Pages


HII HATARI TUPU,NA NI AIBU KUBWA SANA KWA WIZARA HUSIKA TAFUTENI NJIA MBADALA

Kamanga na Matukio | 03:20 | 0 comments
Hii ndiyo hali halisi ya bucha katika mnada wa Mbuyuni,wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wahusika.Je,Wizara husika mwaionaje hii hali na hatua gani mwazichukua ili kuhakikisha afya za walaji zinaimarika baada ya kudhoofika?
Hapa nyama tayari ipo buchani kilo sh 2000 mambo yanaendele mnada wa Mbuyuni, wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.
Kazi ni kazi nae mnoa visu anaendelea na kazi yake katika mnada huo.
Mmh picha inajieleza yenyewe mambo ya mnadani hayo.
Hili ndilo eneo la kupata chakula cha aina mbalimbali katika mnada huo wa Mbuyuni Chunya. Kwa hisani ya Mbeya Yetu Blog.

POLISI YAMNASA MTU MMOJA RAIA WA KENYA KWA KUHUSIKA NA SHAMBULIO DHIDI YA DKT. ULIMBOKA.

Kamanga na Matukio | 05:32 | 0 comments



Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Suleiman Kova.
Na.MO BLOG TEAM
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linamshikilia mtu mmoja raia wa Kenya kwa tuhuma za kuteka nyara na shambulio la kudhuru mwili dhidi ya Dkt. Stephen Ulimboka lilifanyika tarehe 26 Juni 2012.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum Suleiman Kova amesema mtu huyo aitwaye Joshua Gitu Mhindi mwenye umri wa miaka 31, ana kitambulisho cha utaifa Na.29166938 kilichotolewa Nyeri na hati ya kusafiria ya dharura Na.0123431 iliyotolewa Namanga Kenya.

Kamanda Kova amesema katika mahojiano na polisi mtu huyo alieza kwamba yeye ni mwanachama wa kikundi cha kihalifu kinachojulikana kama GUN STAR chenye makao yake eneo la RUIRU wilaya ya Thika nchini Kenya na kudai kuwa kinaongozwa na mtu mwenye jina la utani SILENCE akisaidiwa na PAST, ambao wamekuwa wakifanya matukio mengi ya kihalifu nchini Kenya.

Mtu huyo alipohojiwa zaidi alisema alikuja Tanzania na wenzake 12 kwa lengo la kumdhuru Dkt. Stephen Ulimboka baaada ya kukodiwa na mtu ambaye hakumtaja jina, ambaye anaamini kuwa ni mtumishi wa serikali.

Polisi inaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini wengine waliohusika.

MBWA AVAMIA NYUMBA NA KULALA KITANDANI.

Kamanga na Matukio | 05:29 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Katika hali isiyoyakawaida Mbwa mmoja asiyefahamika mmiliki wake,amevamia nyumba ya Bwana Michael Nkeka(52) ambaye Mkazi wa Nsalaga Uyole,Jijini Mbeya na kulala kitandani.

Tukio hilo limetokea Julai 12 mwaka huu majira ya saa 1 jioni,wakati mmiliki huyo akiwa amerejea nyumbani kutoka matembezini alifungua mlango wa nyumba yake ndipo Mbwa huyo alipoingia ndani na kupitiliza moja kwa moja mpaka chumbani kisha kulala.

Juhudi za kumuondoa mbwa huyo ziligonga mwamba ndipo Bwana Nkeka alipoamua kwenda kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Mtaa,Bwana Peter Ngonde ambapo hakukuwa na mafanikio yoyote hali iliyowapelekea kufikisha taarifa katika Kituo cha Polisi Uyole.

 Aidha,Polisi wa kituo hicho walieleza kuwa wamuache mbwa huyo huenda akaondoka mwenyewe lakini hali ikawa ndivyo sivyo kutokana na kulala mpaka asubuhi majira ya saa 3 ya Julai 13 mwaka huu.

Hata hivyo tukio hilo la aina yake limehusishwa na imani za kishirikina na hakuna tukio lolote la kuhatarisha.

Wakati huohuo mtoto mmoja Edrick Mwashiuya(2),mkazi wa Kijiji cha Halambo,Kata ya Halumbu Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya amefariki dunia baada ya kudondokea katika uji wa moto uliotengenezwa maalum kwa ajili ya kutengenezea pombe ya kienyeji.

Diwani wa kata hiyo Samson Simkoko amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea majira ya saa asubuhi ya Julai 13 mwaka huu na kwamba Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio kwa uchunguzi.

JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LIMEFANIKIWA KUDHIBITI MAANDAMANO.

Kamanga na Matukio | 05:29 | 0 comments
 Na Sjomi Mtaki, Tunduma.

Jeshi la polisi mkoani Mbeya limefanikiwa kudhibiti maandamano makubwa ya baadhi ya wananchi yaliyokuwa yamepangwa kufanyika mjini hapa kinyume na sheria.
 
 Lengo la mpango huo ulikuwa ni kufikisha ujumbe kwa serikali ili iweze kukarabati au kujenga sehemu ya kipande cha barabara chenye urefu wa wa kilometa moja kinacho anzia maeneo ya Customs hadi kanisa la Roma katika barabara ya iendayo Sumbawanga.
 
 Tukio hilo lilitokea hivi karibuni majira ya alfajiri mjini hapa wakati kikosi cha polisi cha kuzuia fujo (FFFU}  kikiongozwa na kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya,kilisambazwa katika maeneo mbalimbali ya mitaa ya mjini hapa.
 
 Askari hao ambao walitumia magari matatu aina ya Land Rover yenye namba za usajili TP 1465,TP 1466 na TP 2079 walikuwa wamevalia mavazi rasmi kwa ajili ya kukabiliana na jambo lolote la uvunjivu wa amani walionekana kuchukua tahadhari
 kukabiliana na hatua za uvunjifu wa amani kama ungetokea.
 
 Taarifa za awali zilizopatikana kutoka katika eneo la tukio,zilidai kuwa pamoja na kuwepo mpango huo wa maandamano pia wananchi hao waliazimia kufunga barabara ya Tunduma unbawanga kwa muda usiojulikana ili kuzuia magari yasipite kwenda Mbeya na nchi jirani ya Zambia.
 
 Diwani wa kata ya Tunduma Franck Mwakajoka,alisema wananchi hao wanahaki ya kudai ujenzi wa barabara hiyo kwa kuwa sehemu hiyo ipo katika mpango wa ujenzi wa  mradi mkubwa wa ujenzi wa barabara ya Tunduma hadi Sumbawanga.
 
 Mwakajoka alisema inashangazwa kuona sehemu hiyo ya barabara haijaguswa na mkandarasi wa ujenzi,ambaye alinzia kujenga mbele ya eneo hilo na kuacha sehemu hiyo ambayo kwa sasa iko katika hali mbaya ikiwa na mashimo mengi.
 
 Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Diwani Athumani,alisema kikosi hicho kilifika mjini humo baada ya kupata taarifa za uhakika kuhusiana na mwenendo mzima na athari ambazo zingeweza kujitokeza kwa raia na wafanyabiashara.
 
 Alisema taarifa hizo zilfikishwa na kujadiliwa katika kamati ya ulinzi na usalama chini ya mwenyekiti wake mkuu wa mkoa huo Mheshimiwa Abas Kandoro,ambaye alitoa magizo kwa meneja wa Tanroad mkoani mbeya kwenda eneo hilo ili kutoa majibu sahihi ya madai ya wananchi hao.
 
 ,”Ukweli mpango huo hakuwa halali na huenda ungesababisha usumbufu mkubwa kwa raia wasiokuwa na hatia,wasafiri wangepata usumbufu mkubwa na biashara zingesimama kufuatia hali hiyo bila shaka vurugu zingeweza kujitokeza,”alisema.
 
 Kwa upande wake meneja wa barabara nkoani Mbeya James Nyabakali alieleza “Uhuru”kuwa mdai ya wananchi hao yamepata ufumbuzi kwa kuwa sehemu hiyo ya barabara itaanza kufanyiwa ukarabati baada ya miezi miwili ijayo.
 
 kuunganisha ujenzi wa sehemu ya barabara hiyo itafuatwa baada ya serikali kufanya upembuzi yakinifu kwa kuwa katika eneo hilo kuna mali za watu.
 
 Mji wa Tunduma umekuwa kinara  kwa kuwa na maandamano ya mara kwa mara ambayo baadhi yake imekuwa ikileta athari kubwa kwa upande wa jamii,hivyo kuleta tishio kwa baadhi ya wafanyabiashara kuuimbia mji huo.

HATIMAYE SIMBA YATWAA KOMBE LA URAFIKI UWANJA WA TAIFA

Kamanga na Matukio | 05:47 | 0 comments

Waziri asiye na Wizara maalum Zanzibar Mh. Machano Othman Said akimkabidhi kombe la ubingwa wa michuano ya Urafiki nahodha wa timu ya Simba Juma K. Juma mara baada ya timu ya Simba kuifunga timu ya Azam FC magoli 5-3 kwa penati,  baada ya kutoka suluhu magoli 2-2 katika kipindi cha dakika tisini, kwenye mchezo mzuri na wa kuvutia kwa timu zote uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa leo hivyo kuifanya Simba kuibuka mabingwa wa kombe hilo.
Wachezaji wa timu ya Simba pamoja na kocha wao wakipiga picha pamoja na kombe lao walilolikabidhiwa leo kwenye uwanja wa Taifa baada ya kuifunga timu ya Azam FC katika michuano ya Urafiki inayoandaliwa visiwani Zanzibar.
Wachezaji wa timu ya Simba wakisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuchukua ubingwa wa kombe la Urafiki.
Wachezaji wa timu ya Azam FC nao wakisalimiana na viongozi mpira wa miguu kutoka Zanzibar pamoja na mgeni rasmi.
Wachezaji wa timu ya Simba wakishangilia mara baada ya kuifunga timu ya Azam FC kwenye uwanja wa Taifa.
Wachezaji wa timu ya Simba wakimnyanyua juu juu golikipa wao Juma K. Juma baada ya kupangua penati mbili katika mchezo huo uliokuwa wa fainali katika michuano ya Urafiki.
Ubao wa matangazo ukionyesha Simba 5 Azam FC 3 kwenye uwanja wa Taifa.
Mchezaji wa kimataifa wa timu ya Simba kutoka nchini Zambia Felix Sunzu akichuana vikali na beki wa timu ya Azam FC katika mchezo huo.
Mashabiki wa timu ya Azam FC wakishangilia timu yao.
Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia timu yao.
Kwa hisani ya http://ujanatz.blogspot.com

CHIFU MERERE II MATATANI TENA,ADAIWA KUCHUKUA PESA NYINGINE.

Kamanga na Matukio | 05:45 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Chifu Merere II wa kabila la Wasangu,ameingia matatani tena baada ya kudaiwa kuchukua pesa kutoka kwa familia ya marehemu Frank aliyefariki juzi Julai 11 mwaka huu katika Kijiji cha Ijumbi,Kata ya Ruiwa,Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya.

Chifu huyo alitakiwa kurejesha fedha zilizotumika katika tambiko ili marehemu huyo apone,lakini hali ikawa tofauti na kufariki,kufuatia tukio hilo wananchi waliandamana na kumtaka chifu huyo kurejesha pesa na kutishiwa kuzikwa akiwa hai.

Aidha Merere II alizilipa pesa hizo katika uongozi wa kata hiyo,pamoja na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha wilaya hiyo na baadae kuachiwa huru.

Hata hivyo jana Chifu Merere II aliifuata familia ya marehemu Frank na kuitaka kutoa shilingi 250,000,akidai fidia ya pesa hizo alizokuwa amezirejesha Julai 11 ndipo wananchi waligadhibika na kutaka kumkamata.

Wakati tukio hilo likiendelea Afisa Mtendaji wa kata hiyo Bwana Jordan Masweve akiwa na sungusungu walimuokoa Chifu huyo kutoka nyumbani kwake na ku,hifadhi katika ofisi ya kata,huku ulinzi mkali ukiwa umeimarishwa.

AFISA MTENDAJI WA KIJIJI MATATANI KWA KUFUJA PESA NA MIFUKO YA SARUJI.

Kamanga na Matukio | 05:45 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Afisa mtendaji wa Kijiji cha Idimi,Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya Bwana Amon Myola,ameingia matatani kwa tuhuma za kufuja pesa za michango shilingi 190,000 kati ya shilingi 746,000 pamoja na mifuko 16 kati ya 30 iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini Mchungaji Luckson Mwanjale.

Hayo yamebainishwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika Julai 12 mwaka huu kijijini hapo na kusimamiwa na Afisa Utumishi wa halmashauri ya wilaya hiyo Bwana Kernslave Wensle Mpoto.

Pesa hizo zilichangwa na wananchi kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Idimi iliyoezuliwa Desemba 24 mwaka uliopita.

Aidha imedaiwa kuwa Bwana Myola,amekuwa akiendesha kamati ya ujenzi wa shule pekee yake hali iliyopelekea kuwepo kwa hasara na wananchi kugomea kuendelea kutoa michango ambapo matarajio ilitakuwa kukusanywa shilingi milioni 11.

Katika Mkutano huo aliagizwa na Afisa Utumishi Bwana Mpoto kuzirejesha fedha hizo na mifuko hiyo ya saruji katika mkutano wa hadhara ujao utakaofanyika Julai 20 mwaka huu.

Hata hivyo juhudi za kumuondoa madarakani Mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Yohana Bahati na halmashauri yake,zilishindikana baada ya tuhuma zilizowasilishwa katika Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Mbeya kukosa nguvu za kumtia hatiani.

Agizo likatolewa kwa viongozi wa vitongoji kuhakikisha michango yote inayochangwa na wananchi imewasilishwa kwa Afisa Mtendaji wa Kata kabla ya tarehe hiyo iliyopangwa kwa ajili ya mkutano ujao wa hadhara.

WAKATI SISI TUNAPOWAONA NYOKA TUNAWAOGOPA HEHE, DUUH HUKU WENZETU WANAFANYA KITOWEO!

Kamanga na Matukio | 05:44 | 0 comments

WAKIWEZESHWA WANAWEZA,SERIKALI IWAANGALIE KWA UKARIBU WANAWAKE ILI WAWEZE KUPATA MIKOPO.

Kamanga na Matukio | 05:53 | 0 comments

 Mkazi wa Jijini Mbeya akitembeza viazi katika mtaa wa Uhindini,akitafuta wateja watakao nunua kwa lengo la kupata kipato kitakacho muwezesha kujikimu na maisha ya familia yake.
Mfanyabiashara wa vitunguu akiwa katika eneo lake la biashara stendi ya  daladala Kabwe Jijini Mbeya, na fungu moja la vitunguu huliuza kati ya shilingi 500 hadi 1000.Serikali iwaangalie wakina mama kama hawa ili kuweza kupata mikopo midogomidogo itakayowawezesha kuendesha biashara zao.
Mkazi wa Meta Jijini Mbeya akianika ulezi kando kando ya ukuta wa Shule ya Sekondari Meta, ulezi huo unatumika kwa ajili ya kutengenezea pombe za kienyeji (picha na mdau wetu Godfrey Kahango).

CHIFU MERERE II WA KABILA LA WASANGU ANUSURIKA KUZIKWA AKIWA HAI - MBEYA.

Kamanga na Matukio | 05:52 | 0 comments

Chifu Merere II wa kabila la wasangu.
******
 Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Chifu Merere II (70) wa kabila la wasangu,amenusurika kuzikwa akiwa hai baada ya kutokea tafrani katika msiba wa kijana aliyefahamika kwa jina moja la Frank,katika Kijiji cha Ijumbi,Kata ya Ruiwa,Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya.

Tukio hilo limefuatia baada ya chifu huyo akishirikiana na ndugu kukubali kwenda kupiga ramli ya ugonjwa wa kijana huyo baada ya kifo kwa Mganga wa kienyeji aishie Wilaya ya Mbozi,ambaye jina lake hakutajwa na mganga huyo kuagiza kuchinjwa ng'ombe mmoja na kupikwa pombe katika pipa lenye ujazo wa debe 12.

Kufuatia agizo hilo marehemu aliuza sehemu ya uwanja aliokuwa anaumiliki kwa zaidi ya shilingi 450,000 na Chifu Merere II kukabidhiwa pesa hizo kwa ajili ya tambiko.

Aidha baada ya makabidhiano hayo ng'ombe alichinjwa,pombe kupikwa na kuitwa baadhi ya wanandugu mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka huu na kwamba baada ya tambiko marehemu atapona.Mganga huyo alidai waliomroga marehemu huyo ni ndugu wa karibu na majirani licha ya kutoweka wazi majina yao.

Sakata la Chifu Merere II kutaka kuzikwa akiwa hai limekuja baada ya marehemu Frank kufariki Julai 10 mwaka huu na vijana wa kijiji cha Ijumbi kutaka maelezo kwanini marehemu amefariki kutokana na sadaka kutolewa huku marehemu akiuza kila kitu alichokuwa nacho.

Aidha haikuishia hapo vijana hao waligoma kuchimba kaburi na kumtaka Chifu huyo atoe maelezo ya kwanini marehemu amefariki lasivyo arudishe pesa vinginevyo atazikwa akiwa hai ili iwefundisho.

Naye,Afisa Mtendaji wa Kata Bwana Jordan Masweve,alipopata taarifa hizo alienda nyumbani kwa Chifu na kukuta vijana wamemzonga wakimdai pesa zilizotumika katika tambiko.

Hata hivyo Chifu Merere II alikuwa hana la kujibu,ndipo Afisa mtendaji huyo alimchukua na kwenda kumfungia mahabusu na yeye kwenda msibani na kuitisha mkutano wa hadhara,ambapo aliwaomba wananchi wakachimbe kaburi huku yeye akiahidi kumfuatilia Chifu huyo ili arejeshe pesa hizo.

Pamoja na vijana hao kukubali kuzika majira ya saa 8 mchana,hali ilizidi kuwa tete ndipo Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Diwani Athuman alituma askari kijijini hapo kwa ajili ya kuimarisha amani na kumwokoa Chifu huyo baada ya mazungumzo marefu na baadhi ya pesa shilingi 350,000 kurejeshewa aliyenunua uwanja.

Wakati kiasi kilichobaki Diwani wa kata hiyo Mheshimiwa Alex Mdimilage amesema watafanya utaratibu wa kuzirudisha katika familia ya ndugu wa marehemu,na chifu Merere II kuachiwa majira ya saa 12 jioni na amani kurejea kijijini hapo.

Siku chache zilizopita mwanamke mmoja wa Kijiji cha Malamba,Kata hiyo Bi Rozina Mwadala(60),aliyezikwa akiwa hai Juni 2 mwaka huu baada ya kutuhumiwa kujihusisha na imani za kishirikina baada ya Mganga wa kienyeji huyo huyo kutoka Wilaya ya Mbozi kupiga ramli kwa madai kuwa marehemu aliyezikwa hai ndiye aliyesababisha kifo cha mkazi mwingine wa kijiji hicho marehemu Frank Lingo(25),aliyefariki Juni Mosi mwaka huu kwa maumivu kwenye sikio na jicho.

SAKATA LA MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI KUFUMANIWA NA MKE WA MTU.

Kamanga na Matukio | 04:31 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Mwimbaji wa nyimbo za Injli mkoani Mbeya Bwana Yona Mwaisango amekanusha kufumaniwa akiwa na mke wa mtu katika mtaa wa Ilolo Kati,Jijini Mbeya Julai 2 mwaka huu majira ya saa 2:30 usiku.

Mwimbaji huyo amesema hiyo ilikuwa ni mbinu tu zilizopangwa ili kumchafua yeye kwani alifika nyumbani hapo(inapodaiwa alifumaniwa) kwa lengo la kumsaidia hudumua ya chakula  na mpango wa kuwaelimisha ili waweze kukopa katika Shirika la mikopo la PRIDE .

Ameongeza kuwa alidaiwa pesa za ugoni shilingi laki tano na kuziahidi kulipa Julai 3 mwaka huu ambapo alitoa jumla ya shilingi 250,000 na kuahidi kiasi kilichobaki atakilipa Julai 7 mwaka huu.

Mwimbaji huyo amekiri kusaini barua ya kulipa faini hiyo na kwamba alifanya hivyo ili kuepuka kudhurika kutokana na kutishiwa usalama wake kutoka kwa wananchi wenye hasira kali na kwamba kwa sasa hayupo tayari kuzilipa pesa hizo kwani hakutenda kitendo hicho cha ugoni na cha aibu.

Aidha kikao hicho kilifanyika katika nyumbani hiyo(inayodaiwa alifumaniwa humo) kilichochukua muda wa masaa mawili kabla ya kuruhusiwa kutoka.

Hata hivyo,wimbi la watumishi wakubwa na kashfa ya ugoni na ubakaji zimezidi kuwaandama waimbaji mkoani hapa ,ambapo hivi karibuni Uncle Machibula alidaiwa kumbaka mwanafunzi wa Kidato cha Pili na kushikiliwa kwa siku kadhaa na kisha kuachiwa huru na Jeshi la polisi mkoani hapa.

WAZIRAI KWA SIKU TATU BAADA YA MGANGA WA JADI KUWANYWESHA DAWA YA KIENYEJI.

Kamanga na Matukio | 04:30 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga.
Wanawake watatu wa familia moja wamezirai baada ya kunyweshwa dawa na Mganga wa Kienyeji walikokwenda kuagua katika Kitongoji cha Mikocheni,Kijiji cha Namambo,Kata ya Totowe,Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.

Tukio hilo limetokea Julai Mosi mwaka huu,ambapo wanawake hao walikwenda kwa Mganga wa kienyeji Bwana Lushinga kwa lengo la kuagua wakitaka kufahamu kwanini mama yao mwenye umri wa miaka 75 haoni na anasumbuliwa na ugonjwa wa macho kwa muda mrefu.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Namambo Bwana Zacharia Mwandanji,amethibitisha tukio hilo na kuwataja wanawake hao kuwa ni pamoja na Bi.Emaculate Gibson,Tatu Gibson na Nampomwa.

Baada ya kunywesha dawa na mganga huyo wanawake hao walizirai mara moja na kuzinduka baada ya siku tatu Julai 3 mwaka huu,majira ya saa saba mchana huku wakiwa hoi kwa uchovu.

Aidha,imani za kishirikiana zimekuwa chanzo cha mauaji mengi mkoani hapa,tabia ambayo imelaaniwa vikali na asasi mbalimbali zikiwemo za Muungano wa Jamii Tanzania(MJATA) na Jeshi la Polisi kupitia ulinzi shirikishi.

Hata hivyo wananchi wametakiwa kujiepusha na waganga wanaosababisha uvunjifu wa amani katika jamii.

CHEKA, WOLPER WAAHIDI KUWATWANGA WAPINZANI WAO KWENYE TAMASHA LA MATUMAINI...!!!

Kamanga na Matukio | 04:29 | 0 comments
Bondia Francis Cheka (katikati) akitamba mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuwa atamchakaza mpinzani wake Japhet Kaseba.
Wolper (kulia) akijitapa kuwa atamtwanga mpinzani wake mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani).
Nahodha wa Bongo Fleva, H Baba (kulia) akiahidi ushindi kwa timu yake dhidi ya Bongo Movie.
waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini

Kwa hisani ya Fununu Habari.

SOKO LA SIDO MWANJELWA LAFUNGWA BAADA YA KIBANDA KIMOJA CHA MAMA NTILIE KUNUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO. MAMA NTILIE MBIONI KUFUNGULIWA MASHTAKA - MBEYA.

Kamanga na Matukio | 05:39 | 0 comments
Sehemu ya Soko la Sido Mwanjelwa lililoteketea kwa moto Jijini Mbeya,mnamo Septemba 16 mwaka jana na kusababisha hasara kubwa kwa wafanyabiashara wa soko hilo.
*****
Na  Venance Matinya, Mbeya.
Halmashauri ya Jiji la Mbeya inatarajia kuwafikisha mahakamani wafanyabiashara wa soko la Sido Mwanjelwa kutokana na kuhusishwa na vyanzo vya moto katika soko hilo mara kwa mara.
 
Baadhi ya wafanyabiashara hao ni wale wanaoshughulika na huduma za kupika na kuuza vyakula ndani ya soko hilo ambapo imedaiwa kuwepo na makubaliano kati ya viongozi na wafanyabiashara wa soko kutoruhusiwa kuwasha mkaa,sigala au moto na kutopika kitu chochote sokoni hapo.
 
Uongozi wa Jiji umesema watuhumiwa hao wamekiuka makubaliano na sheria ndogo ndogo zinazohusu soko hilo ambazo ni kifungu cha 12(1) cha mwaka 2011 ambacho kinakataza kujihusisha au kuwasha moto ndani ya soko hilo ili kuepuka majanga hayo.
 
Makamu Mwenyekiti wa soko la sido Bwana Wilson  Mwakisilwa alisema majanga hayo yamekuwa yakiliandama soko hilo tangu mwaka juzi ambapo wafanyabiashara wengi walipoteza mali zao na kusababisha waendelee kudaiwa kutoka katika taasisi za fedha.
 
Alisema hali hiyo inatosha na ndiyo sababu wameamua kuwafikisha mahakamani wale wote ambao wanakiuka makubaliano na kuendelea kusababisha hali ya hatari katika masoko na kusababisha wananchi kushindwa kufanya biashara zao kwa uhuru.
 
Mwakisilwa alisema wamefikia uamuzi huo baada ya juzi baadhi ya mama ntilie kuwasha moto na kusababisha kubanda kimoja kunusurika kuungua hali iliyosababisha taflani kubwa sokoni hapo na kuleta malumbano kati ya uongozi wa soko na wafanyabiashara.
 
“ Juzi jioni mama mmoja alikuwa akipika ndani ya kibanda na kusababisha moto kuwaka ingawa tulifanikiwa kuuzima lakini hawa akina mama  hawakuwa na lugha nzuri kwetu sisi na kusababisha tukose maelewano hali iliyotulazimu kwenda kwenye vyombo vya dola na hapa tumewakamata watu 9 waliohusika na hali hiyo” alisema Makamu Mwenyekiti huyo.
 
Aidha makamu mwenyekiti huyo aliwataja watu hao watakaofikishwa mahakamani kuwa ni Halima Benard, Lukia Kayuni, Maria Mwakamela,Elizabeth Sikwesi, Agnes Dominick, Rehema Musa, Beth Aron, Agatha Hussein na mwingine aliyejulikana kwa jina moja la Skauti.
 
Kwa upande wake baadhi ya wafanyabiashara wa soko hilo Michael Ashibaye na Lucia Silingwa waliwalalamikia mama ntilie kwa kutokuwa na uchungu wa mali wanazounguliwa hivyo kufikia hatua za kukaidi maagizo wanayokubaliana nayo.
 
Kamanda wa polisi wa wilaya ya Mbeya (OCD) Abraham Silvester alisema Uongozi wa Jiji wako tayari kuandaa hati ya mashtaka tayari kuwafikisha mahakamani watuhumiwa hao ambapo aliongeza kuwa watuhumiwa wote wanashikiriwa katika kituo cha kati cha polisi.

KAMPUNI ya simu za mkononi Zanzíbar ZANTEL kudhamini tuzo za wanamuziki bora Zanzibar

Kamanga na Matukio | 05:37 | 0 comments
Na Ali Issa   Maelezo Zanzíbar    
                                                        
KAMPUNI ya simu za mkononi Zanzíbar ZANTEL imeahidi udhamini wa Shl. milioni 32 pesa taslimu kwa Kampuni ya Zanzibar Medium Corporación  kwa ajili ya tunzo ya wana muziki bora wa Zanzíbar mwaka 2012.

Udhamini huo umetangazwa leo na Mkurugenzi wa Biashara Zantel upande wa Zanzibar Mohammed Mussa wakati akizungumza na wandishi wa habarí katika ukumbi wa Idara ya Habarí Maelezo mjini Zanzíbar.

Amesema pesa hizo zimetolewa kwa ajili ya kudhamini tunzo hiyo ikiwa ni njia moja wapo ya kuthamini na kuheshimu mchango ambao wanamuziki wa Zanzíbar wamekuwa wakiutoa ikiwa ni pamoja na kuielimisha na kuiburudisha jamii. 

Ameongeza kuwa Kampuni ya kizalendo ya Zantel imekuwa ikitoa huduma zake na kujenga mapenzi ya dhati kwa jamii ikiwemo kujenga visima vya maji sita ili kuhakikisha faida inayopatikana inaifaidisha jamii kwa ujumla

Mkurugenzi huyo alisema pesa hizo zitatolewa kwa kuzingatia misingi imara na kuepuka upendeleo na kwamba Zanzitel itaendelea kuwa karibú na jamii kwa kutoa ushirikiano pale ambapo itahitajika.

Kwa upande wake Meneja Masoko kutoka Kampuni ya Zanzibar Medium Corporación ambao ndio waandaaji wa tunzo hiyo Said Khamis aliishukuru kampuni ya Zantel kwa kudhamini tunzo hizo na kuiomba indelee kuwa karibú na jamii pale ambapo watahitajika kutoa msaada wao.

Aidha amefahamisha kuwa tunzo hizo ambazo zitatolewa zitakuwa zimegawika katika makundi 16  ya aina mbali mbali za wasanii ikiwemo makundi ya muziki wa kizazi kipya (Zenji Fleva) na Taarab asilia.

Tamasha hilo la saba litafanyika Bwawani siku ya Ijumaa,Juni 6 mwaka huu ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamo wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa  Tanzania Dk.Mohammed Gharib Bilali .

MJANE AFUMANIWA AKILA URODA NA MUME WA MTU UPENUNI

Kamanga na Matukio | 05:20 | 0 comments

*APINGWA MAPANGA NA KUVUNJWA MGUU.
*MUME NA MKE WATOROKA.
Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Mkazi wa Mtaa wa Ilembo,Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya Bi.Zainab Mapumba(40),ambaye ni mjane amejeruhiwa kwa kukatwa katwa na mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake ukiwemo mguu wa kushoto uliovunjwa na kichwa kuchalangwachalangwa.

Tukio hilo limetokea katika Mtaa wa Ilolo,ambapo inadaiwa kuwa mwanamke huyo mwenye watoto watano alikuwa na Bwana Juma Senka katika eneo la Grocery moja wilayani humo na mara baada ya kunywa pombe Bi. Mapumba alisindikiza Bwana Senka nyumbani kwake na walipofika upenuni mwa nyumba yake wote wawili walivua nguo na kuanza kufanya tendo la ndoa.

Mke wa Bwana Senka aliposikia kelele na kishindo alitoka nje akiwa na panga na kuwakuta watuhumiwa hao wakifanya mapenzi na kuamua kumwita mwanawe na kisha kuanza kumshambulia mjane huyo na kumjeruhi vibaya kichwani na pia kumvunja miguu.

Baada ya mkasa huo Bwana Senka alitoroka kusikojulikana kuepuka adha ya aibu na mkewe naye kutoroka kukwepa mkono wa sheria huku wasamaria wema wakimkimbiza Bi Mapumba katika Hospitali ya wilaya hiyo.

Aidha Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Bwana Nico Mbilinyi amesema kuwa mjane huyo alifikishwa hospitalini hapo Julai 2 mwaka huu majira ya usiku na kwamba hali yake inaendelea vema. 

Hata hivyo baadhi ya mashuhuda wamedai kuwa Mjane huyo alionywa mara kadhaa kuwa nakutokuwa na mahusiano na Bwana Senka,ambapo mkewe alikosa uvumilivu hivyo kupelekea kuanza kujichukulia sheria mkononi.

HAKIMU ALIYETUHUMIWA KWA RUSHWA AACHIWA HURU

Kamanga na Matukio | 04:47 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Mbeya,umemwachia huru aliyekuwa Hakimu mkazi wa mahakama ya Mkoa wa Mbeya Amani Mwihomeke(30),aliyekuwa anakabiliwa na tuhuma za rushwa.

Hakimu huyo anakabiliwa na makosa mawili kinyume cha sheria kifungu cha 15 cha kanuni ya adhabu kifungu kidogo(i) cha 11/2007 ambapo alidaiwa kushawishi na kupokea rushwa ya shilingi 150,000 mnamo Mei 29 mwaka huu.

Mwendesha mashtaka wa Serikali kutoka kikosi cha kupambana na kuzuia rushwa nchini TAKUKURU,Kanda ya Mbeya Bwana Nimrod Mafwele akisaidiwa na Sarah Martin walidai Mahakamani kuwa Amani Mwihomeke alishawishi na kupokea rushwa hiyo katika Bar ya Bonanza iliyoko barabara ya Benki Kuu Jijini Mbeya.

Hakimu mfawidhi wa wilaya ya hiyo a Seif M. Kulita amesema mtuhumiwa anaachiwa huru kutokana na upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha tuhuma hizo hivyo mahakama kuchukua uamuzi huo wa hukumu ambayo ilichukua masaa matatu kusomwa katika mahakama hiyo.

Hakimu Mwihomeke alikuwa anatetewa wakili wa kujitegemea Mika Thadayo Mbise.

Hata hivyo Hakimu mfawidhi Kulita alitaka waeshesha mashtaka kuandaa vema mashtaka ambapo wameshindwa kuthibitisha tuhuma ambazo zingemtia mtuhumiwa hat

WATU WATATU WAFARIKI KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI WILAYA ZA CHUNYA NA MBARALI.

Kamanga na Matukio | 05:30 | 0 comments
Wanawake wawili wamefariki kwa kujinyonga katika Wilaya ya Mbarali na Chunya,matukio yote haya yametokea jana yakihusisha wanawake wenye umri wa zaidi ya miaka 60.

Aidha mwili wa marehemu katika Wilaya ya Chunya amezikwa jana baada ya jeshi la polisi kufika na kuthibitisha kifo hicho nawa wilaya ya Mbarli mwili wake ulikuwa ukiendelea kuning’inia na unatarajia kuzikwa leo.

Wakati huo huo mtu mmoja ameuwa baada ya kutokea mapigano katika mgodi wa dhahabu wilayani Chunya na Jeshi la polisi lilikuwa linaelekea eneo la tukio usiku wa jana..

 *****Kwa habari zaidi endelea kufuatilia mtandao huu******

BREAKING NEWSSS:- MWIMBAJI MAARUFU WA NYIMBO ZA INJILI AFUMANIWA NA AKUBALI KULIPA FIDIA YA SHILINGI 500,000/=.

Kamanga na Matukio | 05:28 | 0 comments
Mwimbaji maarufu wa Nyimbo za Injili Mkoani Mbeya(jina tunalihifadhi),ambaye pia ni mwalimu wa kwaya moja jijini Mbeya, amefumaniwa katika Mtaa wa Ilolo Kati akiwa na mke wa mtu majira ya saa 3 usiku.

Mwimbaji huyo ambaye pia hujihusisha na huduma kwa watoto yatima,amejikuta akinaswa na mume wa mwanamke huyo aliyekuwa naye na kuokolewa na wasamalia wema,ambapo mwimbaji huyo baada ya majadiliano ya masaa matatu alikubali kulipa fidia ya ugoni ya shilingi 500,000.

Aidha mwimbaji huyo amekiri kutenda kosa hilo na kuahidi leo kulipa shilingi 250,000 na kiasi kilichobaki akidai atamalizia Julai 8 mwaka huu.

Ameongeza kwa kuomba kuhifadhiwa kwa lengo la siri kutovuja na kudai kuwa atakuwa mwaminifu katika ulipaji wa deni na kuondoka baada ya kuacha maandishi na kuweka sahihi mbele ya mwenyekiti aliyejihudhuru hivi karibuni wa mtaa huo wa Ilolo Kati..


*****Kwa habari zaidi endelea kufuatilia mtandao huu******

WAKULIMA WAKIUKA AGIZO LA SERIKALI YA MKOA WA MBEYA JUU YA UUZAJI WA KAHAWA MBICHI.

Kamanga na Matukio | 01:41 | 0 comments
Habari na Gabriel Mbwille,Mbozi.
Wakulima wa zao la kahawa wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya,wamesema biashara ya uuzaji wa kahawa Mbichi imekuwa ikiendelea kufanyika licha ya Serikali ya mkoa kupipiga marufuku biashara hiyo kutokana na baadhi ya watendaji wa Serikali kujihusisha na ununuzi wa kahawa hiyo.


Wakiongea na mwandishi wetu kwa nyakati tofauti wa kulima wa zao hilo katika kata ya Mlangali wilayani humo wamesema mtandao wa biashara ya kahawa mbichi (CHERY) umekuwa ukifanywa na watendaji wa Serikali kupitia mawakala ndiyo maana wameshindwa kuwadhibiti.

Aidha mmoja wa wakulima hao Batholomeo Mwayela wamesema mkulima anayeuza kahawa mbichi hupata hasara zaidi ya mara tatu ukilinganisha na bei ya kahawa inayokobolewa.

Kwa upande wake afisa kilimo wa kijiji cha Lukululu kata ya Mlangali Bi.Miriam Philipo amewataka wakulima kuwa na tabia ya kuweka akiba ya fedha ili ziweze kuwasaidia katika msimu wa mavuno.

Wakati huohuo amesema wakulima waekuwa wakipata hasara kubwa kupitia biashara hiyo na Serikali imeombwa kusimamia soko la zao la kahawa ili kuwezesha kuwepo kwa bei itakayomnufaisha mkulima kutokana na kutokuwepo kwa bei maalumu katika msimu wa mavuno wa zao hilo.
 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger