Pages


MJANE WA MIAKA 60 ANAOMBA MSAADA WA KUTIBIWA MKONO WAKE ULIYOANZA KUHARIBIKA BAADA YA KUJERUHIWA NA NYOKA.

Kamanga na Matukio | 02:05 | 0 comments

Mwanamke Mjane FAINES NAMBEYE KAONGA [60] Mkazi wa kijiji cha IGUNDU Kata ya SANGAMBI Wilaya ya CHUNYA Mkoani MBEYA anawaomba wasamaria kumchangia pesa kwa ajili ya kupata matibabu baada ya kujeruhiwa  na nyoka alipokuwa amelala  chumbani kwake.
Hivi ndivyo mkono wake ulivyo kwa sasa
Mwanamke mmoja Mjane aliyefahamika kwa jina la FAINES NAMBEYE KAONGA [60] Mkazi wa kijiji cha IGUNDU Kata ya SANGAMBI Wilaya ya CHUNYA Mkoani MBEYA anawaomba wasamaria kumchangia pesa kwa ajili ya kupata matibabu baada ya kujeruhiwa  na nyoka alipokuwa amelala  chumbani kwake.

Mjane huyo alijeruhiwa mkono wa kushoto na nyoka alipokuwa amelala chumbani kwake hivi karibuni na kusababisha ngozi kutoka hali iliyomsababishia maumivu makali ambapo alikimbizwa Hospitali ya Wilaya ya CHUNYA na kupatiwa matibabu lakini mpaka sasa hali inazidi kuwa mbaya.

FAINES  amesema pamoja na kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya na kuruhusiwa kurudi nyumbani mkono umezidi kuliwa na sumu na kusababisha ngozi kutoka hadi mfupa kutokeza nje ya ngozi hali inayomtia hofu siku hadi siku.

Mama huyo hana pesa za kuweza kupata matibabu zaidi kutokana nayeye kufiwa na mumewe na wanawe hawana uwezo wa kugharamia matibabu katika Hospitali nyingine hivyo kuwaomba wasamaria wema kumsaidia ili aweze kuokoa maisha.

Baadhi ya majirani wamesema mama huyo ameumwa na nyoka siku za hivi karibuni akiwa amelala chumbani kwake na alipopelekwa kupatiwa matibabu hajapata ahueni na afya yake imezidi kuzorota siku hadi siku hali akishindwa kufanya kufanya shughuli za kiuchumi

Picha na Ezekiel Kamanga


Kwa atakaeguswa  kumsaidia mjane huyu wasiliana 
na

0754 49 07 52
AU
0754 37 44 08

Waziri wa afya na ustawi wa jamii Dk. Hussein Mwinyi amezindua kipimo cha malaria.

Kamanga na Matukio | 02:04 | 0 comments


Dk. Mwinyi akihutubia.
Waziri wa afya na ustawi wa jamii Dk. Hussein Mwinyi amezindua kipimo cha malaria kinachotoa majibu ya haraka katika vituo binafsi vya kutolea huduma za afya.


Kipimo hicho ambacho tayari kinafanya kazi katika vituo vya afya vya serikali, kinatoa majibu kwa muda wa dakika 15 tangu mgonjwa kuanza kutolewa damu.


Akiongea katika uzinduzi huo, Dk Mwinyi amesema kuzinduliwa kwa kipimo hicho kinachojulikana kama MRDT wana lengo la kupambana na Malaria na kusogeza huduma kwa wananchi wote kwa gharama nafuu.


Dk. Mwinyi amewataka wananchi kuacha tabia ya kutumia dawa za malaria bila kupima hata kama utakuwa na dalili za homa badala yake mgonjwa afike katika kituo cha afya kilicho karibu yake kwa uchunguzi zaidi. 


Ameongeza kuwa gharama ya kupima kwa kipimo hicho haitakiwi kuzidi shilingi 1,100 na kwamba serikali imejipanga vizuri kuwadhibiti watoa huduma wa afya wa sekta binafsi watakaozidisha bei kinyume na maelekezo ya serikali.


Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha uchunguzi na tiba ya malaria katika mpango wa taifa wa kudhibiti malaria nchini Dk. Sigsbert Mkude amesema kipimo hicho kimefanyiwa utafiti wa kina na kuonekana kuwa kinafa japo kuna baadhi ya changamoto kwa baadhi ya wagonjwa.


Kutokana na taarifa ya utafiti katika jamii THMIS katika kipindi cha miaka mitano, maambuki ya ugonjwa wa malaria yamepungua kwa zaidi ya asilimia 50 kutoka asilimia 18 mwaka 2007/2008 hadi asilimia 9 mwaka 2011/2012.

Theo Walcott ameshangazwa na jeraha la kichwa alilopata mchezaji mwenzake Wayne Rooney.

Kamanga na Matukio | 02:03 | 0 comments
Mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza, Theo Walcott ameshangazwa na jeraha la kichwa alilopata mchezaji mwenzake Wayne Rooney na kusababisha kumuweka nje ya kikosi cha timu ya taifa ya nchi kitakachopambana na Moldova na Ukraine katika kutafuta tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia.



Rooney aliondolewa katika kikosi cha Manchester United ambacho kilichapwa bao 1-0 na Liverpool katika Uwanja wa Anfield baada ya jeraha hilo kwa bahati mbaya wakati wa mazoezi.



Meneja wa United David Moyes alithibitisha nyota huyo kukosekana kwa kipindi cha wiki tatu au zaidi hivyo kumuacha kocha wa Uingereza Roy Hodgson kukosa huduma ya mchezaji huyo.



Akihojiwa Walcott amesema aliona picha ya sehemu alipoumia Rooney na kustushwa huku akidai kuwa sio kitu kizuri kukitazama akifananisha na sinema za kutisha.

Hata Hivyo Walcott ana imani kuwa wapo wachezaji wengine imara wanaoweza kuisadia nchi hiyo kushinda mechi zake zote mbili muhimu kwa ajili ya kufuzu.



Wakati huohuo, mabingwa wa soka barani Ulaya na Ujerumani, klabu ya Bayern Munich wametangaza kuwa kiungo wake nyota Javi Martinez amefanyiwa upasuaji wa kinena wenye mafanikio.



Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa hiyo imedai kulikuwa na ulazima wa kiungo wa kimataifa wa Hispania kufanyiwa upasuaji huo baada ya mara kwa mara kulalamika kuwa na tatizo hilo.



Martinez ambaye aliingia uwanjani akitokea benchi na kufunga bao la kusawazisha katika dakika za majeruhi katika muda wa nyongeza wiki iliyopita katika mchezo wa Supercup dhidi ya Chelsea kabla ya Bayern kushinda mechi hiyo kwa changamoto ya mikwaju ya penati.



Kocha wa Hispania Vicente del Bosque hakumjumuisha kiungo huyo katika kikosi chake ambacho kinakabiliwa na mechi ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Finland na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Chile.

Mashabiki wa soka nchini wametakiwa kuwa nyuma ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars.

Kamanga na Matukio | 02:03 | 0 comments
Mashabiki wa soka nchini wametakiwa kuwa nyuma ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ambayo inakabiliwa na mchezo wa mwisho wa kuwani nafasi ya kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia dhidi ya timu ya taifa ya Gambia mwishoni mwa juma hili.

Rai hiyo kwa mashabiki wa soka, imetolewa na katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini TFF Angetille Osiah ambapo amesema kuna haja kwa watanzania kuendelea kuwa nyuma ya Taifa Stars licha ya kukosa nafasi ya kufuzu kucheza fainali hizo ambazo zitaunguruma mwakani nchini Brazil.

Amesema mchezo dhidi ya Gambia una umuhimu mkubwa kama alivyosema kocha mkuu wa Taifa Stars Jan Poulsen wakati akizungumza na waandishi wa habari hapo jana.

Wakati huo huo timu ya taifa ya Tanzania imeondoka hii leo kuelekea mjini Banjul nchini Gambia tayari kwa mchezo dhidi ya wenyeji wao ambao umepangwa kufanyika Septemba 07.

Kikosi kilichoondoka kinamjumuisha nahodha na mlindamlango wa Taifa Stars Juma Kaseja, Mwadini Ali, Ali Mustafa, Amri Kiemba, David Luhende, David Mwantika, Erasto Nyoni, Frank Domayo, Haruni Chanongo, Henry Joseph, Jonas Mkude, Juma Liuzio, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa, Nadir Haroub, Said Dilunga, Simon Msuva na Vincent Barnabas.

JANGWANI;- Kamati ya wazee wa klabu ya Yanga wadai hawamtambui Katibu mkuu mpya...

Kamanga na Matukio | 02:01 | 0 comments
Siku moja baada ya uongozi wa klabu ya Dar es salaam Young Africans kudaiwa kumuajiri katibu mkuu mpya badala ya Lawrence Mwalusako, kamati ya wazee wa klabu hiyo wameibuka na kudai hawamtambui katibu huyo ambae ni raia kutoka nchini Kenya.



Katibu wa kamati ya wazee wa klabu hiyo Ibrahim Akilimali amesema kama ni kweli viongozi wa ngazi za juu wameamua kufanya maamuzi ya kumuajiri katibu huyo anaejulikana kwa jina la Patrick Nagi wanatakia kutambua wamekiuka kanuni na taratibu zilizoainishwa kwenye katiba inayowaongoza.



Uongozi wa klabu ya Simba umeendelea kutoa tahadhari kwa wafanyabiashara nchini wanaoendelea kukiuka taratibu za kuuza bidhaa zenye nembo ya klabu hiyo inayotambulika kisheria.



Mwenyekiti wa baraza la wadhamini la klabu ya Simba Khamisi Kilomoni kwa muda mrefu wamekua wakitoa tahadhari hiyo kwa wafanyabiashara wakubwa na wale wadogo lakini imeonekana wanadharaulika, hivyo kwa sasa wameamua kutumia nguvu za kisheria kwa lengo la kukomesha biashara hiyo haramu.



Naye Insepekta wa Jeshi la Polisi Mohamed Manyae amesema baada ya kufuatwa na uongozi wa klabu ya Simba na kulalamikia juu ya biashara inayoendelea kufanywa na wafanyabiashara nchini ya bidhaa za klabu hiyo, wameamua kuwa bega kwa bega na uongozi huo kwa lengo la kumaliza tatizo hilo.
 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger