Mtuhumiwa Baraka Mwandibwa(kulia) ambaye amehukumiwa miaka 35 kwenda jela kwa kosa la mauaji.(Picha na Ezekiel Kamanga, Mbeya)
Na Ezekiel Kamanga, Mbeya
MAHAKAMA kuu kanda ya Mbeya imemhukumu Baraka Mwandibwa kwenda jela miaka 35
mtuhumiwa wa mauaji dhidi ya watoto huku mwingine akiachiwa huru baada ya
kukutwa bila hatia.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Jaji wa Mahakama kuu kanda ya
Mbeya Samweli Karua mbele ya mwendesha mashtaka wa serikali Archiles Mulisa
katika vikao vilivyofanyika katika Mahakama ya wilaya ya Rungwe.
Awali mwendesha mashtaka wa serikali Archiles Mulisa
aliiambia mahakama kuwa washtakiwa Baraka Mwandibwa na Zuberi Lwila
walifikishwa mahakamani hapo wa kosa la kumlawiti na kumuua mtoto Esta James(5)
Novemba 21, 2010.
Alisema kosa hilo ni kinyume cha sheria kifungu cha 196 (16)
kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002, ambalo walilifanya katika kijiji cha
Bulyaga Wilayani Rungwe baada ya kumteka mtoto huyo.
Akisoma hukumu hiyo Jaji Karua alisema Mshtakiwa namba moja
anatiwa hatiani kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo ambao ulitoka
kwa shahidi namba moja ambaye ni mtoto aliyejulikana kwa jina la Marietha.
Alisema mtoto huyo ambaye alisema siku ya tukio alikuwa
akicheza na marehemu ambapo mtuhumiwa alifika na kumpa pipi aina ya Ivory
marehemu kisha kuondoka naye ambapo shahidi huyo aliwerza kumtambua mtuhumiwa
katika gwaride la utambuzi.
Mbali na hilo alisema ushahidi mwingine ni ushaidi wa
Vinasaba ambao unawahusisha moja kwa moja watuhumiwa wote wawili ikiwa ni
pamoja na ushaidi wa kimazingira unaomhusisha mtuhumiwa wa kwanza.
Alisema kutokana na ushahidi huo Mtuhumiwa wa kwanza
anahusika moja kwa moja na mahakama inamtia hatiani ingwa kwa mujibu wa
ushahidi hakuua kwa makusudi kutokana na kutokuwa na vifaa vya mauaji kama visu
panga na silaha zingine.
Alisema katika mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa unadamu na
mbegu za kiume sehemu zake za siri na hakuwa amejeruhiwa nsehemu yoyote, hivyo
mahakama iliona mtuhumiwa hakuua kwa kukusudia bali ilikuwa ni bahati mbaya.
Hata hivyo upande wa Mshtaka uliomba mahakama itoe adhabu
kubwa na kali dhidi ya washtakiwa kutokana na mazingira aliyofanyiwa mtoto huyo
ili iwe fundisho kwa wanaume wengine wenye tabia za kuwalaghai watoto wadogo.
Akitoa hukumu hiyo Jaji karua alisema anakubaliana na
ushauri wa upande wa mashtaka kwamba tukio hilo ni kubwa na mstakiwa wa kwanza
Baraka Mwandibwa ataenda jela kwa miaka 35 huku mshtakiwa wa pili Zuberi Lwila
akiachiwa huru baada ya kutokuwa na ushahidi wa kuhusika katika tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment