Picha hii imetumika kupamba habari, lakini haijachukuliwa katika eneo husika la habari hii.
Na Ezekiel Kamanga.
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya Daktari Gerald
Yubaha amewataka wanawake kujitokeza kwa wigi katika zahanati,vituo vya
Afya na Hospitali ili kupima afya zao ili kubaini na kuondoa ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi Wilayani humo.
Yubaha ameyasema
hayo katika maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani iliyofanyika
Kiwilaya katika Hospitali ya Wilaya iliyopo Itumba Mei 12 mwaka huu
ambapo Wauguzi na wahudumu wa Afya walifanya maandamano ya kumkumbuka
Muuguzi wa kwanza Duniani ambapo maandamano hayo yalipokelewa na Mkuu wa
Wilaya Rosemary Senyamule.
Kaimu
Mganga Mkuu amesema kuwa baadhi ya changamoto ni pamoja na ukosefu wa
mashine za kupimia vipimo katika Wilaya ambazo zingebaini magonjwa
mbalimbali yakiwemo ya shingo ya uzazi kwa akina mama kwani kwa sasa
huduma hiyo huipata katika hospitali ya wazazi Meta iliyopo Jijini Mbeya
na Hospitali yake hutumia gharama kubwa kuwasafirisha wagonjwa
wanaowabaini.
Tangu kuanza
kutolewa elimu ya ugonjwa wa shingo ya uzazi wagonjwa wanne walibainika
na ugojwa huo ambapo wawili kati yao walifariki kutokana na kuchelewa
kupata matibabu na wawili walisafirishwa hadi Mbeya ambapo wanapatiwa
matibabu katika Hospitali ya Wazazi ya Meta.
Katika
maandamano wauguzi hao walibeba mabango mbalmbali ili kufikisha ujumbe
kwa serikali ambayo baadhi yakidai malimbikizo ya stahiki mbalimbali
wanazodai watumishi wa sekta ya Afya ambayo hayajalipwa kwa muda mrefu.
Akijibu
kero hizo za Wauguzi Mkuu wa Wilaya alisema Serkali imejitahidi siku
hadi siku kuhakiksha wanalipa malimbikizo yao kwa wakati kadri fedha
zinapopatikana kwani serikali haipo tayari haipo tayari kuona watumishi
wake wanaishi maisha duni.
Alisema Serikali ina
majukumu mengi ikiwa ni pamoja na upanuzi wa Hospitali hiyo ambapo
ujenzi unaendelea ili kuwaondolea adha ya wananchi wa wilaya hiyo badala
ya kusfiri umbali mrefu na wengi hupoteza maisha kwa kukosa gharama za
kuwasafirisha ndugu zao wanapokuwa wanahitaji matibabu zaidi Mbeya.
Aliwataka
kuendelea kuwa wavumilvu na kuwapongeza kwa moyo wa uzalendo ambao
wamekuwa wakifanya wa kutoa huduma licha ya kufanya kazi katika
mazingira magumu na kuwajali wagonjwa wanaofika hosptalini kwa ajili ya
kupata huduma.