaidia kuepusha vifo vya watoto hao kutokana na kupatiwa msaada wa ushauri na makazi rafiki kwa malezi ya mapacha wanaozidi wawili.
Aidha alishauri kila Halmashauri Nchini kutenga bajeti za kusaidia majanga kama hayo na vitu vya dharula wakati Serikali inajipanga kutekeleza kutokana na taratibu zake kuchukua muda mrefu ili kuweza kukabiliana na hali yoyote na muda muafaka.
Akikabidhi msaada huyo kwa mama huyo kijijini kwao Chiwanda Wilayani Momba, Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) Kanda ya Nyanda za Juu kusini, Ahmed Issa kwa niaba ya Watanzania hao alisema wameguswa sana na hali hiyo na kuahidi kuendelea kuchangia kila mara.
Aidha alisifu utendaji kazi wa Waandishi wa Habari hususani Mbeya yetu Blogwaliofanikisha kuibua jambo hilo na kulitolea taarifa kila wakati jambo lililosaidia kufahamisha watu wengi wakiwemo wanaoishi nje ya Tanzania na kutuma kile wanachokuwa wameguswa nacho.
Mbali na Hilo, Meneja wa TMA Kanda ya Mbeya, Ahmed Issa, pia amejitolea kuusafirisha mwili wa Marehemu kutoka Hospitali ya Meta Mbeya hadi Kijijini kwao Chiwanda Wilayani Momba kwa ajili ya taratibu za Mazishi.
|