Pages


TAMAA:- ADUNDWA MAKABURINI BAADA YA KUTAFUNA PESA ZA JENEZA

Kamanga na Matukio | 05:11 | 0 comments
**Marehemu azikwa bila jeneza.
**Fundi aliyepewa pesa atorokea Mbeya.
**Watumishi wa Mungu washuhudia kichapo.
Habari na Ezekiel Kamanga.,
Bwana Marco Sikalunga Mkazi wa Kijiji cha Chilangawana,Sumbawanga Vijijini mpakani na Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya amenusurika kufikwa na mauti paacha ya kupokea kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali,baada ya kupewa jukumu la kuchangisha fedha shilingi 50,000 kwa ajili ya kuchonga jeneza.

Bwana Sikalunga alidai kuwa fedha hizo zilizochangishwa alimkabidhi fundi anayefahamika kwa jina la Senga na kwamba utakapofika muda wa saa za kuzika ataleta jeneza hilo.

Lakini katika mshangao mnamo Septemba 13 mwaka huu ulitokea msiba kijijini hapo,ambapo alifariki Suzana Upepo,na kijana huyo alipotakiwa kupeleka jeneza alidai anaenda kuchukua kwa fundi na alipofika nyumbani kwa fundi huyo hakufanikiwa kumkuta.

Kufuatia sakata hilo wananchi waliamua kuuchukua mwili wa marehemu na kwenda kuuzika bila jeneza,wakiwa njiani wananchi hao wakiwa na hasira kali walimpiga Bwana Sikalunga mbele ya Mchungaji Ladislaus Kamanga na Gidion .A. Simponda(Mwandete).
Hata hivyo Bwana Senga ambaye ni fundi aliyepewa jukumu la kutengeneza jeneza hilo anadaiwa kutorokea Mkoani Mbeya na kiasi hicho cha fedha cha shilingi 50,000.
Wakati huo huo wananchi hao wanatarajia kumchukulia hatua za kisheria Bwana Sikalunga.

MWENYEKITI WA KIJIJI AKATA MITI YA SHULE BILA RIDHAA YA KAMATI

Kamanga na Matukio | 05:06 | 0 comments
*Kamati yacharuka yamtaka alipe fidia.
*Vijana watishia kikao cha ndani.
*Diwani akanusha kumbeba mwenyekiti.

Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Motomoto Bwana Kassimu Mwagala,amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuitwa na Kamati ya Shule ya msingi Motomoto alipotakiwa kutolea maelezo suala la kukata miti saba ya shule hiyo kutokana na shinikizo la vijana kutaka kuongeza uwanja wa shule pasipo ridhaa ya kamati hiyo.

Akiongea kwa masikitiko Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bi Lydia Mdoe,amesema kitendo hicho kilichofanywa na mwenyekiti huyo nicha dharau,hivyo kuwafanya waishi kwa hofu shuleni hapo licha ya dhamana waliyopewa na Serikali ya kulinda mali za shule na mazingira yetu.

Aidha Mwenyekiti wa Kamati ya shule hiyo Bwana Yusuph Tosha amesema ukataji wa miti hiyo uliofnya na Mwenyekiti wa kijiji ni kuifanya kamati yake kuonekana haifanyi kazi na ni kuingilia majukumu.

Hali hiyo ilizua taflani katika kikao ambapo Bwana Mwagala kwa kujihami aliandamana na kundi la vijana,ambao walifanya fujo katika mkutano na baadae Diwani wa Kata ya Ruiwa mheshimiwa Alex Mdimilage aliagiza kuwa vijana wote waitwe Ofisi ya kata watoe maelezo ni kwani walivamia mkutano usiowaruhusu.

Hata hivyo kutokana na kukera na kitendo cha Mwenyekiti wa kamati hiyo ilimtaka kulipa jumla ya shilingi 210,000 ili iwe onyo kwake,ambapo ametakiwa kuomba radhi,kamati hiyona kutakiwa kuzilipia kabla ya Oktoba 12 mwaha huu.

MWANAMKE AISHI NA WANAUME WAWILI KWA WAKATI MMOJA.

Kamanga na Matukio | 05:05 | 0 comments
Habari na Ezekiel,Kamanga.
Mwanamke mmoja Vi Matrida Charles(42) Mkazi wa Kitongoji cha Motomoto B,Kijiji cha Motomoto,Kata ya Ruiwa,Welaya ya Mbarali Mkoani Mbeya,anaishi na wanaume wawili kwa wakati mmoja kwa takribani siku nne mpaka hivi sasa.

Tukio hilo la aina yake lililofanywa na mwanamke huyo baada ya kutelekezwa na mumewe wa awali Bwana George Mwasomola anayetoka Kijiji cha Mahango,ambaye ameishi naye kwa mika 25 kabla ya kumtelekeza miaka saba iliyopita naye kukimbilia Mkoani Morogoro na kurejea Septemba 8 mwaka huu.

Baada ya kurejea alimkuta mkewe Matrida akiishi na mwanamke mwingine aitwaye Idd Msongole(50),miaka saba iliyopita katika nyumba ambayo mwanamke huyo alijengewa na mwanae ambaye baba yake alifariki kabla ya kuolewa na mwanamme wake wa sasa anayeishi naye.

Septemba 9 mwaka huu Bwana Mwasomola alimwita mkewe huyo wa zamani nyumbani kwao Kijiji cha Mahango,ndipo mwanamke huyo akamjibu kuwa aje kijijini kwao Motomoto na kumtaka mumewe wa saa Bwana Msongole aondoke hapo nyumbani na alitakiwa kuishi kwa Balozi wa Shina Bwana Mussa Haonga,huku kila mmoja akipata huduma ya chakula,maji ya kuoga na kila mmoja kutembelewa kwa nyakati tofauti.

Baada ya kuona vitimbi hivyo viongozi wa Kitongoji cha Motomoto B ukiongozwa na Mwenyekiti wake Bwana Andrea Mwambije,aliamua kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kijiji Bwana Kassim Mwagala ambaye naye alimtaarifu Afisa Mtendaji wa Kijiji Hussein Mwantanji na baadae Bi Matrida kuulizwa kuwa yupi ni mume wake halali ambapo alijibu kuwa ni Bwana Idd Msongole,ingawa ndiye aliyetolewa nyumbani hapo nakwenda kuishi kwa balozi akimwacha bwana Mwasomola akijivinjari na kuzua gumzo kijijini.

Hata hivyo uongozi wa kijiji umekuwa na wakati mgumu endapo mmoja kati ya wanaume hao atakapo taharuki hivyo umetoa taarifa katika Ofisi za Kata na Kituo cha Jeshi la Polisi Igurusi ili kuchukua tahadhari.

Aidha katika uchunguzi umebaini kuwa Bwana Idd Msongole ambaye anaishi kwa Balozi kwa sasa yupo tayari kusubiri hata mwezi mmoja ili Bi Matrida amalizane na Bwana Mwasomola kuweka saini katika ofisi ya kijiji kuhakikisha usalama wa wanaume hao,licha ya mwanamke huyo kukiri wazi kuwa kwa sasa anependa kuishi na mumewe wa sasa Msongole kwa kuwa mume wake wazamani Bwana Mwasomola alimtelekeza miaka saba iliyopita.

Habari za ndani zinadai kuwa katika sakata hilo uongozi ulimtoza adhabu ya shilingi 100,000 mwanamke huyo,ambapo alilipa shilingi 90,000 na mumewe wa zamani alitozwa shilingi 50,000 na kutakiwa aondoke mara moja.

Wakati hayo yakijiri Bwana Msongole kila asubuhi alikuwa akifika nyumbani kwa mwanamke huyo akitokea kwa Balozi na kuichukua mifugo kwenda nayo machungoni na kurejea majira ya jioni na baadae kuelekea kulala kwa balozi huku Bwana Mwasomola alikuwa akielekea Mahango kwa ajili ya biashara.

****Hatima ya kitendawili hiki kitateguliwa na Matrida mwenyewe endelea kufuatilia mtandao huu******.  

NEW TRACK:- TENZI ZA DUNIA - SAMICHO ft JAY P and ISS MATERIAL

Kamanga na Matukio | 05:04 | 0 comments
Sikiliza na download ngoma hii yenye mashairi yaliyo na utunzi wa aina yake? Ki ukweli ni wasanii wachache katika Bongo HipHop ambao huandika mashairi yenye Ujumbe uliobeba uhalisia wa jambo fulani katika Jamii inaayotuzunguka kwa kila mmoja wapo katika maisha ambapo hits zao huelimisha na vilevile huelimisha kutokana na uelewa na umakinifu wao katika ufasini wa kazi husika.
Ngoma inafahamika kwa Jina la TENZI ZA DUNIA ikiwa ni utunzi na rap ya Msanii SAMICHO akiwashirikisha JAY P na ISS MATERIAL,tushirikiane kwa pamoja katika kusapoti muziki wa Bongofleva ili uweze kufikia maalengo ya kuuza katika nyanja za kimataifa. 
Phone no* +255713251540
Artist:- Samicho ft Jay P & Iss Material Song Name:- Tenzi za Dunia Phone no* +255713251540

WASUSIA KUZIKA MAITI KWA SIKU MBILI,MFIWA ATAKIWA KULIPA SHILINGI 460,000/= ILI APEWE MSAADA..

Kamanga na Matukio | 05:34 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga,Mbozi.
Wananchi wa Kitongoji cha Njiapanda,Kijiji cha Msamba,Kata ya Nyimbili,Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya,walisusa kuzika maiti kwa takribani siku mbili na nusu kwa kile kilichodaiwa kuwa mfiwa alikuwa hahudhurii misiba wenzie kijijini hapo.

Hayo yalibainishwa na mwandishi wa habari hii baada ya kufika kijijini hapo,ambapo imedaiwa Bwana Samson Mwazembe(35),ambaye alifiwa na mwanae aitwaye Hassan Samson(7) mwanafunzi wa darasa la kwanza Shule ya Msingi Chizumbi wilayani humo,aliyefariki siku ya Ijumaa Septemba 7 mwaka huu majira ya saa 10 alfajiri.

Mtoto huyo anadaiwa kufariki baada ya kuugua ugonjwa wa kuharisha kwa muda wa siku tatu lakini hakufanikiwa kupelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

Baada ya kifo hicho,kutokana na kasumba ya Bwana Mwazembe kutohudhuria katika misiba kijiji hapo,aliamua kwenda kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha wilaya hiyo ili kuomba msaada wa kusaidiwa kuzika mwanae,lakini polisi walikataa na kumtaka arudi kijijini ili azungumze na wananchi.

Kufuatia juhudi zake kugonga ukuta,aliamua kujifungia ndani ya nyumba yake na ndipo mkewe aitwaye Bi.Daina Kananda(25),aliamua kwenda kumuona Mwenyekiti wa kitongoji Bwana Eston Silomba ambapo alikwenda kwa Mwenyekiti wa Kijiji Bwana Ikson Halihoka Sikaponda(48) kwa pamoja walimtaka mfiwa azike mwenyewe kutokana na tabia yake ya kutohudhuria misibani.

Aidha,baada ya agizo hilo Bwana Mwazembe wakati akielekea tena katika Kituo cha Polisi alikutana na kaka njia aitwaye Bwana Adam Mwazembe(55),na alimwambia warudi kijijini na kuchukua jukumu la kuomba msamaha kwa uongozi wa kijiji ili wamsamehe mdogo wake huyo,viongozi walikataa ombi hilo na kumtaka mfiwa alipe jumla ya shilingi 460,000 ikiwa shilingi 400,000 kwa ajili ya kuchimba kaburi na shilingi 60,000 ya jeneza la kumhifadhia marehemu.

Hata hivyo mfiwa alikataa kulipa akidai kuwa hana fedha zozote ndipo maiti ikabaki bila kuzikwa na asubuhi ya Jumamosi Septemba 8 mwaka huu,Bwana Mwazembe alifanikiwa kupata shilingi 110,000 nakuomba uongozi upokee fedha hizo lakini bado walikataa na kumweleza kuwa akachimbe kaburi mwenyewe na kukabidhiwa vifaa vya kuchimbia lakini alishindwa na kubaki akiangua kilio.

Septemba 9,mwaka huu siku ya Jumapili ndugu wa Bwana Mwazembe kwa pamoja walimueleza auze mifugo wakiwemo mbuzi,nguruwe vilevile mazao(mahindi) baada ya kuuza jumla ya shilingi 400,000 zilipatikana lakini wananchi waliendelea kuwa na msimamo wakitaka zitimie shilingi 460,000,ndipo Mwandishi wa habari hii alipowasihi wananchi wakubali kupokea pesa hizo walikubali na kufanya mazishi majira ya saa 8 mchana.

Uchunguzi umebaini kuwa mfiwa anatuhumiwa kujihusisha na imani za kishirikina kwani mkewe alishawahi kujifungua watoto wawili na baadae kufariki kwa nyakati tofauti na yeye kuwazika pasipo kutoa taarifa kijijini na baadhi ya viungo kuvichukua na kuvipeleka kusikojulikana.

Wakati huohuo Bwana Mwazembe,amedai sababu za kutohudhuria katika misiba ni kutokana na kusisikia utofauti awapo msibani na ndiyo sababu ambayo hupelekea kutohudhuria.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji Bwana Sikaponda amesema kuwa hilo ni fundisho kwa mfiwa huyo na kwamba asirudie tena kitendo hicho na kwamba kijiji hakitatoa msamaha tena bali watamtaka kuondoka kijijini hapo kutokana na kutokuwa na ushirikiano.

Katika pesa zilizotolewa na mfiwa Bwana Mwazembe,shilingi 50 ilitumika kununulia vifaa vya kuchimbia kaburi kijijini hapo.

(Picha zaidi za tukio hili fuatilia mtandao huu)

Jaji Ihema, M/Kiti Kamati ya Kuchunguza Mauaji ya Mwangosi, Atoswa Kamati ya Vitalu Inayotuhumiwa kunuka Rushwa

Kamanga na Matukio | 05:33 | 0 comments

Iliwahi kuripotiwa kuwa Mkurugenzi wa Katiba na Haki za Binadamu wa Chadema, Tundu Lissu, aliipinga Tume iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt Emmanuel Nchimbi kuchunguza mauaji ya mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, marehemu Daudi Mwangosi.Moja ya sababu alizotoa Lissu ni Tume hiyo kuwa chini ya uenyekiti wa Jaji Mstaafu Stephen Ihema,ambaye alimtuhumu kuwa na rekodi ya utendaji kazi yenye walakini.

Katika pitapita yangu mtandaoni, nimekutana na habari inayomhusu Jaji Mstaafu Ihema, ambapo alikuwa mjumbe wa Kamati ya Ushauri wa Ugawaji Vitalu vya Uwindaji wa Kitalii, na sasa kamati hiyo imevunjwa kutokana na kulalamikiwa mno kwa vitendo vya rushwa miongoni mwa wajumbe.

Binafsi nimeguswa sana na habari hii hasa kwa vile inahusu tuhuma za rushwa kwa kamati iliyokuwa inamjumuisha Jaji Mstaafu Ihema.Sasa tukiamini kuwa Jaji Ihema ameshindwa jukumu la ujumbe tu kwenye tume hiyo ya ushauri,kwanini tumwamini kwenye uenyekiti wa kamati ya uchunguzi wa kifo cha marehemu Mwangosi?

Wakati ninawapongeza wanahabari waliojitokeza jana kuifahamisha bayana Serikali ya Rais Jakaya Kikwete  kuwa wanalaani vikali mauaji ya mwanahabari mwenzao yaliyofanywa na jeshi la polisi,ningependa kushauri kuwepo upinzani zaidi dhidi ya Tume hii ambayo kuna kila dalili kwamba itaishia kuwa kiini-macho tu.Awali,hofu yangu kuhusu Tume hiyo ilielemea zaidi Watanzania wameshashuhudia utitiri wa tume ambazo mara nyingi ripoti zake zimeishia kufungiwa maandazi na vitafunwa vingine badala ya kuwekwa hadharani//hatua kuchukuliwa.Wengi wetu tunakumbuka kuhusu tume ya milipuko ya mabomu huko Mbagala na Gongo la Mboto.Hadi leo hakuna kilichoelezwa kuhusu ripoti ya tume hiyo...and life goes on.

Je wewe ni mdau wa habari? Unapenda kuona uchunguzi wa kifo cha marehemu Mwangosi unafanywa independently na watu wasio na harufu ya utendaji kazi wenye walakini?Basi ungana na wanahabari kupiga kelele dhidi ya tume hiyo ya kisanii
 

DIWANI ATISHIWA KUUAWA

Kamanga na Matukio | 05:27 | 0 comments
Diwani wa Kata ya Myunga,Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya mheshimiwa Godfrey Siame kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)(kushoto),alipokuwa akimuonesha mpiga picha wetu moja ya kati ya makaburi saba yanayodaiwa kuwa waliozikwa waliuawa kwa imani za kishirikiana kisha kutolewa viungo vyao kama vile meno,sehemu za siri na Moyo pembezoni mwa Mto Momba.Hata hivyo zaidi ya watu watatu wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo hivyo hawajakamatwa licha ya kufahamika.
*******
Habari na Ezekiel Kamanga,Mbozi.
Diwani wa Kata ya Myunga,Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya Mheshimiwa Godfrey Siame,amedai kutishiwa kuuawa na wafanyabiashara watatu waliopo Wilaya Momba na Mbozi mkoani hapa.

Hayo yamethibitishwa na diwani huyo baada ya awali Majambazi wawili waliokodiwa kutoka Mkoani Morogoro kuuawa na wananchi wenye hasira kali,ambapo kabla ya mauti majambazi hao walikiri kwa maandishi na kuibua siri nzito kuwa wao wametumwa na Mfanyabiashara Benard Simundwe, Kasambilo Mteka na Yohana Simkonda wote wakazi wa Kijiji cha Myunga.

Aidha Diwani Siame amesema kuwa wananchi walifanikiwa kukamata silaha mbili aina ya Short Gun ambazo zilikuwa maalumu kwa ajili ya mauaji yake,simu mbili zenye SMS ya kutumiwa pesa kutoka kwa wafanyabiashara hao.

Hata hivyo vielelezo vyote hivyo vilikabidhiwa kwa Mkuu wa Kituo cha Jeshi la Polisi Mji mdogo wa Tunduma mkoani hapa Bwana Wendo na taarifa kutolewa kwa Mkuu wa kituo cha Polisi wilaya ya Mbozi Bwana Dudu,lakini cha kushangaza zaidi mpaka sasa watuhumiwa hao hawajakamatwa na kufikishwa mahakamani licha ya kuwepo kwa vielelezo hivyo.

Imedaiwa kufuatia tuhuma mbalimbali dhidi ya wafanyabiashara hao ambao pia wamedaiwa kujihusisha na mauaji ya kikatili kijijini hapo,Jeshi la polisi linawashikilia wananchi 14,ambao wanadaiwa kuibomoa na kuiteketeza kwa moto nyumba ya Mfanyabiashara Simundwe.

Wananchi waliokamatwa na kufikishwa mahakama ya Wilaya Mbozi kusomewa shtaka la kesi ya jinai ya wizi wa kutumia silaha na kupora mali ni Alick Siame, Hosea Sinsungwe, Amani Siame, Musa Siame, Laurent Simsokwe, Lighton Sichone, Sadock Simwanza.

Wengine ni Osphat Siame, John Simbeye, Jacob Mwakalibule, Paulo Sichona na katika kesi hiyo watoto wawili waliopo chini ya miaka 18 wamehusishwa katika sakata hilo ambao ni Damas Sinzumwi na Zebius Sinzumwi.

Watuhumiwa wote wamenyimwa dhamana,ambapo kesi yao imeahirishwa na Hakimu Mushi na itatajwa tena Septemba 24 mwaka huu na watuhumiwa wote wanatetewa na Wakili wa kujitegemea mheshimiwa Edgar Bantulaki.

Kwa upande wake mwendeshwa mashtaka wa Serikali anatarajia kurekebisha mashtaka baada ya kupata marekebisho kutoka kwa Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya Diwani Athumani ambapo jalada limewasilishwa kwake.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida simu mbili zilizokuwa na vielelezo zimekabidhiwa kwa ndugu wa marehemu waliouawa kitu ambacho kimewashangaza watetezi wa haki za binadamu akiwemo Mwenyekiti wa mkoa wa Mbeya Bwana Said Mwadudu,hali inayotia shaka hali ya utendaji kazi wa Polisi kituo cha Tunduma na Mbozi kwa kushirikiana na wahalifu.

Diwani Siame alitoa taarifa za kutishiwa kwake kuuawa,lakini amedai kusikitishwa na kitendo cha Polisi kushindwa kuwakamata watuhumiwa na hata Septemba 10 mwaka huu mfanyabishara Benard Simundwe alionekana mahakamani na baadae kuamuliwa na mmoja wa askari wa polisi alimuondoa eneo la tukio na mfanyabishara biasharaa huyo kuelekea kituo cha polisi Mbozi hali iliyowashangaza wananchi kwa polisi kudai hapatikani.

Vituo vya Polisi vya Tunduma,Mlowo na Mbozi vimedaiwa kuwakumbatia wahalifu na hivi sasa diwani huyo amekuwa akilindwa na wananchi.

KIFO CHA KUTATANISHA AKUTWA AMEKUFA AKIWA SHAMBANI.

Kamanga na Matukio | 01:06 | 0 comments


Habari na Ezekiel Kamanga,Rungwe na Chunya.
Mwananchi Mmoja Mkazi wa Kijiji cha Ipelo,Kata ya Kandete Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya, Mwalisu Kilole (67) amefariki dunia akiwa shambani kwake baada ya kmwili wake kuteketea kwa moto.

Tukio hilo limetokea Septemba 5 mwaka huu majira ya saa 1 usiku wakati marehemu huyo akiwa shambani kwake alipokwenda kulima.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bwana Yuda Mwasambogole,amesema kuwa alipata taarifa za kifo cha mtu huyo ambapo alipofuatilia alikuta mwili wa marehemu umeteketea kwa moto na mpaka sasa chanzo cha moto huo hakichaweza kufahamika.

Baada ya uchunguzi uliofanywa na madaktari,mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya maziko.

Wakati huohuo Mkazi wa Kijiji cha Ifuko Sifa Pascal Nyerenga amefariki dunia baada ya kutumbukia katika Mto Songwe,Wilaya ya Chunya Mkoani hapa wakati akiogelea.

Marehemu amesadikika kuwa kabla ya kifo chake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kifafa,ambapo mwili wake ulipatika majira ya tatu asubuhi Septemba 5 mwaka huu.

UMOJA WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA (UTPC) UMEITAKA SERIKALI KUWASIMAMISHA KAZI ASKARI WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO LA MAUAJI YA MWANDISHI DAUDI MWANGOSI.

Kamanga na Matukio | 01:04 | 0 comments
Habari na Ester Macha,Mbeya.
Kufuatia mauaji  ya mwandishi wa habari wa  kituo cha Channel Ten  Mkoani Iringa Bw. Daudi Mwangosi Umoja wa klabu za waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) umeitaka serikali kuwasimamisha kazi askari waliohusika katika tukio la mauaji ya kutisha ya mwandishi huyo.

Umoja huo umesema kuwa askari walioshiriki katika oparesheni  hiyo ambayo ni haramu wamesema serikali iwasimamishe kazi mara moja ili kupisha uchunguzi kufanyika.

Hayo yalisemwa jana  Jijini Dar Es Salaam na  Rais wa Umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania Bw.Keneth Simbaya wakati alipokuwa akitoa tamko  la mauaji  dhidi ya mwandishi wa habari aliyeuwawa akiwa mikononi mwa polisi katika kijiji cha Nyololo Wilayani Mufindi.

“Hapa tunataka uchunguzi  huu ukikamilika tunaitaka serikali  kuutangazia umma na kupisha sheria kwa wale watakaobainika  kuhusika kwa uzembe huo kwa namna moja au nyingine wachukuliwe hatua dhidi ya mauaji haya ya mwandishi wa habari Bw. Daudi Mwangosi”alisema.

Hata hivyo Bw. Simbaya alisema wakati uchunguzi ukiwa unaendelea  serikali iridhie  na kurasimisha  malipo  kwa ajili ya Mjane wa mwandishi huyo  na watoto walioachwa na marehemu ili waweze kujikimu.

Aidha alisema licha ya kutoa tamko hilo wanaendelea  kulitazamia jeshi la polisi  kama mdau  mwenye shaka namna wanavyotenda kazi  na waandishi wa habari  mikoani  na kwamba watataarifu umma kuhusu mwenendo wao hapo baadae.

“Lakini pia katika mkutano huu tumeridhia  kushirikiana na taasisi  zingine za haki za binadamu  ,uwakili na Utetezi ili kubaini  namna bora ya kuistaki serikali kama mwenendo wa suala hili  hautakuwa  unaleta tija hivyo tunakarisha mashirika  ya haki za binadamu ,asasi zisizokuwa za kiserikali ili kuweza kufanikisha azma hii”alisema Bw. Simbaya.

Akizungumzia kuhusu usalama kwa waandishi wa habari Bw. Simbaya alisema katika kuhakikisha kuwa waandishi wa habari wanafanya kazi yao kwa usalama amelitaka jeshi la polisi  kutoa utaratibu ambao  utawezesha wanahabari  nchini  kufanya kazi kwa usalama bila hofu wala dharau,kutoa elimu kwa jeshi la polisi  kuhusu  umuhimu wa wanahabari  na jukumu lao katika Taifa.

Hata  hivyo baadhi ya viongozi wa Vyama vya waandishi wa habari Tanzania  ambao wanahudhulio mkutano mkuu wa umoja wa clabu za waandishi wa habari Tanzania walisema tamko hilo halijapewa uzito kutokana na tukio la mauaji lenyewe jinsi lilivyo inatakiwa kupewa uzito wa kina.

“Hili Tamko lilitakiwa kupewa uzito sana kwani  sisi tuliokuwepo katika msiba huo kwa ujumla inasikitisha sana hivyo tamko ni muhimu lipewe uzito zaidi kulingana na mauaji yenyewe yanavyotisha  hivyo tufuate maamuzi ya viongozi wa clabu waliotoa matamko ya kususia habari za polisi mpaka pale watakapokuwa wameridhia  kukaa meza moja na wanahabari  juu ya mauaji hayo”alisema mmoja wa viongozi wa clabu za waandishi wa habari Tanzania Bw. Christopher Nyenyembe.

WASIFU WA MAREHEMU DAUDI MWAGOSI

Kamanga na Matukio | 01:01 | 0 comments
Wasifu wa Marehemu Daudi Mwagosi

Aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha chanell Ten kituo cha Iringa aliyefariki kwa kuuawa na askari kwa kufyatiliwa kitu kinachodaiwa kuwa ni bomu Agosti 2 saa 9;30 kijijini Nyololo wilayani Mufindi.

 Alizaliwa Januari 30 1972 katika mji wa Bankroft nchini Zambia: Baba yake ni Anyingisye Mwangosi na mama yake  Bi, Kissa Myogels akiwa ni mtoto wao wa kwanza kati ya  watoto wao wawili wa pili anaitwa Anderw Mwangosi.

Elimu.
Alipata elimu ya msingi katika shule ya Chambeshi nchini Zambia ambapo alisoma hadi darasa la tatu na kuhamia nchini Tanzania wilaya ya Tukuyu kijiji cha Bsoka ambapo alimaliza darasa la saba na kufaulu kujiunga shule ya sekondari ya Tosamaganga na kusoma kidato cha kwanza hadi cha nne ambapo alijiunga na Chuo cha Uhasibu Mbeya na kumaliza diploma mwaka 1998 ambapo mwaka 2000 aliajiriwa na shirika la umeme Tanesco na kufanya kazi kwa muda wa miaka miwili tu na kuacha kazi hiyo mwaka 2002. Alianza kazi ya upigaji picha za mnato na za kutembea ambapo alihamia mkoani Iringa na kufanya kazi zake huko.

Mwaka 2002 alifanikiwa kuoa mke Bi. Itika Rauben Mwakapeje  na kufanikiwa kupata  watoto wanne wakiwemo watatu wa kiume na mmoja wa kike.

Mwaka 2005 akaanza kujihusisha na kazi ya uandishi habari kwa ushawishi wa Bw. Dominick Hule ambaye alikuwa rafiki yake wa karibu aliyekuwa akiripotia chombo cha channel ten na kumfundisha kazi hiyo ambapo uongozi uliona anafaa kufanya nae kazi wakamkubali atumikie chombo chao, na kujikita zaidi kwa kujiunga na chama cha waandishi wa habari  IPC. Mwaka 2011 alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa klamu ya waandishi wa habari Iringa IPC  na kufanya kwa uadilifu na kuongoza wanahabari mkoani humo hadi mauti yalipomkuta.

Salam pamoja na Ibada ya Mazishi imeanza sasa Itete Tukuyu mkoani Mbeya katika mazishi ya Mwandishi wa Habari Daudi Mwangosi

Kamanga na Matukio | 03:07 | 0 comments
Mke wa Marehemu Daudi Mwangosi akilia kwa Uchungu Muda huu
 Maelfu ya  watu wakiongezeka kufika katika Mazishi ya mwandishi wa habari wa Chanel Ten Daudi Mwangosi Muda huu
 Mheshimiwa Mark Mwandosya ambaye ni Waziri ofisi ya Rais na pia Mbunge wa Rungwe Mashariki akitoa salam kwa Niaba ya Serikali
 Watu wakiwa wengi na wenye utulivu wakisikiliaza watu mbalimbali wakitoa salam zao kwa ndugu wa Marehemu
 Mjane Mke wa Marehemu Daudi Mwangosi aliyejishika, akiwa na uchungu muda huu
Ibada ikiwa inakaribia kuanza
 Ibada ya mazishi ndio imeanza muda huu
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa wenye majonzi Makubwa
Waandishi wa Habari wakiwa katika msiba wa kwanza kutoka kulia ni Ndugu Joseph Mwaisango ambaye ni mwandishi mkuu wa Mbeya yetu Blog, Rais wa UTPC Keny Simabaya, pamoja na Felix Mwakyembe .

Endelea kufuatilia Moja kwa moja hapa

PICHA ZOTE NA MBEYA YETU BLOG

TAMKO LA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MBEYA (MBPC) DHIDI YA JESHI LA POLISI NCHINI.

Kamanga na Matukio | 04:27 | 0 comments

TAMKO LA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MBEYA (MBPC) DHIDI YA JESHI LA POLISI NCHINI.

Chama cha waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya (MBPC)kimepokea kwa masikitiko taarifa ya mauaji ya Mwandishi na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Iringa, Daudi  Mwangosi yanayodaiwa kufanywa na Jeshi la Polisi Mkoani Iringa tarehe 2/9/2012.

Kutokana na mauaji hayo na kutoridhishwa na nguvu kubwa kupita kiasi inayotumiwa na polisi dhidi ya raia, Waandishi wa habari Mkoa wa Mbeya wanaungana na waandishi wa habari nchini kusitisha kutoa taarifa za jeshi la polisi hadi hapo jeshi hilo litakapokubali kuchukua hatua kali za kinidhamu kwa polisi waliohusika kufanya mauaji  hayo akiwemo, Kamanda wa polisi Mkoa wa Iringa  aliyeongoza operesheni hiyo.

Tamko hilo pia limeeleza wazi kuwa muda umefika kuwe na mkataba maalumu wa kazi  kati ya waandishi wa habari na jeshi la polisi na kwamba atakayekiuka hatua za kisheria dhidi ya majukumu ya kila chombo zichukuliwe hatua kali za uwajibishaji.


Ili kujenga dhana ya uwazi na uwajibikaji,Waandishi wa habari Mkoa wa Mbeya wanamtaka Waziri wa mambo ya ndani, Mkuu wa jeshi la polisi nchini (IGP) na Kamanda wa mkoa wa Iringa wajiuzulu nyadhifa zao kwa kuwa wameshindwa kusimamia vyema usalama wa raia na mali zao.

Pia Tamko hilo limebainisha mfumo wa uundwaji wa tume ya kuchunguza kifo hicho haupaswi kuongozwa na Jeshi la polisi kwa kuwa ndio waliohusika na mauaji hayo na kwamba tume huru itakayoundwa ipewe muda maalumu ili majibu yapatikane mapema na  kwa haraka na hatua za kisheria zichukuliwe kwa wahusika.

Waandishi wa habari Mkoa wa Mbeya, wanaamini kuwa Serikali na jeshi la polisi litachukua hatua stahiki kwa waliohusika na mauaji ya Mwandishi Daudi Mwangosi, na pia Polisi watajitathmini upya katika utendaji wa shughuli zake hasa katika udhibiti wa vurugu na uzuiaji wa maandamano.


………………………………..
Christopher Nyenyembe,
Mwenyekiti MBPC.


Nakala ;

1.Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama.

2.Inspekta wa Jeshi la Polisi(IGP).

3.Vyombo vyote vya Habari.

SITA WASHIKILIWA NA POLISI KWA KUFANYA VURUGU,KUVUNJA VIOO GARI LA DC MBARALI, BAADA YA CHUO KUFUNGWA

Kamanga na Matukio | 02:09 | 0 comments
Na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
 JESHI  la polisi Mkoani Mbeya linawashilia wanafunzi  sita akiwemo Mkuu wa Chuo  cha uuguzi   Chimala  Francis Mteja  kwa  tuhuma za kuhamasisha vurugu  zilizopelekea  kuharibu gari la Mkuu wa Wilaya ya  Mbarali Gulamu Hussen Kiffu kuvunjwa vioo,kutoa upepo wa matairi baada ya serikali kufunga chuo hicho kwa kutokuwa na hadhi ya kudaili wanafunzi.
 
Akizungumza Kamanda wa polisi mkoni mbeya.Athuman Diwani alisema kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 11 za jioni baada ya mkuu wa wilaya kuongoza na baadhi ya viongozi wa serikali  hususan kamati ya ulinzi na usalama wilaya kwa lengo la kutaka kujua sababu za chuo hicho kuendelea kufundisha wakati serikali ilitoa agizo kifungwe.

Aidha kamanda  Diwani  amewataja wanaoshikiliwa na polisi kuwa ni Mkuu wa Chuo  Francis Mtega () steven Mapunda (19) Isaya Katuwa (23)  Lugano Mwalupasya (22) emmanue bukuku (24) na steven Mapunga ambao wanatarajia kufanya mtihani wiki ijayo ya kuhitimu mafunzo ya uuguzi.

Aidha alisema kuwa kutokana na upelezi kukamilika watuhumiwa watano watafikishwa mahakani leo ambapo mkuu wa chuo atafikishwa mara baada ya uchunguzi kukamili
 
Alisema   muda mfupi  kwa  lengo la  kuzungumza na uongozi wa chuo ndipo baadhi ya wanafunzi  walivamia gari la mkuu wa wilaya na kuaza kuvunja vioo kwa kutumia mawe,na kisha kutoa upepo kwa malengo yasiyojulikana.
 
“Tukio hilo lilitokea jana na linaonyesha ni mpango uliokuwa umepangwa na uongozi wa chuo kwani serikali ina malengo mazuri kwa watanzania  na lengo kuu ilitaka chuo hicho kisajiliwe  ili kitambulike serikali na kuweza kutoa wauguzi walio na sifa na kuwawezesha kupata ajira itakayotambulika serikalini”Alisema

“Ni kitu cha kushangaza sana mkuu wa chuo ni mwalimu huyo huyo,mhasibu,na kwamba kulikuwa hakuna sababu ya kufanya vurugu bali  kilikuwa ni kitu cha kutoa vielelezo vya udaili wa chuo na  uchunguzi umebaini chuo hicho kimeanza muda mrefu na tayari  kimeweza kutoa wauguzi katika Nyanja mbalimbali  bila ya serikali kutambua  kama hakijasajiliwa na hakitambuliki ’Alisema.

Aidha diwani ametoa onyo kwa wanafunzi katika vyuo kutojiingiza katika mikumbo isiyokuwa na tija na hivyo kuchangia kuisabishia hasara serikali kutokana na uharibifu uliojitokeza katika vurugu hizo na  kuongeza kuwa watuhumiwa wa takaobainika kuhusika katika vurugu hizo watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
 
Diwani alisewa mpaka sasa wanafunzi wanaoshilikiwa 32 ambapo kati ya hao 5 ndio waliobainika kuhusika na vurugu hizo na wanatarajiwa kufikiswa  mahakamani wakati wowote kujibu tuhuma zinazowakabili ili sheia ichukue mkondo wake ili iwe fundisho kwa wengine.
 
Akizungumza kwa  njia ya Simu Mkuu wa Wilaya ya Mbarali . Gulamu Hussen Kiffu alikiri kutokea kwa vurugu hizo  zilizotokana na uamuzi wa serikali kufunga chuo hicho  kutokana na kutokuwa na sifa ya kufundisha na kudaili wanafunzi  wa fani ya uuguzi kwani kilikuwa hakina hati ya utambulisho wa usajiri serikalini.

Kiffu alisema kuwa baada ya serikali kutambua tatizo hilo ndipo walipo kumuhita  Mkuu wa Chuo  hicho Francis Mteja katika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ambapo aligoma kuhudhuria na kueleza kuwa yeye anaendelea kufundisha ndipo walipolazimika kufika chuoni hapo jana.
 
“Serikali ilikuwa na lengo zuri sana na chuo hicho lakini kutokana na uelewa mdogo ndio imeweza kutokea hali hiyo kwani serikali haiwezi kuvumilia  vyuo kuendeshwa kienyeji wakati huo watu watakaohitimu hapo watapata ajira katika vituo vya afya ,hali hiyo inaweza kuleta madhara kwa watanzania wasiokuwa na hatia kiafya.”Alisema.

Aidha baadhi ya wanachi  Mkoani mbeya wamelaani vikali tabia hiyo na kuitaka serikali kuchua hatua za makusudi kwani kufanya hivyo ni uvunjifuni ya nchi yetu na taifa kwa ujumla kwani kiongozi wa serikali anapaswa kuheshimwa kwani ndio kiungo kikuu katika kuleta maendeleo ya nchi yetu.


Aidha uchunguzi uliofanywa na mwananchji umeabaini  kuna baadhi ya wananchuo walikuwa wametoka katika mazoezi ya vitendo katika vituo mbalimvali vya afya na wanatarajia kufanya mitihani ya kuhitimu  jumatatu na hivyo kujikuta wakiingia hasara kutokana na chuo hicho kufungwa.

WIVU WA KIMAPENZI , MWANAUME AFUMANIWA NA KUUAWA, - MBEYA.

Kamanga na Matukio | 02:07 | 0 comments
Na Ester Macha,Mbeya
Matukio ya wivu wa kimapenzi yameendelea kushika kasi Mkoani Mbeya ambapo Mkazi wa Kijiji cha Ivela  kata ya Bara Mkoani Mbeya  Denis Nelson kuuwa kwa wivu wa kimapenzi baada ya kukutwa akifanya mapenzi na mke wa mtu .

Imeelezwa kuwa marehemu alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mmoja aitwaye Maines Fwambo  na siku ya tukio marehemu alikwenda nyumbani kwa mwanamke huyo kwa lengo la kufanya mapenzi.

Wakizungumza na majira mashuhuda wa tukio hilo wambao hawakutaka kutaja majina  yao wamesema kuwa Agosti 29 mwaka huu majira ya saa 4.asubuhi wakati marehemu akielekea nyumbani kwa mwanamke huyo walitokea shemeji za mume wa mwanamke huyo na kuanza kumfuatilia marehemu.

Wamesema kuwa mara baada ya kufika marehemu nyumbani kwa mwanamke huyo  shemeji za mwanamke huyo nao walifika eneo la tukio na kufanikiwa kumkuta marehemu akiwa ndani na kuanza kumshushia kipigo.

Baada ya kuingia ndani walimkuta marehemu akifanya tendo la ndoa  na mwanamke huyo ndipo walipochukua jukumu la kumnywesha sumu na kuanza kumpiga  mwanaume huyo sehemu mbali mbali za mwili wake.

Hata hivyo marehemu alifariki dunia  kabla ya kufika hospitali hospitali ya mission mbozi kupatiwa  matibabu.

Kamanda wa polisi Mkoani Mbeya Diwani Athuman amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba wahusika wote wanasakwa na polisi ili waweze kuchukuliwa hatrua za kisheria.

CHANJO YA MIFUGO HASA MBWA NI KITENDAWILI MKOANI MBEYA

Kamanga na Matukio | 02:06 | 0 comments
Na Esther Macha, Mbeya
Licha ya Mkoa wa Mbeya kuwa na idadi kubwa ya Mbwa bado imeonekana kuwa kuna tatizo kubwa kwa wafugaji kutokuwa na utamaduni wa kuchanja mbwa zao kwa madai kuwa grama  za dawa  za uchanjaji kuwa kubwa.

Akizungumza na Mwandishi wetu ofisini kwake , Ofisa Mifugo wa Mkoa wa Mbeya Dkt.Solomon Nong’ona alisema kuwa mbwa waliopo katika Mkoa ni wengi ukilinganisha na waliochangwa kwa Mkoa mzima.

Dkt. Nong’ona alisema kuwa Mkoa mzima una mbwa zaidi ya 70,000 lakini kati ya hao waliochanjwa ni wachache ukilinganisha na idadi iliyopo ya mbwa katika Mkoa.

“Kati ya julai 2011 mpaka julai  2012  ni mbwa 7,849 ambao ni sawa na asilimia 10 tu ya mbwa waliochinjwa hili ni tatizo kubwa  hivyo kuna haja wafugaji  wa mbwa wakaelimishwa si kutoa saababu za grama kubwa za uchanjaji”alisema.

Hata hivyo alisema Mbeya jiji pekee  kwa wiki inakuwa na matukio 20 ya watu kuumwa na mbwa  na kwamba wilaya ambazo zinaongoza ni pamoja na Mbeya Jiji  ambapo watu 223 waliumwa na Mbwa, Mbozi 206,Chunya 64.

Aidha Ofisa Mifugo huyo alisema kuwa wafugaji wa Mbwa hawako makini na mifugo yao kwa kuona hakuna umuhimu wa kuchanja  mbwa zao ambazo zinaleta athari kwa jamii.

Akizungumzia kuhusu grama za uchanjaji alisema kila mbwa anachanjwa kwa sh.5000 lakini badala yake wafugaji wa mbwa wamekuwa wakiona hiyo ni fedha nyingi na kuacha mifugo hiyo ikiendelea kuteketeza maisha ya wananchi wakati uwezo wa kuwachanja upo.

“Grama ambayo mimi naweza kuiona ni kwa mtu ambaye ameumwa na mbwa kwani Wilaya zingine hakuna hiyo dawa ambapo humlazimu mwananchi kupanda gari na kuja Mkoani kupata dawa hiyo kwa kutumia fedha ili aweze kufika hapa,ni jana tu alikuja mwananchi mmoja kutoka Ileje ambaye aliumwa  na mbwa ”alisema.

Aidha alitoa wito kwa  wafugaji wa mbwa kufuga mbwa na paka kwa ustaarabu ili zisiweze kuleta athari kwa jamii .

CHANJO YA MIFUGO HASA MBWA NI KITENDAWILI MKOANI MBEYA

Kamanga na Matukio | 02:04 | 0 comments
Na Esther Macha, Mbeya
Licha ya Mkoa wa Mbeya kuwa na idadi kubwa ya Mbwa bado imeonekana kuwa kuna tatizo kubwa kwa wafugaji kutokuwa na utamaduni wa kuchanja mbwa zao kwa madai kuwa grama  za dawa  za uchanjaji kuwa kubwa.

Akizungumza na Mwandishi wetu ofisini kwake , Ofisa Mifugo wa Mkoa wa Mbeya Dkt.Solomon Nong’ona alisema kuwa mbwa waliopo katika Mkoa ni wengi ukilinganisha na waliochangwa kwa Mkoa mzima.

Dkt. Nong’ona alisema kuwa Mkoa mzima una mbwa zaidi ya 70,000 lakini kati ya hao waliochanjwa ni wachache ukilinganisha na idadi iliyopo ya mbwa katika Mkoa.

“Kati ya julai 2011 mpaka julai  2012  ni mbwa 7,849 ambao ni sawa na asilimia 10 tu ya mbwa waliochinjwa hili ni tatizo kubwa  hivyo kuna haja wafugaji  wa mbwa wakaelimishwa si kutoa saababu za grama kubwa za uchanjaji”alisema.

Hata hivyo alisema Mbeya jiji pekee  kwa wiki inakuwa na matukio 20 ya watu kuumwa na mbwa  na kwamba wilaya ambazo zinaongoza ni pamoja na Mbeya Jiji  ambapo watu 223 waliumwa na Mbwa, Mbozi 206,Chunya 64.

Aidha Ofisa Mifugo huyo alisema kuwa wafugaji wa Mbwa hawako makini na mifugo yao kwa kuona hakuna umuhimu wa kuchanja  mbwa zao ambazo zinaleta athari kwa jamii.

Akizungumzia kuhusu grama za uchanjaji alisema kila mbwa anachanjwa kwa sh.5000 lakini badala yake wafugaji wa mbwa wamekuwa wakiona hiyo ni fedha nyingi na kuacha mifugo hiyo ikiendelea kuteketeza maisha ya wananchi wakati uwezo wa kuwachanja upo.

“Grama ambayo mimi naweza kuiona ni kwa mtu ambaye ameumwa na mbwa kwani Wilaya zingine hakuna hiyo dawa ambapo humlazimu mwananchi kupanda gari na kuja Mkoani kupata dawa hiyo kwa kutumia fedha ili aweze kufika hapa,ni jana tu alikuja mwananchi mmoja kutoka Ileje ambaye aliumwa  na mbwa ”alisema.

Aidha alitoa wito kwa  wafugaji wa mbwa kufuga mbwa na paka kwa ustaarabu ili zisiweze kuleta athari kwa jamii .
 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger