Pages


MGOMO WA WALIMU,IMEKUWA FURSA KWA VIBAKA KUNUFAIKA - TUNDUMA - MBEYA.

Kamanga na Matukio | 04:35 | 0 comments
Na: Ezekiel Kamanga,Tunduma Kufuatia Mgomo wa walimu ulioanza jana, wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi katika Mji mdogo wa Tunduma,Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya waliamua kuandamana ili kudai haki ya kufundishwa katika maandamano ambayo yaliingiliwa na vibaka ambao baadaye walivunja ofisi za Halmashauri ya mji huo na kuiba mali kadhaa kisha kuchoma nyaraka zilizokuwemo. Hatua hiyo ilijitokeza mapema saa 2 asubuhi wakati wanafunzi wa shule 14 za msingi zilizopo katika halmashauri wa Tunduma,walipojikusanya na kufanya maandamano hadi nyumbani kwa diwani ambapo baada ya kumkosa walielekea kituo cha polisi cha mjini hapa kabla ya kufika ofisi za halmadhauri ya mji. Kwa mujibu wa...

SIKU AMBAYO SERIKALI YA KIJIJI CHA IYOVYO ILIYOTOONDOLEWA MADARAKANI.

Kamanga na Matukio | 02:55 | 0 comments
 Jinsi alivyokuwa akiondoka mkutanoni Mwenyekiti wa Kijiji cha Iyovyo,Kata ya Totowe,Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Bwana Rashid Likuta mara baada ya kuvuliwa madarakani kwa kile kilichodaiwa kuwa anajihusisha na ufujaji wa pesa za kijiji wa zaidi ya shilingi laki nne na kutosoma taarifa za mapato na matumizi.  Baadhi ya Wajumbe walioteuliwa kuchunguza ubadhilifu wa pesa za Kijiji cha Iyovyo,wakikamilisha taarifa kabla...

UGALI WASABABISHA WANANCHI KUUMWA MATUMBO - MBOZI

Kamanga na Matukio | 02:52 | 0 comments
Na Esther Macha,Mbozi Wakulima wa Kijiji cha Ichesa Kata ya Myovisi ,Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya wamelalamikia kuumwa matumbo baada ya kula ugali unaodaiwa kutokana na mbegu feki ya  mahindi ya njano inayodaiwa kusambazwa na wakala mmoja kijijini hapo. Kutokana na adha hiyo wakulima hao wameziomba mamlaka husika na watafiti kulifuatilia kwa kina suala la ununuzi wa vocha za mbolea ya ruzuku kutoka kwa wakulima kumuuzia wakala kwa bei ya kati ya sh.2,000 hadi Sh.4,000 unaodaiwa kufanywa na wakala mmoja jina limehifadhiwa. Wakizungumza na waandishi wa habari hizi baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Ichesa (majina tunayo)walisema kuna hatari kubwa kwa mwaka huu waananchi wa Kijiji hicho...

UMUHIMU WA MAJI VIJIJINI NA MIJINI KWA WANANCHI

Kamanga na Matukio | 02:51 | 0 comments
Na Ester Macha. Tunapozungumzia maji  kwa binadamu  ni pamoja na huduma hiyo kupatikana vijijini na mijini ambako mahitaji hayo ni muhimu kwa wananchi waishio maeneo  hayo lakini hali hiyo imekuwa tofauti kwa maeneo ya pembezoni na kujikuta wakiishi bila ya kupata huduma ya maji safi na salama. Kutokana na hali hiyo  serikali ilitunga sera ya maji kwa kushirikiana na walengwa  kwa kubuni, kupanga, kujenga, kuendesha, kufanya matengenezo na kuchangia gharama za huduma utunzaji na usimamizi endelevu wa rasilimali za maji kwa kushirikisha wadau wote kwa kupunguza   majukumu ya utekelezaji kwa serikali ili kusimamia,kuratibu, kushauri, kuwezesha na kutoa...

HAKIMU ATOKA NJE YA MAHAKAMA NA KUZICHAPA KAVU KAVU NA MWANANCHI.

Kamanga na Matukio | 05:22 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga,Iyula Mbozi. Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo,Kata ya Iyula,Tarafa ya Iyula,Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya Mheshimiwa Grace Kivelege aliuacha Ukumbi wa mahakama hyo na kutoka nje kisha kuanza kuzozana na mwananchi mmoja Bwana Sebastian Kilindu aliyekuwa amefika mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza kesi. Sababu ya ugomvi huoni pale Hakimu huyo alipomtaka mshitakiwa Bwana Laurence Julias,kuingia mahabusu ndipo Bwana Kilindu alipinga hali iliyompelekea hakimu kumkunja shingoni na kuamuliwa na mwandishi wa habari hizi,huku wananchi wakishangilia zogo hilo wakitaka Hakimu apigwe kutokana na kinachodaiwa kuwa kajijengea mazingira ya rushwa. Baada ya kuamuliwa hakimu...

SERIKALI YAOMBWA NA WAKULIMA NA WAFUGAJI KUFANYIA UCHUNGUZI MADINI YA KULAMBA NA MIFUGO.

Kamanga na Matukio | 03:18 | 0 comments
*Habari na Ester Macha,Mbeya. Wakulima na Wafugaji wa Kijiji cha Itizi,wilaya ya Mbeya Vijijini wameiomba Serikali kufanya uchunguzi kuhusu aina ya madini yanayodaiwa kuchakachuliwa na hivyo kusababisha asilimia kubwa ya ng’ombe kutokuzaa kwa zaidi ya miaka miwili sasa licha ya mifugo hiyo kulamba madini,kupata joto na kupandishwa. Wamesema kuwa wameshindwa kuendelea kujenga mitambo ya Biogesi kutokana na kuhofia mradi huo kumalizika mapema na kukosa ruzuku,inayotokana na mradi unaofadhiliwa na Programu ya uenezi wa mitambo ya biogesi ngazi ya Kaya Tanzania (TDBP) chini ya Camartec kwa wakulima wanaojenga. Wakizungumza na gazeti hili wakazi wa kijiji cha Itizi Bw.Anyesile Mwasanga...

MWANANCHI ATAKAYEHARIBU VYANZO VYA MAJI NCHINI KUCHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.

Kamanga na Matukio | 03:16 | 0 comments
 Mh. Rais Kikwete akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji safi na upimaji wa maji katika Kijiji cha  Swaya,Wilaya ya Mbeya vijijini Julai 22 mwaka huu.  *********  Na Bosco Nyambege Mbeya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema itamchukulia hatua kali za kisheria  mwananchi yeyote atakayebainika kuharibu  vyanzo vya maji nchini.  Onyo hilo limetolewa hivi karibuni ...

UGOMVI ULIOKUWA UKIHUSISHA PANDE MBILI ZA FAMILIA YA MAREHEMU WASULUHISHWA,.

Kamanga na Matukio | 01:42 | 0 comments
Normal 0 false false false MicrosoftInternetExplorer4 /* Style Definitions */ table.MsoNormalTable {mso-style-name:"Table Normal"; mso-tstyle-rowband-size:0; mso-tstyle-colband-size:0; mso-style-noshow:yes; mso-style-parent:""; mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt; mso-para-margin:0in; mso-para-margin-bottom:.0001pt; mso-pagination:widow-orphan; font-size:10.0pt; font-family:"Times...

TUKIO LA WANAFAMILIA KUGOMBANIA MALI ZA MAREHEMU.

Kamanga na Matukio | 01:32 | 0 comments
Sehemu ya samani iliyokuwa ikimilikiwa na marehemu Eva Emmanuel Mligula na Emmanuel Mwaigaga,iliyogombaniwa na ndugu zikiwa zimetolewa nje kwa lengo la kuhamishwa katika Mtaa wa Utukuyu,Kata ya Uyole Jijini Mbeya.  Baba Mzazi na Kaka wa marehemu Eva wakiwa nje ya nyumba iliyokuwa ikimilikiwa na  marehemu Eva Emmanuel Mligula na Emmanuel Mwaigaga katika Mtaa huo nayo iliingizwa katika mgogoro wa kugombaniwa,hali iliyopelekea Serikali...

HII NI HALI HALISI YA ELIMU YA TANZANIA

Kamanga na Matukio | 02:42 | 0 comments
 Mwanafunzi wa darasa la 5 akigalagala chini ya sakafu kutokana na mwalimu kutokuwepo darasani ni katika Shule ya Msingi Iyovyo,Kata ya Totowe Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.  Mandhari ya moja ya Chumba cha darasa katika Shule ya Iyovyo.  Wazazi wa Kijiji cha Iyovyo wakiwa katika malumbano juu ya suala la michango kufunjwa na Uongozi wa kijiji hivho. Pichani ni chumba cha darasa kikiwa kimejaa vumbi na baadhi ya wanafunzi...

UHABA WA WALIMU WA MASOMO YA SAYANSI,SERIKALI YASHAURIWA KUANDAA MIKAKATI ENDELEVU JUU YA VIJANA

Kamanga na Matukio | 02:40 | 0 comments
Na Bosco Nyambege,Mbeya Serikali imeshauriwa kuwa na mikakati maalumu ya kuwaandaa Vijana katika misingi ya kuyapenda masomo ya Sayansi kwa lengo la kuwa walimu watakaobobea katika ufundishaji wa masomo hayo yatakayowasaidia wanafunzi kujitegemea na siyo kutegemea ajira. Wito huo umetolewa na baadhi ya wakuu wa shule za sekondari mkoani Mbeya wakati wa mahojiano maalum kuhusiana na uhaba wa walimu wa sayansi mashuleni na kitu ambacho kinapelekea kukosa walimu wa masomo hayo. Kwa upande wake mwalimu mkuu wa Shule ya sekondari Regco iliyopo Jijini Mbeya,Joshua Mwakitalima amesema kuwa ili kujenga kizazi ambacho kitaweza kujitegemea na kupambana na maisha ni vema Serikali ikajikita...

WIZI WA MTOTO WA MIEZI 9 NA WIKI MIWILI.

Kamanga na Matukio | 02:39 | 0 comments
Na Bosco Nyambege,Mbeya Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamtafuta mtu aliyehusika na kitendo cha kumwiba mtoto mwenye umri wa miezi miwili katika Kijiji cha Manga Madibira Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya. Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa polisi Mkoani hapa Diwani Athumani amesema kuwa tukio hilo limetokea mnamo Julai 18 mwaka huu majira ya saa kumi jioni. Amemtaja mama wa mtoto huyo kuwa ni Bi.Tabu Chapunga(18),mkazi wa mkunywa na aliibiwa mtoto wake aitwaye Gulo Manga wakati mama yake akiwa amekwenda kuchota maji. Aidha,amesema kuwa mtu huyo aliingia chumbani kwa mama huyo na kumchukua kichanga hicho na kutokomea nacho kusiko julikana. Hata hivyo Kamanda Diwani...

WATU WATATU WAFARIKI DUNIA.

Kamanga na Matukio | 05:17 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya. Watu watatu wamefariki dunia katika matukio matatu tofauti Mkoani Mbeya,likiwemo la fundi seremala Furaha Msongole kudondoka juu ya paa la nyumba Mtaa wa Mwenge,Kata ya Vwawa Wilaya ya Mbozi. Tukio hilo limetokea majira ya saa 5 asubuhi Julai 17 mwaka huu,fundi huyo ambaye alidondoka wakati akipaua nyumba ya Mtumishi wa Halmashuri ya wilaya hiyo Bwana Moses Kibona. Aidha,jitihada za kujaribu kuokoa uhai wake ziligonga mwamba baada ya kufikishwa katika Hospitali ya wilaya hiyo na kugundulika kuwa ameshafariki dunia. Naye Mwenyekiti wa mtaa huo Bwana Michael Mwaipwisi,amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa katika...

MAAJABU:- KIJANA AFUMANIWA AKIMBAKA NG'OMBE WA JIRANI YAKE ZIZINI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 04:11 | 0 comments
Na Bosco Nyambege,Rungwe. Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Tumsifu Mwambusi (20),mkazi na mkulima wa Kijiji cha Mwela,Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya amefumaniwa akimbaka ng’ombe. Tukio hilo la ajabu yake limetokea Julai 15 mwaka huu majira ya saa mbili za usiku ambapo jamaa huyo alikwenda kwenye makazi ya Bwana Leonard Mwangwemba,kisha kuingia ndani ya zizi na kuanza kumbaka   ng’ombe huyo hali iliyopelekea ng’ombe huyo kuanza kupiga kelele kwa kuomba msaada.  Ndipo wakazi wa eneo hilo walielekea eneo la tukio na kumkuta kijana huyo akiendelea na kitendo hicho na kumshushia kipigo cha mbwa mwizi mara baada ya kuvunja amri...

COCACOLA YAZIDI KUMWAGA MAMILIONI KWA WATEJA WAKE.

Kamanga na Matukio | 03:21 | 0 comments
Habari na Angelica Sullusi,Mbeya. Idadi ya washindi wa promosheni ya Vuna Mkwanja inayoendeshwa na Kampuni ya vinywaji baridi ya Cocacola tawi la Mbeya, imeendelea uongezeka mkoani Mbeya baada ya watu wawili kuzawadiwa shilingi milioni moja kila mmoja na mwingine shilingi laki moja walizojishindia baada ya kunywa soda za kampuni hiyo. Washindi hao wamekabidhiwa fedha zao juzi kwenye kituo cha mabasi madogo maarufu kama daladala katika eneo la Sido mbele ya umati mkubwa wa watu waliojitokeza kushuhudia tukio hilo. Nafed Sanga, makazi wa Tunduma wilayani Mbozi na Juma Aron Kaseka mkazi wa mji mdogo wa Mbalizi ndio walioibuka na kitita cha shilingi milioni moja kila mmoja . Mwingine ...
Pages (14)1234567 Next
 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger