Pages


MTOTO Adolotea Njavike(1.4) anaomba msaada wa matibabu kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kufanyiwa upasuaji kutokana na Kichwa na Kiwiliwili kuungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi.

Chimbuko Letu | 07:36 | 0 comments
MTOTO Adolotea Njavike(1.4) ambae Kichwa na Kiwiliwili vimeungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi.








Mama Mkubwa wa Mtoto huyo, Salome Kiegu(35) mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Iyunga Jijini Mbeya anasema Mtoto huyo akiwa na mama yake walipata janga la moto katika mazingira ya kutatanisha waliangukia kwenye moto ambapo Mtoto huyo aliungua vibaya.








Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu akiwa amempakata mtoto huyo




Baadhi ya waandishi wa habari wakiongea na mama mkubwa wa mtoto huyo




MTOTO Adolotea Njavike(1.4) anaomba msaada wa matibabu kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kufanyiwa upasuaji kutokana na Kichwa na Kiwiliwili kuungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi.

Akizungumza kwa masikitiko Mama Mkubwa wa Mtoto huyo, Salome Kiegu(35) mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Iyunga Jijini Mbeya anasema Mtoto huyo akiwa na mama yake walipata janga la moto katika mazingira ya kutatanisha waliangukia kwenye moto ambapo Mtoto huyo aliungua vibaya.

Anasema tukio hilo lilitokea Mwaka jana Mwezi wa Nane lakini alipopatiwa matibabu katika kituo cha afya mtoto huyo aliungana ngozi ya kidevu na kifua hali inayomletea shida ya kula na kufurahi na wenzake.

Anasema tangu kipindi hicho alimchukua mtoto huyo kwa mama yake na kuanza kuomba msaada wa matibabu baada ya kumpeleka katika Hospitali ya Ikonda iliyoko Makete Mkoani Njombe ambapo Wataalamu walimwambia atafute Shilingi Milioni Moja ili mtoto wake aweze kutibiwa.

Ameongeza kuwa baada ya muda wataalamu hao walimwambia asubiri Wazungu kutoka Ulaya ambao wataweza kumtibia mwanaye ambapo baada ya kusubiri kwa muda kidogo Wazungu hao walifika na kumcheki Mwanaye kisha kumwambia wao hawana utaalamu isipokuwa aende CCBRT Dar Es Salaam ambako ataweza kutatuliwa tatizo lake.

Aidha kutokana na kuambiwa hivyo Mama huyo anaomba msaada kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kumpeleka Mtoto wake kwa matibabu kutokana na kutokuwa na uwezo wa kuweza kusafiri hadi DSM pamoja na gharama za matibabu kuwa kubwa.

Amesema anahitaji zaidi ya shilingi Milioni 2 ili ziweze kumsaidia kusafiri kugharamia matibabu pamoja na huduma za Kawaida kipindi atakachokuwepo Jijini Dar Es Salaam wakati akisubiri matibabu ya Mwanaye.

Mtu yeyote mwenye kuguswa na tatizo hilo anaweza kuwasiliana moja kwa moja na Mama huyo kupitia simu yake ya Mkononi namba 0752 986879 au Nyumbani kwake Iyunga Mtaa wa Maendeleo Jijini Mbeya.

Na Mbeya yetu

VIONGOZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI WATAKIWA KUWA KARIBU NA WANANCHI.

Chimbuko Letu | 23:46 | 0 comments
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Dr, Jakaya Kikwete akiinua jembe na nyundu kwa maana ya nembo ya chama hicho mara baada ya kuingia uwanjani.

Jakaya Kikwete alipokuwa akianza kutoa hotuba mara baada ya kuingia katika uwanja huo.

baadhi ya viongozi wa chama hicho wakimshangilia mwenyekiti Jakaya Kikwete alipokuwa akiingia uwanjani.

Raisi Kikwete alipokuwa akiingia katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine kwaajili ya maadhimisho hayo.
............................................................................................................


Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Dr, Jakaya Mrisho Kikwete amewataka viongozi na wanachama wa chama hicho, kuwa karibu na wananchi kwa lengo la kusikiliza matatizo ya wananchi na kuyatatua, kwakufanya hivyo itakuwa chachu ya wananchi kukiamini chama.

Kikwete ameyasema hayo alipokuwa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 37 tangu kuanzishwa kwake yaliyofanyika leo katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini  Mbeya.
Kikwete amesema kumekuwa na tabia kwabaadhi ya viongozi wa chama hicho kutotatua matatizo ya wananchi pindi wanapopewa taarifa kuhusu kero hizo.

Aidha Kikwete amempongeza katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana kwakufanya ziara katika mikoa ya nyanda za juu kusini iliyoleta mafanikio  makubwa katika cha hicho.

Amesema Kinana katika ziara yake alikuwa akisikiliza matatizo ya wananchi na kuyatafutia ufumbuzi, pia amekuwa nao wananchi bega kwa bega katika Nyanja mbali mbali.

Pia Kikwete amesema mpango wa chama cha Mapinduzi ni kuboresha maisha ya watanzania katika sekta mbali mbali ikiwa pamoja na maji, umeme, elimu afya na miundombinu.


SHAHIDI wa tatu katika Kesi inayowakabili Maaskari wawili na Raia watatu ya unyang’anyi wa kutumia Siraha, Pasupuret Sreedhar ambaye ni raia wa India na Mhanga wa tukio hilo ameiambia Mhakama jinsi washtakiwa walivyofanikiwa kuwateka na kuwapora mali zao.

Chimbuko Letu | 14:56 | 0 comments



SHAHIDI wa tatu katika Kesi inayowakabili Maaskari wawili na Raia watatu ya unyang’anyi wa kutumia Siraha, Pasupuret Sreedhar ambaye ni raia wa India na Mhanga wa tukio hilo ameiambia Mhakama jinsi washtakiwa walivyofanikiwa kuwateka na kuwapora mali zao.

Akizungumza katika kesi hiyo huku akiongozwa na Wakili wa upande wa Jamhuri, Basilius Namkambe mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Michael Mteite, Shahidi huyo ambaye hakuweza kuzungumza Kiswahili kabisa hali iliyopelekea Mahakama kumtafuta Wakili maarufu Mkoani Mbeya, Sambwee Shitambala kuwa Mkalimani wake aliweza kuwatambua Watuhumiwa wote watano.

Shahidi huyo aliiambia Mahakama hiyo kuwa Mnamo Januari Mosi Mwaka huu aliwasili Jijini Dar Es Salaam akitokea kwao Nchini India akitumia usafiri wa ndege wa Shirika la Oman akiwa na lengo la kufuatilia mradi wa Uchimbaji dhahabu katika Migodi ya Chunya Mkoani Mbeya inayoendeshwa na kampuni yao ya Otro Mining.

Alisema Januari 3,Mwaka huu alisafiri kutoka Dar Es Salaam kuja Mbeya akitumia Shirika la Ndege la Precision ambapo aliwasili majira ya Saa Saba na Nusu Mchana na kupokelewa na rafiki yake Isaya Mkindi ambaye walielekea naye moja kwa moja hadi Mbeya Hotel alikopata chakula cha Mchana.

Alisema baada ya hapo alipewa Dereva aliyemtaja kwa jina la Ezekia ambaye alimpeleka Mwanjelwa kununua Mablanketi mawili kisha kurudi katika Ofisi ya Rafiki yake huyo ambapo ilipofika majira ya Saa 10:45 jioni walianza safari ya kuelekea Chunya akiwa na rafiki yake pamoja na dereva Ezekia.

Alisema wakiwa njiani walipofika katika Milima ya Kawetere kilomita 20 kutoka Mbeya Mjini walikuta magari mawili yakiwa yameachana kwa mita 200 ambapo walilipita gari moja na ndipo walipokaribia gari lingine wakakutana na vijanaWanne ambao mmojawapo aliwasimamisha na kuomba msaada wa Spana ya kufungulia tairi ya gari yao wakidai kuwa inapancha.

Baada ya kueleza hivyo Wakili wa Serikali aliiomba Mahakama imruhusu Shahidi huyo kama anaweza kuwatambua Watuhumiwa jambo ambalo alitekeleza kwa kuwagusa Mshtakiwa namba moja, Tatu, Nne na Tano kisha kuendelea na kutoa maelezo kuhusu kilichoendelea baada ya kuombwa spana.

Shahidi huyo aliendelea kusema kuwa baada ya Dereva wake kuwajibu kuwa hawana spana ndipo Mtuhumiwa namba tatu ambaye ni Askari Magereza alipotoka na kurudi akiwa na pingu mkononi na kumfunga Dereva kisha kumshusha kwenye gari na kuelekea naye kwenye gari yao ndogo.

Aliongeza kuwa baada ya kufanya hivyo walimshika yeye huku wakimuoneshea panga na kumwamuru asiongee neno lolote kisha kuhamisha mizigo kwenye gari na kupeleka kwenye gari yao ambayo li Kompyuta za Mkononi mbili, begi, mablanketi na Simu za Mkononi ambazo kabla hawajachukua alikuwa ameshawasiliana na Mwenzie aliyoko Chunya aliyemtaja kwa jina la Jamir Amar.

Alisema akiwa ameshikwa na kuongeleshwa na watu hao simu yake ilikuwa ikisikika na wenzie ambao waliweza kutoa taarifa katika Jeshi la Polisi ambalo lilifanikiwa kuwakamata muda mfupi baada ya watu hao kutokomea na vitu vyao na baada ya wao kuachwa akiwemo Dereva aliyekuwa amefungwa pingu kuachiwa.

Hata hivyo Wakili wa utetezi katika kesi hiyo Ladislaus Lwekaza alimuuliza Shahidi huyo kama kweli aliwaona watuhumiwa wakiwa eneo la tukio na siyo kalishwa maneno alijibu anawafahamu kwa sababu aliwaona wakifanya tukio kwa sababu ilikuwa jioni kabla jua halijazima.

Wakili Lwekaza aliongeza kuwa akiruhusiwa kuwabadilisha watuhumiwa mkao wao anaweza kuwatambua Shahidi huyo alijibu anaweza hivyo akatakiwa kutoka nje ili waweze kuwachanganya ndipo awatambue jambo ambalo lilipingwa na Wakili wa Serikali kuwa haijawahi kutokea utambuzi ukafanywa wakati kesi inaendelea kusikilizwa na kuongeza kuwa jambo hilo hufanyika kipindi cha upelelezi.

Kutokana na hoja hizo Hakimu Mteite alikubaliana na hoja ya upande wa Mashtaka hivyo kutupilia mbali maombi ya upande wa mashtaka ya kumtaka Shahidi atoke nje ili wamchanganyie watuhumiwa kwa ajili ya kuwatambua  na kuamuru kuendelea na maswali mengine.

Watuhumiwa hao ni pamoja na Mshitakiwa namba moja ambaye ni Askari Polisi PC James mwenye namba F8302 wa Wilaya ya Mbeya ambaye kabla ya kufikishwa mahakamani alivuliwa Uaskari baada ya kuhukumiwa kijeshi.

Wengine kuwa ni mshtakiwa namba mbili kuwa ni Elinanzi Mshana(22)Mkazi wa Iyela Jijini Mbeya, Askari Magereza mwenye namba B 500 Sajenti Juma Mussa(37) wa Gereza la Ruanda Mbeya,Mbaruku Hamis(29) Mkazi wa Iyela na Amri Kihenya(38) Mkazi wa Iyela.

Akisoma mashtaka yao Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite, Basilius Namkambe alisema watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Januari 3, Mwaka huu majira ya saa 11 jioni katika eneo la Mlima Kawetere barabara ya Mbeya Chunya.

Alisema watuhumiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo kwa kulizuia gari aina ya Pick Up lililokuwa likiendeshwa na Ezekia Matatira (34) Mkazi wa Iyunga Jijini Mbeya ambaye alikuwa na mtu aliyekuwa akifahamika kwa jina la Sreedhar Pasupelet(38) mwenye asili ya Kiasia wakitumia magari madogo mawili ambayo ni GX 100 Toyota Cresta T 782 BEU na Gari linguine ambalo lilikuwa na namba za Chesesi GX 6011832 aina ya Grand Mark II.

Hata hivyo Kesi hiyo iliahirishwa hadi Februari 13, Mwaka huu itakapoendelea tena kwa upande wa mashtaka kuwaleta mashahidi wake.

NDOA YAVUNJIKA RASMI WAVUTANA KURUDISHIANA FEDHA WALIZOPOKEA.

Chimbuko Letu | 15:10 | 0 comments
Bwana harusi akiwa na mpambe wake kanisani wakimsubiri bibi Harusi
Jamaa wameshika vichwa hali haieleweki


Bi Harusi Naomi Ngoje akiwa amejilalia chumbani akiwa anahuzunika na kushangaa wazazi wake kurudisha mahali ya mchumba wake



HABARI zilizotufikia hivi punde kutoka nyumbani kwa familia ya Bi harusi ambayo ilikuwa ikipinga ndoa isifungwe kutokana na Bwana harusi kushindwa kumalizia sehemu ya Mahari zinadai kuwa ndoa imevunjwa rasmi na kilichobaki ni mzozo wa kurudishiana fedha.

Pande hizo mbili ya Kiume na Kike zimengia kwenye Mzozo na kuvutana kuhusu fedha baada ya Wazazi wa Mwanamke kukubali kurudisha fedha hizo pamoja na vitu walivyopokea huku kikubwa kikiwa ni upande wa Mwanaume kudai wapewe papo hapo.

Vitu vinavyodaiwa ni Fedha taslimu takribani Shilingi 310,000/= ambazo zilitolewa kwa ajili ya Mkaja pamoja na kiingilio, Blanketi na Mashuka.

Kwa habari zaidi endelea kufuatilia mtandao wako huu ambapo mpaka sasa zaidi ya shilingi 50,ooo zimechangwa na ndugu wa Mume na kujaribu kuziwasilisha kwa ndugu wa Bibi harusi hata hivyo ndugu hao wamekataa kuzipokea.

Kwa habari zaidi Jumatatu endelea kufuatlia.

MAHARI YASABABISHA NDOA ISIFUNGWE , WAUMINI NA MCHUNGAJI WAKESHA KANISANI MBEYA

Chimbuko Letu | 14:10 | 0 comments
Bwana Harusi Fadhili Mahenge akiwa ndani ya Suti akisubiri kufungishwa ndoa 
Bi Harusi Naomi Ngoje akiwa amejilalia chumbani akisubiri hatima ya Wazazi ndipo ajiandae kwenda kanisani tayari kwa kufunga ndoa na mchumba wake waliodumu kwa miezi saba.
Bwana harusi akiwa na mpambe wake kanisani wakimsubiri bibi Harusi
Askofu Kenani Mpalala akiwa katika picha ya pomaja na Bwana Harusi na mpambe wake muda mfupi baada ya kuwasili kanisani
Askofu Keenan Mpalala wa kanisa la Free Pentecost Church of Tanzania akionesha tangazo la Ndoa
Baadhi ya ndugu wa mwanamke wakiwa katika kikao na kuendelea na msimamo wao kuwa mahali lazima imalize ndipo wamtoe binti yao
Jamaa wameshika vichwa hali haieleweki


Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilolo Ndugu Benson Mbwana(aliyevalia shati rangi ya Zambarau) akionyesha ratiba ya sherehe.
Baadhi ya akina mama wakiangalia ratiba ya harusi
Kanisani
Baadhi ya waumini na majirani wakisubiri kanisani



KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Familia moja ya Makunguru  Mtaa wa Ilolo Jijini Mbeya imesababisha sintofahamu dhidi ya Familia nyingine baada ya kumkatalia binti yao kuolewa kwa madai ya waoaji kutokamilisha Mahari waliyokuwa wamepangiwa.

Tukio hilo la aina yake limetokea leo ambapo Bwana harusi aliyefahamika kwa jina la Fadhili Mahenge(28) Mkazi wa Songea aliyekuwa amuoe Naomi Ngoje na harusi yao kufungwa katika kanisa la Free Pentecoste Church Of Tanzania(FPCT) lililopo Makunguru Jijini hapa kushindwa kufungwa baada ya wazazi wa Bibi harusi kuzuia ndoa hiyo hadi Mahari itakapokamilika.

Wakizungumzia tukio hilo Nyumbani kwa Familia ya Bibi Harusi, Mjomba wa Bibi Harusi Dickson Ngoje amesema tatizo la wao kugomea ndoa hiyo ni kutaka waoaji kutimiza masharti waliokuwa wamekubaliana awali ambayo hadi siku ya mwisho familia hiyo haijatekeleza.

Amesema siku ya kwanza waoaji walifika Nyumbani kwa Mzee Ngoje na kujitambulisha ambapo walipangiwa taratibu za mahari kwa mujibu wa Mila kuwa watatakiwa kutoa Blanket 2, Mashuka mawili, Mkaja(200,000), mbuzi 4, Majembe 4, Ng’ombe Jike 2 na Ngo’mbe Dume 1 pamoja na fedha taslimu Shilingi Laki 3.

Amesema baada ya Familia hiyo ya Waoaji ambao ni Ukoo wa Mahenge kupangiwa vitu hivyo waliondoka na kuahidi kurudi siku nyingine kwa ajili kukamilisha vitu walivyopangiwa ambapo walirudi Septemba 11, Mwaka huu wakiongozwa na Mshenga aliyejulikana kwa jina moja la Mzee Katete wakiwa na Blanketi 2, Mashuka mawili pamoja na Fedha shilingi 10,000/= ambazo walizipokea na kuwaambia hawawezi kuzungumza chochote juu ya Ndoa.

Mjomba huyo anaongeza kuwa baada ya wiki mbili familia hiyo ilirudi na kukuta Nyumbani kuna ukoo mzima wakiwa na Shilingi 200,000/= ndipo walipoambiwa walipe kiingilio shilingi 100,000/= ndiyo wanaweza kupokelewa nyumbani jambo ambalo walilitekeleza kisha kulipa fedha walizokuwa nazo kama Mkaja na kuomba wapewe kibali cha kuandikisha ndoa na taratibu za kumalizia vilivyobaki zikiendelea.

Anasema tangu hapo Ndoa ilianza kutangazwa Disemba 8 na kuisha Disemba 22, Mwaka huu baada ya kutangazwa mara tatu huku tangazo likiashiria ndoa kufungwa tarehe 28/12/2013 ambapo wazazi wakiahidi kumalizia Mahari iliyobaki kabla ya siku ya kufunga ndoa.

Akizungumzia kwa kirefu kashishe hiyo, Mjomba huyo anasema baada ya wazazi wa Mwanaume kusisitiza kumaliza kila kitu hadi ifikapo Disemba 23, Mwaka huu na wao walijikusanya na kupanga taratibu za sherehe hususani ya kumwaga binti yao(Send Off) ambayo ilifanyika Disemba 24, Mwaka huu.

Aidha baadhi ya ndugu wameongeza kuwa familia hiyo haioneshi uaminifu wa kumalizia Mahari hiyo kutokana na ahadi zisizotekelezeka walizotoa tangu kipindi cha nyuma na kuongeza kuwa hata kwenye sherehe ya kumwaga binti yao walifika baadhi ya ndugu wakiwa na Zawadi tofauti na taratibu zinavyotaka.

Wamesema kwa mujibu wa taratibu za Sherehe za SendOff upande wa Mwanaume unatakiwa kuleta zawadi ambazo ni  nguo za Bibi Harusi za kuvaa siku ya Ndoa Pamoja n Harusi lakini wao hawakufanya hivyo ingawa walikuwa na Nguo ambazo tayari zilikuwa zimetumika.

Kwa upande wa Mchungaji aliyekuwa anataka kufingisha Ndoa hiyo ambaye pia ni Askofu wa Kanisa hilo, Mchungaji Kenan Mpalala alipoulizwa kuhusu hali hiyo amesema kwa mujibu wa taratibu za Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 kifungu cha 8 pingamizi litolewe ndani ya siku 21.

Amesema upande wa Wazazi wa Mwanamke ulishindwa kuwasilisha pingamizi lao kanisani kabla ya Siku 21 badala yake walifika kutoa malalamiko kuhusu kutomaliziwa kwa mahali jambo ambalo alisema yeye kama Mwandikisha Ndoa halimhusu bali pande mbili wanatakiwa kulimaliza kabla ya Ndoa.

Naye Bwana Harusi Mtarajiwa Fadhili Mahenge(28) alipoulizwa kuhusiana na suala hilo huku akiwa tayari Kanisani kwa ajili ya Kufungishwa Ndoa alisema anachosubiri ni hatma ya Wazazi wa Mwanamke kama wanaweza kumwachia Mkewe iliwanachodai awe anamalizia taratibu.

Amesema yeye kama yeye kwa sasa hana fedha zozote za kuweza kumalizia anachodaiwa zaidi ya kuomba busara za wazazi wa Mwanamke kumruhusu Ndoa ifungwe ndipo aweze kulipa Mahari anayodaiwa kwa awamu kutokana na hali yake ya kiuchumi kuwa Mbaya.

Ameenda mbali zaidi kwa kusema kama Wazazi wa Mwanamke wataendelea kuwa na Msimamo huo basi hata yeye ataomba arudishiwe kile alichokitoa awali ili ajipange upya kwa ajili ya ndoa baada ya kukamilisha madai yao.



Hadi tunaingia mtamboni Mbeyayetu ambayo ilikuwepo sehemu ya tukio timu ya usuluhishi ilikuwa ikiendelea na kazi yake ikiongozwa na Mchungaji, Mwenyekiti wa Mtaa na Mzee Maarufu ambaye ni Katibu wa Chama cha Wakulima (TASO) kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Ramadhani Kiboko, huku muafaka ukiwa haujapatikana.

Na EZEKIEL KAMANGA, MBEYA.
 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger