Pages


KUNG'OLEWA KWA BENDERA ZA CHADEMA TUNDUMA MKOANI MBEYA KWAZUA TAFLANI.

Kamanga na Matukio | 01:59 | 0 comments

Habari na Ezekiel Kamanga, Tunduma.
Vurugu  zilizotokea katika  mji wa Tunduma wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya  kabla ya kuwasili Makamu wa raisi wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania mheshimiwa Mohammed Gharib Bilali. 

Vurugu hizo zilitokana na watu wasiofahamika kung’oa bendera za Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambapo ilimlazimu Diwani wa Kata ya Tunduma Frenk Mwakajoka  na Mkuu wa kituo cha Polisi Tunduma Bwana A.S.Wendo kuwa na wakati mgumu kuwatuliza vijana hao waliokuwa na mukali  kabla ya Makamu wa Raisi kuwasili eneo hilo kwa ajili ya kuzindua soko la Mji mdogo wa Tunduma lililoungua mwishoni mwa mwaka jana.

Aidha Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa Advocate Nyombi aliwasihi wananchi wa eneo hilo kuwa watulivu na kuwataka  wakazi wa eneo hilo kuondoa bendera zao kwa ajili ya kuheshimu mamlaka kwani kiongozi huyo hana itikadi ya chama chochote na bali anawakilisha Serikali.

Kwamjibu wa wananchi wa eneo  hilo walidai kuwa bendera zao za vyama pinzani kuwa zimeng’olewa bila ridhaa yao.

Hata hivyo sakata hilo lilitulizwa na Mbunge wa Jimbo la Mbozi Magharibi Mheshimiwa David Silinde ambaye naye aliwaasa wananchi kuwa watulivu ili kumsikiliza Makamu wa Rais na kusahau yaliyotokea, ambaye anakuja kwa shughuli za Kiserikali na sio kisiasa na kama kuna tatizo lolote basi ni muda muafaka wa kumuuliza Makamu wa Rais ili kutafutiwa ufumbuzi.
 
Wakati huo huo Silinde ameongeza kuwa  ameweza kufanya mazungumzo na mweshimiwa Dokta Slaa kuhusiana na kutokea kwa tukio hili  hivyo naye amewaomba wananchi wamsikilize Makamu wa Rais ikiwa ni kutoa matatizo yanayowasumbua bila kufanya vurugu zozote. 

Mheshimiwa Makamu wa Rais  Dakta Mohamed Gharib Bilali   kabla ya yote aliwashukuru wananchi  wa Tunduma kwa ujenzi  wa soko hilo  ikiwa ni  kutoa pole kwa watu wote  walioathirika na janga la moto  lililotokea hivi karibuni na kuharibu mali za watu na kwamba Seriakali inaangalia ni namna gani inaweza kuwasaidia waathirika hao.

Aidha Bilali  aliahidi kutoa ushirikiano wa dhati ili  kuwa nusuru wale wote walioathirika na janga  hilo na kuwataka wananchi wa eneo hilo kuwa na hulka ya kuwamini vingozi wao kwakile wanachokizungumza.

Baada ya kuhutubia wananchi hao Makamu wa Raisi alimkaribisha Mbunge Silinde ili kupokea kero zinazowasibu wananchi jimbo lake, ambapo Mbunge huyo amesema kuwa amesisitishwa na maamuzi ya Serikali kusitishwa uandikishwaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza kwa mwaka huu, ambapo alimtaka Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bwana Philip Mulugo kujibu swali hilo.

Kwa upande wake Waziri Mulugo amesema kuanzia siku ya Jumatatu Februari 26 watoto wote wanaostahili kwenda shule waanze masomo mara moja na ifikapo mwezi Aprili atakuja kukagua kama wanafunzi hao wamekwishaanza masomo..
 
Kwa mjibu wa mheshimiwa diwani Frenk Mwakajoka  amesema kuwa tangu Mwaka 2005 wanaupungufu wa vyumba vya madarasa 214, hivyo amemuomba Makamu wa Rais kumuonya Afisa Elimu wa mkoa wa Mbeya Bwana Juma Kaponda kutoendelea kutoa maamuzi ambayo yanawaathiri na kudidimiza elimu mkoani hapa na awe tayari kupokea ushauri  ili kuondoa ujinga.

TAARIFA ZA MAUAJI YA KUCHINJWA RAIA WASIO NA HATIA WILAYANI SONGEA-RUVUMA, FEBRUARI 2012.

Kamanga na Matukio | 01:57 | 0 comments

Wilayani Songea yapata watu wanne(4) wamechinjwa kikatili kwa siku tofauti tofauti na watu wasiofahamika na kwa sababu zisizojulikana fuatilia mtiririko wa matukio haya;-

· Mnamo tarehe kati ya 15 na 16.02.2012 mtu mmoja aliuawa kwa kuchinjwa na kisu katika maeneo ya Ruhwiko Wilayani Songea –Ruvuma.

· Tarehe 20.02.2012 siku ya Jumatatu alichinjwa mtu mwingine kutoka maeneo ya Rizaboni Wilayani Songea-Ruvuma kwa sababu zisizojulikana.

· Tarehe 21.02.2012 alichinjwa mtu mwingine.

· Tarehe 22.02.2012 kijana mmoja Dereva wa Boda Boda wilayani Songea alichinjwa kikatili nyakati za usiku akiwa nyumbani kwake baada ya kuitwa nje na mtu kwa madai ya kuwa kuna mtu anamazungumzo nawe.

Kimsingi matukio hayjo yote yamekuwa yakitokea nyakati za usiku,aidha Jeshi la Polisi Wilayani Songea limekuwa likifanya DORIA usiku pasipo mafanikio kwani matukio ya watu kuuawa bado yanaendelea kufanyika.

Hadi sasa ni watu WANNE(4) wameuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana na watu watano(5) wamejeruhiwa na Jeshi la Polisi leo asubuhi baada ya Jeshi la Polisi kutuliza GHASIA za wananchi wa Wilaya ya Songea wakifanya maandamano kuelekea katika Ofisa za Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa madai ya kuwa kwanini hawaoni jitihada za Serikali katika kudhibiti tatizo hilo,aidha majeruhi hao wamelazwa katika Hospital ya Mkoa

Nami nikiwa Mwanaharakati(Human Rights Deffender-THRD) Tunduru nitaendelea kuwajuza nini kinaendelea juu ya matukio haya.

Aidha naomba wanaharakati(THRDs) wote kufuatilia kwa karibu vyombo vya habari.
Chanzo cha taarifa;THRDs Wilayani Tunduru
Ndg.John Raphael Nginga
TUFAE EDUCATION AIDS TRUST
P.O.BOX 290,Tunduru
Fax;+255 25 2680001/81
Cell:+255 787 523030/765 636161/713 138525

KUFUATIA MAUAJI YA KUTISHA MKOANI RUVUMA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU WALAANI VIKALI VITENDIO HIVYO NA KULITAKA JESHI LA POLISI KULINDA USALAMA WA RAIA.

Kamanga na Matukio | 01:56 | 0 comments

By correspondent Rose Mwalongo
AT LEAST two people were shot to death yesterday with dozens injured following a fracas between angry Wananchi and the police in Songea municipality yesterday. 

The move came following an angry move taking on the street to boycott over what they said failure by the police to contain a new wave of killings that has seen six people butchered in recent days. 

Earlier on, the Guardian received reports from a human rights monitor in the region who said 4 people had their heads chopped by unknown people between February 15th and 17th, 20th, 21st and 22nd this year respectively.
A human rights monitor with the Legal and Human Rights Centre (LHRC) in the area whose name can not revealed for security reasons told the Guardian yesterday. 

“At least 4 people have been slaughtered within different days by unknown people on unfounded reasons. Between February 15th and 16th, this year a person whose name could not be established was slaughtered with a knife at Ruwhiko, in Songea district. Another incident took place on February 20th at Rizaboni where yet another innocent person was terminated in a similar manner. Worse still on February 21st, yet another person was butchered and not to mention of February 22nd where a BodaBoda driver was slaughtered in Songea district,” said the monitor. 

According to him, the Boda Boda driver was called outside from his house at night on account that someone needed to talk to him but never came back as he was slaughtered within the same night.
He said yesterday, people around the Songea municipality took to the street saying he had seen at least 5 people who had been shot and injured when police officers in Songea dispersed an angry mob which was marching yesterday morning on what they said failure by the police to curb the killings.
Those shot were admitted at the Songea Region Hospital for treatment.
 
In an immediate rejoinder yesterday, the Ruvuma Regional Police Commander (RPC) Michael
 
Kamuhanda told the Guardian that at least six people had been killed in Songea with some having their parts chopped due to witchcraft beliefs while some have been killed due to love. 

According to the RPC, the killings took place between November 28th to February this year. 

“ At least three women were killed due to love while as the rest were burnt to death with some having their body parts chopped off due to superstitious beliefs. There is a new wave of such beliefs in the area with some perceiving that the body parts can be used in mining as a concoction to strike a deal,” said the RPC.
In another move, the RPC said at least two people were shot to death when police officers attempted to restore order following the rioting. He however said he could not establish the number of those injured as he was in a meeting over the same issue promising to give a detailed report there after. 

“ I am in a meeting now but what I can tell you is the situation was not good at all as an angry mob went on the street rampaging business premises, burning tires, invading offices, banks and even police
stations and the police had to use efforts to calm them. Currently the situation is calm but am in a meeting to ponder over the issue,” said the RPC while requesting this reporter to call him back later on. 

ENDS

Tunamshukuru Mungu kwa siku ya leo,kwani hadi tumeamka kwa siku ya leo Mkoani Ruvuma hakuna mauaji yaliyofanyika ukilinganisha na siku chache zilizopita ambayo yalisababisha wananchi wa Wilaya ya Songea kuandamana hapo jana tarehe 22.02.2012 baada ya mauaji ya kikatili ya kuchinjwa raia wanne(4) wasio na hatia kwa siku kadhaa mfululizo.

Kimsingi tunazidi kulishauri jeshi la Polisi kuimarisha ulinzikwa RAIA wake mkoani Ruvuma kwani wananchi wengi sasa wanaishi kwa mashaka na sikweli kwamba kikosi kinachofanya mauaji hayo hakijulikani au inashindikana kufanya utafiti wa kina katika kuwatambua wahalifu hao.

Sisi wananchi wa Tanzania tunaamini kwamba jeshi letu la Tanzania lina wataalam wengi wa kutosha na kwa mbinu ya ULINZI SHIRIKISHI si jambo la kuweza jeshi la polisi kushindwa,aidha kama Askari hawana ushirikiano mzuri na jeshi la Polisi haya yanaweza kuendelea kufanyika.

Taarifa za majeruhi waliolazwa jana hadi jioni walifikia 40 na RAIA wawili WALIKUFA baada ya askari POLISI kuwapiga risasi katika harakati za kutuliza ghasia kutokana na maandamano yaliyofanyika jana.Aidha hakuna mgonjwa yeyote aliyekufa kati ya wale WALIOLAZWA jana.

Hiyo ndiyo hali halisi ya matokeo ya TAFRANI za jana Mkoani Ruvuma.
Aidha nitaendelea kuwajuza wanaharakati na watetezi wa haki za Binadam nchini.

THRDs na Mwangalizi wa Haki za Binadamu Tunduru kupitia LHRC
BY NGINGA THRD
Onesmo  Paul Kasale Olengurumwa,
Coordinator Tanzania Human Rights Defenders Coalition
Lega and Human Rights Centre

Justice  Lugangira  House, Kijitonyama. P.O.BOX 75254,Dar es Salaam ,Tanzania. TEL +25522 2773038/48 FAX +255 222773037 mobile +255 717-082228/08783-172394


“Marriage is not about finding the right person. It’s about becoming the right person. Many people feel they married the wrong person, but I’ve learned that it’s truly about growing to become a better husband.”

MKUU WA MKOA WA MBEYA, ABBAS KANDORO AMEWATAKA WAKULIMA MKOANI HUMO KUANDAA VEMA MAZAO YAO KWA KUYASINDIKA

Kamanga na Matukio | 01:52 | 0 comments

Habari na Angelika Sulusi, Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro amewataka wakulima Mkoani humo kuandaa vema mazao yao kwa kuyasindika na kufungasha vizuri ili waweze kupanua soko lao kwa bidhaa zao kuuzwa ndani na nje ya nchi.

Kandoro amesema hayo leo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wajasiriamali wadogo wanaojihusisha na usindikaji na uuzaji wa mazao ya kilimo, yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa wajasiliamali kutoka Wilaya zote za Mkoa huo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Benjamini Mkapa.

Amesema kuwa wakulima wengi nchini wanauza mazao yao kwa bei ndogo kutokana na kutoyaanda vizuri kwa uyasindika na kuyafungasha vema, hali inayochangia wakose soko la uhakika  pia kuyauza kwa bei ya chini.
Amesema kuwa jitihada za makusudi zinatakiwa kumkwamua mkulima wa Tanzania kwa kumpatia elimu ya ujasiriamali katika uandaaji na fungashaji wa mazao ili aweze kupata bei nzuri hivyo kumudu ushindani wa soko.

Kwa upande wake,Mwakilishi wa Mkurugenzi wa TBS, Agnes Mneney amesema kuwa Shirika hilo limeamua kutumia fedha zake za ndani ili kuwafundisha wajasiriamali kuhusu ubora wa viwango vya mazao ya kilimo na matakwa ya masoko ya nje ili wakulima waweze kunufaika na mazao yao.

MBABE WA KIJIJI AUAWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 03:42 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mtu mmoja maefariki dunai mkoani Mbeya baada ya kupingwa na wananchi wenye hasira kali wakimtuhumu kuwanyanyasa wananchi wa kijiji cha Halambo Kata ya Halungu wilaya ya Mbozi mkoani hapa.

Tukio hilo limetokea kijijini hapo ambapo wananchi hao walimpiga hadi kumuua mkazi huyo aliyefahamika kwa jina la Imani Msinjili (23), kwa madai kuwa marehemu akilewa huwapiga wananchi hao na kuwaletea vurugu kubwa hali waliiona ni bughudha kwao.

Imeelezwa kuwa majira ya saa tano asubuhi marehemu Msinjili alikuwa amelewa na kisha kuwapiga baadhi ya wananchi ndipo walipomkamata na kuanza kumpiga mpaka pale mauti yake yalipomfika katika eneo hilo la kilabu cha pombe alipokuwa marehemu akinywa.

Hata hivyo Jeshi la Polisi halikuweza kufika eneo la tukio mpaka jana Februari 23, mwaka licha ya kupewa taarifa na maiti iliendelea kuwepoeneo hilo.

Mwandishi wetu alipofanya jitihada za kumtafuta Kamanda wa Jeshi la Polisi Advocate Nyombi ili aweze kuthibitisha taarifa za tukio hilo hakuweza kupatikana mara moja.

Aidha kumekuwepo na tabia za baadhi ya wananchi mkoani hapa kuendelea na tabia za kujichukulia sheria mkononi licha ya Jeshi la Polisi na Viongozi wa madhehebu mbalimbali kuendelea kukemea vitendo hivyo viovu vinavyokiuka haki za binadamu.

Wakati huohuo wafanyabiashara wa Kijiji cha Mlowo bado wameendelea na mgomo wa kutolipa ushuru wa biashara na mazao wakidai wanahitaji kuonana na Mkuu wa wilaya ya Mbozi Mheshimiwa Gabriel Kimoro.

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DOKTA MOHAMED GHARIB BILAL KUWASILI MKOANI MBEYA LEO.

Kamanga na Matukio | 03:41 | 0 comments
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya kitabu cha mtafiti bingwa duniani wa Masokwe, Jane Goodall, aliyefika Ikulu ndogo ya Wlaya ya Mpanda mkoa wa Katavi jana kwa ajili ya mazungumzo. Jane amekaa nchini kwa miaka 50 akifanya utafiti katika mapori ya Gombe na Mahale yaliyopo mkoa wa Kigoma na Katavi.
******
Habari na Mwandishi wetu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Mohamed Gharib Bilal anatarajia kuwasili Jijini Mbeya leo kwa ziara ya siku tatu ambapo jumla ya miradi minane itafunguliwa.

Akiongea na waandishi wa habari ofisi kwake mkuu wa mkoa wa Mbeya Abasi Kandoro amesema Dokta Bilal anatarajiwa kuwasili Jijini hapa mapema siku ya Ijumaa akitokea Mkoani Rukwa ambapo atatembelea Wilaya za Mbozi, Mbarali, Rungwe na Wilaya ya Mbeya.

Akiwa mkoani hapa Dokta Bilali atafungua soko la wafanyabiashara Tunduma, kutembelea shule ya sekondari Vwawa ambapo atazindua rasmi matumizi ya Teknolojia ya maabara rafiki na kuzindua ofisi ya CCM eneo la Mlowo.

Aidha ataweka jiwe la msingi katika jengo la Saccos ya UWAMU iliyopo eneo la Uyole, kufungua kituo cha mafunzo ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Simambwe Mbeya Vijijini, pamoja na kuweka jiwe la msingi katika hosteli ya Jiji iliyopo eneo la Sokomatola.

Akiwa wilayani Mbarali atakagua miradi miwili ya ujenzi wa bwawa la umwagiliaji pamoja na ujenzi wa soko la mpunga katika eneo la Igurusi, wilayani Rungwe atafungua ofisi ya Muungano wa wakulima wadogo wadogo wa Chai wilayani humo, kufungua mradi wa umwagiliaji na kutembelea shamba darasa katika vijiji vya Kisegese Kasyabone.

MAHAKAMA YA MKOA WA MBEYA IMEWAACHIA HURU WATU WAWILI WALIOKUWA WAKITUHUMIWA NA WIZI WA NYAYA ZA UMEME (TANESCO).

Kamanga na Matukio | 03:40 | 0 comments
Habari na Mwandishi wetu.
Mahakama ya mkoa wa Mbeya imewaachia huru Sadiki Mbango mkazi wa Air Port jijini Mbeya na Ibrahim Mponzi mkazi wa Chimala wilayani Mbarali ambao walikuwa wakituhumiwa na kosa wizi wa nyaya za umeme mali ya shirikala umeme nchini (TANESCO) zenye thamani shilingi milioni 16 laki saba ishirini na saba elfu mia tisa hamsini na nane.

Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Venasi Mlingi amesema mahakama inawaachia huru watuhumiwa hao baada ya ushahidi uliotolewa na TANESCO pamoja na shahidi aliyeandaliwa kutoa maelezo yanayotofautiana, jambo ambalo limeipelekea mahakama hiyo kuwaona watuhumiwa hao hawana hatia.

Aidha Katika mahakama ya mwanzo Mbalizi Richadi Mkwasa mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa Songwe viwandani amefikishwa katika mahakama hiyo kwa kosa la wizi.

Hakimu wa mahakama hiyo Jonasi Mwakyusa amesema mshatikiwa anatuhumiwa na kesi ya wizi wa kuvunja kisha kuiba mali zenye thamani ya shilingi milioni moja mali ya Frola Mwakyusa.

Mshtakiwa amekana shitaka linalomkabiliri na amerudishwa rumande kwa kukosa dhamana ya shilingi laki tano na kwamba kesi hiyo itasomwa tena machi mosi mwaka huu.

TUCTA MKOANI MBEYA LAPATA VIONGOZI WAPYA.

Kamanga na Matukio | 03:38 | 0 comments
Habari na Mwandishi wetu
Shirikisho la vyama huru vya wafanyakazi TUCTA mkoani Mbeya limepata viongozi wapya watakaoongoza kwa miaka mitano ijayo.

Viongozi hao wamepatikana kufuatia uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Wafanyakazi kilichopo Mwanjelwa jijini Mbeya chini ya usimamizi wa katibu mkuu wa TUCTA bwana NICHOLOUS MGAYA.

Katika uchaguzi huo Alinanuswe Mwakapala ametetea nafasi yake na kuendelea kuwa mwenyekiti wa shirikisho hilo ngazi ya mkoa na Thomas Kasombe akachaguliwa kuwa katibu.

Mwakilishi wafanyakazi wanawake Peles Lugala, Mwakilishi wa vijana Nasra Nasoro na Willium Barton akachaguliwa kuwa mwakilishi wa wafanyakazi walio na ulemavu.

Awali katibu mkuu Mgaya aliwataka viongozi waliochaguliwa kutambua kuwa nafasi walizopewa zinatokana na kuaminiwa na wafanyakazi kuwa wanao uwezo wa kuwaongoza hivyo wana wajibu wa kuhakikisha wanajituma katikaa utendaji kazi wao.

WANANCHI WAANZA UJENZI WA SHULE YA MSINGI KWA LENGO LA KUPUNGUZA UTORO KWA WANAFUNZI - CHUNYA MKOANI MBEYA.

Kamanga na Matukio | 03:57 | 0 comments

Habari na Mwandishi wetu
Wananchi wa kata ya Sangambi wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wameanza ujenzi wa shule ya msingi katika kijiji cha Izumbi ili kupunguza tatizo la utoro kwa wanafunzi.

Akiongea na mtandao huu Afisa mtendaji wa kata hiyo bwana Ongara Daudi amesema wameamua kujenga shule kijijini hapo kwa sababu wanafunzi wengi wamekuwa hawahudhurii masomo kwa sababu ya umbali wa shule iliyopo sasa

Aidha Daudi ameongeza kuwa wanakijiji wengi wamepata hamasa na kuonyesha juhudi ili kukamilisha ujenzi wa shule hiyo pia ameiomba serikali kuwaunga mkono wanakijiji ili kukamilisha malengo yao.

Hata hivyo amesema uhamasishaji wa ujenzi huo unalengo la kufuta ujinga kwa kizazi cha sasa na kijacho kujikomboa kielimu na kupunguza wimbi la idadi kubwa ya watu wasiojua kusoma na kuandika wilayani humo.

WATU WAWILI WAFARIKI KWA AJALI YA PIKIPIKI, WAWILI WAJERUHIWA KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 03:55 | 0 comments

 Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Watu wawili wamefariki dunia  Mkoani Mbeya, wakiwemo wawili waliokuwa wamepakizana watu watatu katika pikipiki moja maarufu kama mishikaki na kuanguka barabara ya Mbeya/Iringa, FebruarI  21 majira ya saa Tatu usiku.

 Ajali hiyo imetokea  maeneo ya Mabadaga wilaya ya Mbarali ambapo dereva  aitwae  Kilubai  Kisota (44) mkazi wa Matebete akiendesha pikipiki yenye namba za usajiri T 971 BVU ilisababisha kifo chake na abiria aitwae Amina (25) mkazi wa Ilemi jijini MBEYA

Pia ajali hiyo ilisababisha majeruhi kwa abiria mwingine aitwae  Michael Kisota (26) ambaye amelazwa katika hospitali ya Chimala Missioni  na hali yake inaendelea vizuri pia miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali hiyo.

 Hata hivyo chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi ambapo dereva alishindwa kuimudu pikipiki hiyo.

Aidha majira ya saa 2;30 usiku Februari  21 eneo la Mlowo wilaya ya Mbozi  mtu mmoja aitwae Hakimu Pendo (32) mkazi wa eneo hilo alipigwa na kunyang’anywa pikipiki yake na watu wasiofahamika

Mbinu iliyotumika na watu hao kukodi pikipiki  kwenda Mlowo ndipo walipofika eneo hili walimpiga na kunyang’anya pikipiki hiyo

Pendo amelazwa  katika hospitali ya Mbozi Mission ambapo Jeshi la Polisi  wanafanya msako mkali ili kubaini waliohusika ingawa namba na aina ya pikipiki haijulikani kwa mjibu wa Kamanda wa Jeshi hilo Advocate Nyombi .

JAMII YATAKIWA KUTOWATENGA NA KUWAFICHA WATOTO WALEMAVU.

Kamanga na Matukio | 03:53 | 0 comments

Habari na Mwandishi wetu.
Mkurugenzi wa taasisi ya kusaidia watoto walemavu Child Support tanzania iliyopo Block T jijini Mbeya  Bi Noela Msuya ametoa wito kwa jamii kutowatenga na kuwaficha watoto wenye ulemavu.

Hayo yamesemwa na Bi Msuya alipokuwa akiongea na mwandishi wetu ofisini kwake amesema jamii inatakiwa kuwashirikisha na kuwawezesha walemavu katika mambo mbalimbali ya maendeleo katika jamii

Aidha ameongeza kuwa watoto walemavu ni sawa na watoto wengine na wana uwezo ,vipaji pia jamii inatakiwa kuviendeleza vipaji ili wasije kuwa tegemezi kwa maisha ya baadae.

WATU WATANO WAFARIKI KATIKA MATUKIO MATATU TOFAUTI MKOANI MBEYA

Kamanga na Matukio | 03:21 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Watu watano wamefariki dunia katika matukio matano tofauti, yakiwemo matatu yanayohusishwa na ajali za barabarani mkoani Mbeya.

Kamanda  wa polisi mkoani mbeya Advocate Nyombi  amesema Benardi Bakinga  (32),  mkazi wa Ilomba  Jijini Mbeya ameuwawa na wananchi wenye hasira kali wakimtuhumu kujihusha na wizi.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hosipitali ya Rufaa jijini hapa na mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo .

Aidha Nyombi ameongeza kuwa tukio jingine lili tokea katika kijiji cha Masebe wilayani Rungwe ambapo Helodi Mwakesesya (56) mkazi wa kijiji hicho ameuwawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kumtuhumu marehemu kujihusisha na imani za kishirikina.

Jeshi lapolisi linawashikilia watu wawili ambao ni Zacharia Mwauibinga (30) na Zaward Emmanuel (30) wote wakiwa  wakazi wa kijiji cha Masebe ambapo wanatuhumiwa kutenda kosa hilo majira ya saa tano usiku Februari 20 mwaka huu.

Chanzo cha mauaji hayo ni kile kilichodaiwa marehemu alikuwa akijihusisha na imani za kishirikina na kabla ya kufanya mauaji hayo nyumba ya marehemu ilichomwa  na moto.

Kamanda Nyombi ameongeza kuwa Essau Kiswaga (22) amefariki baada ya gari aina ya pikipiki yenye namba za usjili T255 APR kupinduka na kusababisha kifo chake  tukio hilo lilitokea Februari 20  katika barabara ya Mbeya - Iringa ambapo gari hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva aitwaye Deodatusi Neumwa (36)  ambaye ni mkazi wa  Mafinga na kupinduka katika kijiji cha Uinyagogwa huko Madibila wilayani  Mbarali.

Chazo cha ajali hiyo kimetajwa kuwa ni mwendokasi na Jeshi la Polisi  linamshikilia dereva wa gari hiyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Na katika tukio lingine jijini Mbeya  katika eneo la Mwanji barabara ya Mbeya - Iringa gari lenye namba za usajili  T 642 AED Toyota Hiace  lililokuwa likiendeswa na dereva aitwaye Laightoni Frolence  (25) mkazi wa Ilomba jijini Mbeya ilimgonga mpanda pikipiki yenye namba za usajili T 127 BUV  aitwaye Tidibows  Mwakatowe  (30)  na kusababisha kifo chake  papo hapo na abiria wake KERVINI NDONDE mkazi wa ILOMBA jijini hapa kupatwa majeraha .

Mwili wa mrehemu umehifadhiwa kastika  Hospitali ya Rufaa jijini hapa na majeruhi wote wamelazwa katika hospitali hiyo kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa gari na pikipiki  vyombo hivyo vipo katika kituo cha polisi jijni humo 

Wakati huo huo Geophrey Mwankenja amefariki dunia baada ya kugongana uso kwa uso na gari aina ya Hiaceakiwa kwenye pikipiki na abiria aitwaye Njala Mwankulu  ambaye aliyelazwa katika hosipitali hiyo.

Ajali hiyo imetokea baada ya pikipiki hiyo   kujalibu kuli pita basi la FALCON  majira ya saa kumi  za jioni  na hivyo kukutana uso kwa  uso na HIACE   na kufariki papo hapo.

WAFANYABIASHARA WA MLOWO MKOANI MBEYA WAGOMA KULIPA USHURU.

Kamanga na Matukio | 03:18 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Wafanyabiashara kutoka mji mdogo wa Mlowo, wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya bado wameendelea na msimamo wao wa kugoma kulipa ushuru wa soko na mazao kwa halmashauri ya wilaya hiyo kutokana na mazimio yaliyofanywa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika  siku ya alhamisi  Februari 16 mwaka huu katika mji huo.

Kukosekana kwa huduma za choo na kusanyiko wa takataka wa muda mrefu bila kuzolewani sababu zilizochangia wafanyabiashara hao kugoma kulipa ushuru, licha ya kuwepo kwa makusanyo ya kila siku kutoka kwa wafanyabiashara hao na ushuru hutozwa  kutokana na mazao yanayosafirishwa kutoka wilayani humo.

Kufatia mgomo huo uongozi wa wa halmashauri hiyo umeamua kuitisha kikao  cha dharula ili kupata mustakabali wa suala hili ambao limeendelea kuikosesha halmashauri ya wilaya ya Mbozi mapato yake yanayotokana na vyanzo hivyo.

Katika mkutano huo mkuu wa wilaya hiyo Mheshimiwa Gabrel Kimoro alialikwa kuhudhuria ambapo uchunguzi umebaini mara kadhaa amekuwa akialikwa na bila kuhudhuria, hali ambayo ilichangia kuwa moja ya ajenda ambapo wengi wamelalamikia katika mkutano huo uliohudhuriwa na wananchi zaidi ya mia nne wa mji wa Mlowo.

Wakati huo huo sakata la Shule ya msingi Ichenjezwa kukataa kuandikisha wanafunzi wa darasa la kwanza imechukua sura mpya baada ya watoo watatu kuandikishwa darasa la pili na kuanza masomo huku watoto wengine wakikataliwa uchunguzi huo umebainiwa .

MTU MMOJA AKUTWA AKIWA AMEKUFA CHUMBANI KWAKE JIJINI JIJINI MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:23 | 0 comments

   Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Rashid Mtila (35), mkazi wa Kata ya Manga jijini Mbeya amekutwa amefariki chumbani kwake.

Mwili wa marehemu umegunduliwa na watu wawili waliokuwa wakienda kupata pombe za kienyeji katika moja ya nyumba iliyopo katika eneo hilo maarufu kama Jua Kali  Mwanjelwa, majira ya saa sita mchana Februari 19 siku ya jumapili.

Kwamujibu wa Balozi wa mtaa huo Bwana Godwini Kitwika alitoa taarifa kwa Diwani wa kata hiyo ya Manga mheshimiwa  Daniel Mwakisyala ambapo alitoa taarifa katika kituo cha polisi cha Mwanjelwa.

Pia marehemu alikuwa akiishi peke yake na siku mbili zilizopita na alianguka hivi karibuni katika kituo cha mabasi cha Mwanjelwa kwa kile kilichodhaniwa kuwa ni ugonjwa wa kifafa na siku hiyo alianguka mara tatu hali iliyomlazimu kwenda kupumzika chumbani kwake.

Hivyo kutokana na ukata wa maisha vijana wa mtaa huo walipitisha mchango wa dharura kwa ajili yakupata shuka ili kumuhifadhia marehemu huyo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Advocate  Nyombi ameruhusu mwili wa marehemu kuchukuliwa na ndugu zake kwa ajili ya mazishi.

RAIS JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA NA KUKAGUA SHAMBA LAKE LA MANYASI YA MIFUGO-MSOGA

Kamanga na Matukio | 05:19 | 0 comments
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa shambani kwake Msoga, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani leo. Shamba hilo ni la manyasi ya kulishia mifugo kwa njia ya kisasa (zero grazing), akiwa ni mmoja wa wafugaji kijijini hapo. Rais Kikwete, ambaye aghalabu hutumia muda wake wa likizo shambani kwake, pia analima mananasi ambayo hustawi vizuri katika wilaya hiyo. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mh Mwantumu Mahiza.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa shambani kwako Msoga, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani. Shamba hilo ni la manyasi ya kulishia mifugo.
PICHA NA IKULU.

NAPE AHUDHURIA IBADA KATIKA KANISA LA UFUFUO NA UZIMA KAWE

Kamanga na Matukio | 05:17 | 0 comments

Katibu wa NEC ya CCM Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akipongezwa na Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, baada ya kutoa mahubiri yake katika kipindi cha ‘Hekima za Viongozi’ alipohudhuria ibada ya Kanisa hilo jana kwenye Viwanja vya kilichokuwa kiwanda cha kusindika
nyama cha Tanganyika Packers, Kawe mjini Dar es Salaam. Nape alihudhuria ibada hiyo kutokana na mwaliko wa kanisa hilo.
(Na Mpiga picha Wetu).

WAGANGA WA JADI WAPINGA VITENDO VYA UOVU JIJINI MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:15 | 0 comments

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Waganga wa jadi na tiba asilia mkoani Mbeya  wamelitaka Jeshi la Polisi kutoa ushirikiano na watabibu wa asili  ili kukomesha vitendo  vya uovu  vinavyohusishwa na imani za kishirikina.

Hayo yamebainishwa na watabibu wa tiba asilia na tiba mbadala katika mkutano ulio fanyikia katika ukumbi wa Shamba la Bibi uliopo katika eneo la Sokomatora  Jijini Mbeya

Mwenyekiti wa mkutano huo Bwana Boniventura  Mwalongo uliohusisha vyama vya ATME, MJATA ,CHAWATATA , na CHAUMUTA vinavyohusika na tiba asilia hizo amesema tiba zao zimekuwa zikihusishwa na imani za kishirikina kwa kuchochea vitendo vya upigaji nondo, mauaji ya maalbino(walemavu wa ngozi) na ubakaji ambapo asasi hizo hazija kanusha hadharani kutokana na baadhi ya watu kuvamia fani hiyo kwa nia ya kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.

Katika mkutano huo vyama hivyo vimeadhimia kupunguza vitendo vyote vya uovu vinavyofanywa na baadhi ya watu waliovamia fani hiyo kutoka nje ya nchi kwa kushirikiana na wa watanzania wasiosajiliwa wala kuwa na leseni ya kufanyia kazi hiyo.

Aidha wamelitaka Jeshi la Polisi kuwafichua hadharani wale wote wanaohusika na vitendo hivyo kwani wamekuwa wakifumbia macho licha ya kutajwa baadhi ya vigogo ambao ndio wenye mtandao huo.

Pia matabibu hao wa asili wamepiga vita marufuku matangazo yote ambayo hayana stahara katika vituo vya redio na matangazo yote yanayotoa matangazo yote yanayotangaza kuondolewa mara moja.

JK AFUNGUA MKUTANO WA MAWAZIRI WA KILIMO JIJINI DAR ES SALAAM .

Kamanga na Matukio | 05:34 | 0 comments
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa Mawaziri wa Kilimo toka nchi saba za Afrika hapo jana February 17, 2012 katika hoteli ya Kilimanjaro Hyatt jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete akiongea na Mawaziri wa kilimo wa nchi saba za Afrika baada ya kufungua mkutano hapo jana February 17, 2012 katika hoteli ya Kilimanjaro Hyatt jijini Dar es salaam. Nyuma ya Rais Kikwete ni kamishna wa Maendeleo vijijni na Kilimo wa Umoja wa Afrika Bi. Rhoda Tumussime.(PICHA NA IKULU).

MWENYEKITI WA MTAA AMTAPELI MFIWA SHILINGI 5,000/= AJIHAMI KWA KUWASHITAKI VIJANA WALIOCHIMBA KABURI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:05 | 0 comments

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Kaimu mwenyekiti wa mtaa wa Ivwanga katika Kata ya Iwambi Jijini Mbeya amejikuta kuingia matatani baada ya kumtoza mfiwa jumla ya shilingi elfu tano kwa ajili  ya vijana wa mtaa huo wa Ivwanga kwa ajili ya kuchimbia kaburi.

Mwenyekiti huyo anayejulikana kwa jina la Nicholousi Njoua amedaiwa kujipatia shilingi elfu tano kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa mchungaji Amoni Mahava aliye fiwa na mwanaye Februari 4 na kuzikwa Februari 7 mwaka huu katika makaburi ya Iwambi jijini hapa.

Katika siku ya mazishi Njoua alimtaka mchungaji kulipa shilingi elfu tano kwa ajili ya vijana waliokuwa wakichimba kaburi kitu ambacho si kweli kwani mwenyekiti huyo alizichukua na kuziweka mfukoni mwake hali iliyopelekea  iliyopelekea kuwaudhi vijana wa mtaa huo mara kadhaa aliendelea kumbugudhi mfiwa akimtaka  atoe pesa hizo vinginevyo vijana wasingechimba kaburi.

Baada ya mchungaji Mahava kukerwa na kauli  za Njoua  aliamua kulipa pesa hizo na kuamua ndugu wawapelekee vijana wanaochimba kabuli na kufanya mgomo ndipo ndugu walikuta kaburi limemalizika mapema walishangazawa na kauli ya mwenyekiti  hivyo ndipo walipo mwamuru azirejeshe mara moja kutokana na amri ya mfiwa na akafanya hivyo.

Kutokana na hali hiyo Nichalous Njoua hakutokea tena katika  msibani badala yake Februari 8 aliamua kuwafungulia mashitaka katika baraza la kata ya Iwambi akidai kuwa baadhi ya vijana wameleta fujo makaburini ambao ni Ibu Gibsoni,Juma Mwanzalizya,Ezekieli  Anangisye ,Osward Mwaka Swala ,Zainabu Mjaliwa Omali Wanga Na Mama Doto ambao walifikishwa katika baraza la kata ya Iwambi Februari 10 na kusomewa shitaka hilo.

Katika hali ya  kushangaza Njoua na mtendaji wa mtaa Jacobu Sanga  hawakutokea barazani ndipo waliamriwa kufika Februari 14  mwaka huu walipofika siku  hiyo mwenyekiti Njoua hakufika badala yake  mtendaji alidai suala hilo limefutwa  hivyo vijana hao wapo huru jambo lililowaudhi vijana hao waliosindikizwa na wenzao 8 na kuomba kuandika barua ya hakimu au mwenendo wa shauri lao na baraza kukataa katakata ombi la vijana hao.

Alipoulizwa mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji  Juma Iddi amesema kuwa halmashuri yake haina utaratibu wa kumtoza mfiwa pesa kwa ajili ya kuchimba kaburi inao utaratibu wa kutoza katika makaburi ya sabasaba na maeneo mengine hayatozwi malipo yoyote

Pia mkurugenzi huyo ameongeza kuwa suala hilo atalifuatilia ili kujua mwenyekiti alipataje jukumu la kutoza pesa bila stakabadhi kama yalikuwa malipo halali  kwani pesa zote za halimashuri hutolewa stakabadhi.

LAWAMA- JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LAWAMANI KUHUSIKA NA KIFO CHA MWANACHUO, MMOJA AFUFUKA BAADA YA KUFARIKI .

Kamanga na Matukio | 05:02 | 0 comments
 Marehemu Daniel  Godluck Mwakyusa (31) ambaye ni mwanafunzi wa chuo cha TEKU  aliyeuawa na Askari wa Jeshi la Polisi PC Maduhu tarehe 14/02/2012 katika sikukuu  ya wapendanao {valentine day].
 Baadhi ya majeraha ya majeraha yaliyotokana na kipigo katika mwili wa marehemu Daniel  Godluck Mwakyusa (31) ambaye ni mwanafunzi wa chuo hicho  aliuawa na Askari wa Jeshi la Polisi PC Maduhu tarehe 14/02/2012 katika sikukuu  ya wapendanao {valentine day].
 Baadhi ya majeraha yaliyoyokana na kipigo atika mwili wa marehemu Daniel  Godluck Mwakyusa (31) ambaye ni mwanafunzi wa chuo hicho  aliuawa na Askari wa Jeshi la Polisi PC Maduhu tarehe 14/02/2012 katika sikukuu  ya wapendanao {valentine day].
******
 Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Watu watatu wamefariki dunia mkoani MBEYA katika matukio matatu tofauti, likiwemo la tukio la Mwanafunzi wa chuo kikuu cha TEKU kilichopo jijini mbeya marehemu Daniel  Godluck Mwakyusa (31) ambaye ni mwanafunzi wa chuo hicho  aliuawa na Askari wa Jeshi la Polisi PC Maduhu tarehe 14/02/2012 katika sikukuu  ya wapendanao {valentine day].

 Marehemu akiwa na wenzake wanne walikuwa katika matembezi ambapo polisi walikuwa doria walikuta vijana hao wakipata vinywaji ndipo waliwatuhumu kuwa ni majambazi ambapo PC Maduhu alimpiga marehemu risasi mbili kwa kutumia bunduki aina ya [SMG].

Pia marehemu aliporwa shilingi laki tatu pamoja na simu ya mkononi .

Kwa mujibu wa baba mzazi wa marehemu huyo  Bwana Pastory Mwakyusa amesema kuwa anasikitishwa sana na kitendo hicho  kilichotokea kwani mwanawe hakuwa na tabia ya wizi au ujambazi  hivyo ameliomba Jeshi la Polisi kueleza sababu ya kumuua mtoto wake.

Hata hivyo Jeshi la Polisi lilitoa usafiri wa gari lenye nambari za usajili T 138 AFK aina ya Coster kwa ajili ya kusafirisha Mwili wa marehemu kwenda katika wilaya ya Kyela kwa ajili ya mazishi baada ya uchunguzi wa  daktari kuthibitisha kuwa marehemu ameuwawa kwa risasi.

Tukio la pili marehemu Zuberi Mwajeleba (21) mkazi wa kijiji cha Ibumba wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya ambaye  alinyongwa kisha mwili wake kutupwa katika mto wa Kanyegele wilayani humo.

 Kamanda wa polisi mkoani Mbeya  Advocate  Nyombi amesema chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika na Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo.

Katika tukio la tatu limetokea majira ya saa nane mchana katika eneo la Ilomba jijini Mbeya ambapo pikipiki yenye namba za usajili T 834 BOX aina ya Shinray ambayo dereva wake bado hajafahika alimgonga mtoto Mildred Immanuel (10) mkazi wa eneo hilo.

Hata hivyo dereva alitoroka na kuitelekeza pikipiki katika eneo la tukio na pikipiki hiyo imehifadhiwa katika Kituo cha kati cha Jeshi la Polisi, na  mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Jijini Mbeya  na Polisi wanafanya juhudi za kumtafuta dereva  huyo.

HABARI YA KUFUFUKA.
Wakati huo huo katika hali isiokuwa ya kawaida Roza  Simbeye ambaye ni mama wa mtoto mmoja katika kitongoji cha Isandula, kijiji cha Vuwile, Kata ya Isandula, aliyefariki  Februari 16 majira ya saa kumi na mbili za jioni amefufuka wakati taratibu zote za mazishi zipokamilika  kama kuchimba kaburi na kuchonga jeneza na taratibu za ibada.

Na ilipofika majira ya saa 3:30 asubuhi ya Februari 17 baada ya kaburi kuchimbwa na jeneza kukamilika zilianza taratibu za kuchukua mwili wa marehemu Roza  chumbani ndipo watu waliopewa jukumu la kumwosha walishangaa kumwona marehemu akiwa hai huku akiwa amtoa macho kama vile mtu ametoka usingizini ambapo mpaka sasa kaburi halijafukiwa  wala jeneza halijatumiwa na kufanya wanakijiji kubaki na mshangao.
 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger