Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Dr, Jakaya Kikwete akiinua jembe na nyundu kwa maana ya nembo ya chama hicho mara baada ya kuingia uwanjani.
Jakaya Kikwete alipokuwa akianza kutoa hotuba mara baada ya kuingia katika uwanja huo.
baadhi ya viongozi wa chama hicho wakimshangilia mwenyekiti Jakaya Kikwete alipokuwa akiingia uwanjani.
Raisi Kikwete alipokuwa akiingia katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine kwaajili ya maadhimisho hayo.
............................................................................................................
Mwenyekiti wa chama cha
mapinduzi Dr, Jakaya Mrisho Kikwete amewataka viongozi na wanachama wa chama hicho,
kuwa karibu na wananchi kwa lengo la kusikiliza matatizo ya wananchi na
kuyatatua, kwakufanya hivyo itakuwa chachu ya wananchi kukiamini chama.
Kikwete ameyasema hayo
alipokuwa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 37 tangu kuanzishwa kwake
yaliyofanyika leo katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Kikwete amesema kumekuwa na
tabia kwabaadhi ya viongozi wa chama hicho kutotatua matatizo ya wananchi pindi
wanapopewa taarifa kuhusu kero hizo.
Aidha Kikwete amempongeza
katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana kwakufanya ziara katika
mikoa ya nyanda za juu kusini iliyoleta mafanikio makubwa katika cha hicho.
Amesema Kinana katika ziara
yake alikuwa akisikiliza matatizo ya wananchi na kuyatafutia ufumbuzi, pia
amekuwa nao wananchi bega kwa bega katika Nyanja mbali mbali.
Pia Kikwete amesema mpango wa chama cha
Mapinduzi ni kuboresha maisha ya watanzania katika sekta mbali mbali
ikiwa pamoja na maji, umeme, elimu afya na miundombinu.
0 comments:
Post a Comment