Pages


MAKAMU WA RAIS DKT BILAL KATIKA SEMINA YA KUBADILISHANA UZOEFU NA TAASISI YA MAZINGIRA YA STOCKHOLM

Kamanga na Matukio | 04:26 | 0 comments
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mama Asha Bilal, Waziri wa Mazingira Huvisa, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Taasisi ya Mazingira ya Stockholm, John Kuylenstierna, wakati wakiwa katika semina ya kubadilishana uzoefu kati ya taasisi hiyo na Wizara ya Mazingira iliyo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais. Semina hiyo ilifanyika jana katika ofisi za taasisi hizo zilizopo Stockholm nchini Sweden.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mama Asha Bilal, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Mazingira ya Stockholm, baada ya kumalizika kwa semina ya kubadilishana uzoefu kati ya taasisi hiyo na Wizara ya Mazingira iliyo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais, iliyofanyika jana septemba 27 katika ofisi za taasisi hizo zilizopo Stockholm nchini Sweden.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mama Asha Bilal, wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Muhammed Mwinyi Mzale na baadhi ya mabalozi wa nchi mbalimbali baada ya hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na Balozi wa Tanzania, Sweden jana Septemba 27. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Askari Polisi Aliyeuwawa Kwa Kupigwa Nondo MkoanI Mbeya Aagwa..

Kamanga na Matukio | 04:25 | 0 comments
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Evance Balama akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa askari Polisi PC Meshack Urasa ambaye aliuawa kwa kupigwa na nondo juzi Jijini Mbeya. Mwili wa marehemu ulisafirishwa leo kwenda nyumbani kwao Machame mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi akitoa heshma za mwisho kwa mwili wa askari Polisi PC Meshack Urasa ambaye aliuawa kwa kupigwa na nondo juzi Jijini Mbeya. Mwili wa marehemu ulisafirishwa leo kwenda nyumbani kwao Machame mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi
skari Polisi wakitoa wakitoa heshma za mwisho kwa mwili wa askari mwenzao, PC Meshack Urasa ambaye aliuawa kwa kupigwa na nondo juzi Jijini Mbeya. Mwili wa marehemu ulisafirishwa leo kwenda nyumbani kwao Machame mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.
Picha Zote na Venance Matinya na Mtandao huu
Baadhi ya wakazi jijini Mbeya wakijadiliana kuhusu tatizo la upigaji Nondo mkoani Mbeya kushoto ni Mwenyekiti wa TTP Maendeleo Bwana Godfrey akiwa na Mchungaji Mwamalanga(katikati) na Mzee Mwambola Mwenye umri wa miaka 82.
Maafisa wa vikosi vya ulinzi na usalama mkoani Mbeya wakitoa heshima za mwisho kuuaga mwili wa askari Marehemu Meshack Urassa, upande wa kulia ni Kamanda wa uhamiaji wa mkoa wa Mbeya, akifuatiwa na Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi, anayefuata Mkuu wa wilaya ya Mbeya Bwana Evans Balama, anayefuata Kamanda wa Jeshi la magereza mkoani Mbeya na wengineo.
Baadhi ya askari wakiwa wamebeba Jeneza
Utani wa makabila uliibuka katika harakati za kuuaga Mwili wa marehemu Urassa baina ya Wachaga na wapare ambapo anaonekana Bwana Ernest Mdee akionesha pesa zenye thamani ya elfu hamsini kuwataka Wachaga kulipa Shilingi laki moja. Ambapo Wachaga walifanikiwa kutoa shilingi Laki moja na elfu nne ambazo zilisaidia mahitaji katika msiba huo.
Mke wa marehemu Urassa akishindwa kujizuia baada ya kuuaga mwili wa marehemu mumewe.

TIBA YA KIKOMBE CHA JAFARI MKOANI MBEYA YASIMAMISHWA KUTOKANA NA SABABU MAALUMU HAZIRUHUSU KUENDELEA KUTOLEWA.

Kamanga na Matukio | 02:41 | 0 comments
Na mwandishi wetu.
Kijana Fikiri Jafary mwenye umri wa miaka 17 mkoani mbeya eneo la mabatini amesitisha zoezi la utoaji wa kikombe kwa sababu maalumu ambazo hazimruhusu yeye kuendelea na zoezi hilo la utoaji dawa.

Mratibu wa tiba za asili mkoani hapa Bwana Boniventure Mwalongo amesema kuwa kijana huyo aliyekuwa akitoa huduma ya kikombe amekatazwa kutoa huduma hiyo kwasababu hajakidhi vigezo na masharti katika utoaji wa huduma ya tiba ya asili.

Aidha ameongea kuwa kijana huyo alikuwa hajafuata taratibu za kujisajili kama mganga wa tiba za jadi na umri wake hauruhusu kuwa mtaalamu wa tiba za asili kwa kuwa hakufikisha umri wa miaka 18 na hakuwa mtaalamu miaka ya nyuma kabla ya kuanzisha kikombe.

ZAIDI YA WATU 12 WAMEPINGWA NONDO MPAKA SASA NDANI YA SIKU SABA

Kamanga na Matukio | 02:40 | 0 comments
 Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi.
=====
Na mwandishi wetu.
Zaidi ya watu 12 wamepigwa Nondo mpaka sasa kwa muda wa siku 7 ambapo miongoni mwao wakiwemo askari polisi wawili mmoja kutoka kitengo cha usalama barabarani na mwingine katika kitengo cha ufundi Mbeya ambaye alifariki dunia.

Habari za uhakika zinadai kuwa kati ya watu hao 12 watu 11 wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa Mbeya akiwemo askari wa kike kutoka kitengo cha usalama barabarani WP.HAWA ambaye amelazwa katika wodi ya watu mahututi (ICU).

Kutokana na matukio hayo kuanza kuchukuwa kasi kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amesema kuwa Jeshi la polisi limejipanga kikamilifu kuhakikisha matukio hayo yanakomeshwa mara moja.

Aidha ameiomba jamii kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kutoa taarifa za uwepo wa watu wanaodhaniwa kuwa ni wahusika wa matukio hayo ili waweze kudhibitiwa mara moja.

WATOTO WANUSURIKA KIFO BAADA YA MAMA YAO KUPEWA TARAKA.

Kamanga na Matukio | 06:15 | 0 comments
Baada ya Mama yao Bi Madawa kupewa taraka na mmewe, alichanganyikiwa hali iliyopelekea kuwatumbukiza shimoni watoto hawa na kutaka kuwanyonga, ndipo wasamalia wema walipofanikiwa kuwaokoa na sasa wanatunzwa katika mtaa wa Senjele, kwa Mwenyekiti wa mtaa Bwana Elieza Mtindi hivyo wasamalia wema wanaombwa mchango wa hali na mali ili watoto hao kuweza kujikimu na kuenda shule kwani mama yao amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya katika Wadi ya wagonjwa wa akili.

Aliyembeba mtoto anaitwa Valena Jumanne mwenye umri wa miaka saba, aliyebebwa anaitwa Exaud Smith umri wa mwaka mmoja na kushoto anitwa Siri Smith umri wa miaka minne. Mchango wowote wasiliana na mmiliki wa mtandao huu kwa simu namba 0754 490 752 ili kukufikisha walipo ili kuweza kuokoa maisha ya watoto hawa.

MBEYA KUNANI NA ZIMWI HILI LASABABISHWA NA NANI KILA SIKU AJALI

Kamanga na Matukio | 05:54 | 0 comments
Gari ya abiria yenye jina la Shapa Bup lenye namba ya T 999 ABP iliyokuwa ikiendeshwa na Bwana Khalifa Mussa umri wa miaka 33, mkazi wa Kabwe jijini Mbeya. Gari hili liligongana na gari mali ya Idara ya Sheria lenye namba STK 5960 lililokuwa likiendeshwa na Bwana Robert. Na kizungumkuti pale madereva walivyoanza kubishana kuwa mwenzie ndiye kasababisha ajali hiyo.
Mtandao umebaini kuwa chanzo hicho ni Mwendokasi na hivyo Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi amewaonya madereva wanaosafiri kwa mwendokasi na kwamba atakayebainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

MWENDOKASI BADO NI TATIZO MKOANI MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:17 | 0 comments
Gari hili ambalo lilipinduka eneo la Mahenje wilayani Mbozi ambapo Namba za usajili zilifunguliwa na dereva wake inadaiwa alikimbizwa katika hospitali ya Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya.

JAMII YATAKIWA KUONDOKANA NA DHANA YA KWAMBA UTUMIAJI WA TIBA ZA ASILI NI USHIRIKINA.

Kamanga na Matukio | 02:29 | 0 comments
 Na mwandishi wetu.
Jamii imeshauriwa kuondokana na dhana ya kwamba utumiaji wa tiba za asili ni ushirikina na badala yake wametakiwa kuzitumia tiba hizo kwa kuwa ndio chimbuko la tiba zinazotolewa hospitalini.

Ushauri huo umetolewa na mmiliki wa tiba ya sayansi na asili Boniventure Mwalongo wakati wa mahojiano ofisini kwake kuhusu umuhimu wa tiba za asili kwa binadamu.

Amesema tiba za asili zimeruhusiwa na wizara ya Afya na kwamba huduma za tiba asili zinazopigwa marufuku ni zile zinazotolewa na waganga wa jadi wanaopiga ramli.

Septemba 24 mwaka huu Waziri mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda aliruhusu tiba asili na kuwataka waganga wa jadi kufuata masharti yaliyotolewa na wizara ya afya wakati wa utojia wa huduma zao kwa jamii.

WANANCHI KIJIJI CHA NAMING'ONG'O WILAYA MPYA YA MOMBA - MBEYA HUSAFIRI UMBALI MREFU KUTAFUTA HUDUMA YA SAFI NA SALAMA

Kamanga na Matukio | 02:27 | 0 comments
 Picha hii ni kielelezo cha miundombinu ya maji Nchini Tanzania.
Na mwandishi wetu.
Wakazi wa kijiji cha Naming’ong’o kata ya Chitete wilaya mpya ya Momba mkoani Mbeya wanalazimika kutembea umbali mrefu kutafuta maji kutokana na kijiji hicho kutokuwa na miundombinu ya maji safi

Wakiongea na nasi wananchi hao wamesema licha ya kata hiyo kuwa na mto mkubwa wa Nkana bado wanakabiliwa na tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi.

Afisa mtendaji wa kijiji hicho Venans Simkoko amesema kuwa kijiji hicho kimekuwa kikikabiliwa na tatizo la maji kwa muda mrefu na kwamba hawaoni jitihada zozote zinazochukuliwa ili kutatua tatizo hilo na kumtaka mbunge wa jimbo la Mbozi Magharibi David Ernest Silinde kulimaliza tatizo hilo kwa kipindi atakachokuwepo madarakani.

Hata hivyo huenda tatizo hilo likamaliza mapema kutokana na mpango unaoendelezwa na serikali kuwapatia huduma ya maji safi wananchi waishio vijijini.

WANAWAKE NCHINI TANZANIA WASHAURIWA KUJISHUNGULISHA NA KAZI ZA MIKONO.

Kamanga na Matukio | 02:25 | 0 comments
 Na mwandishi wetu.
Wanawake jijini Mbeya wameshauriwa kujishughulisha na shughuli mbalimbali zikiwemo kazi za mikono ili kujikwamua katika dimbwi la umaskini na kuwa tegemezi kwa waume zao.

Hayo yamesemwa na katibu wa idara ya wanawake kanisa la Moravian jimbo la kusini wilaya ya kyela BI.Idda Mwaiseba katika mahojiano wilayani humo.

Amesema mwanamke anaweza kukombolewa endapo yeye mwenyewe atachukua hatua za haraka kujishughulisha na kazi mbalimbali badala ya kutegemea kupewa huduma na mumewe.

Kwa upande wao baadhi ya wanawake wa kanisa hilo wamesema kuwa kupitia vikundi vya wanawake wameweza kupeana elimu ikiwa ni pamoja na kupata mikopo kutoka kwenye taasisi mbalimbali kwa urahisi zilizowawezesha kuanzisha shughuli mbalimbali za ujasiriamali.

HALI NI TETE YA DEREVA WA LORI LILILOUA WATU WATATU WATEMBEA KWA MIGUU MJI MDOGO WA MBALIZI.

Kamanga na Matukio | 06:32 | 0 comments
Dereva wa gari aina ya Lori lenye namba IT.9518 Bwana Wilfred hali yake si shwari kutokana na kushidwa kuzinduka, baada ya kupata maumivu makali kichwani.
Muuguzi wa hospitali Teule ya Ifisi, wilaya ya Mbeya vijijini, Rhoda Kasongwa,alipolazwa dereva huyo.

HALI MPAKANI TUNDUMA SASA NI SHWARI BAADA YA KUTANBGWAZWA KWA MATOKEA NCHINI ZAMBIA.

Kamanga na Matukio | 06:03 | 0 comments
 Katikati mwenye koti jeusi diwani wa kata ya Tunduma Mheshimiwa Frank Mwakajoka Baada ya wafanyabiashara kushindwa kufanyabiashara zao na kupelekea kufunga kutokana na vurugu zilizotokea za kupingwa ucheleweshaji wa matokea ya uchaguzi nchini Zambia sasa ni shwari na wananchi wameanza kuvuka mpaka na wafanyabiashara kurejea katika shughuli zao.
 Baadhi ya wananchi waishio mji mdogo wa Tunduma waliokuwa wamekusanyika sehemu moja baada ya kufungwa kwa biashara zao.
Madereva wakielekea kukamilisha ushuru wa foroza na kukamilisha taratibu za kuvuka mpaka kuelekea nchini Zambia na Kongo.

MGOMO WA MADEREVA MKOANI MBEYA WAGONGA MWAMBA

Kamanga na Matukio | 05:34 | 0 comments
 Baadhi ya madereva waliogoma hapo jana wakishinikiza Serikali kutoa Tochi zinazotumika kuzuia mwendokasi barabarani, ili kuwapa fursa ya kusafiri kwa mwendokasi suala ambalo Mkuu wa Usalama wa barabarani Ezekiel Mgeni aligoma kuruhusu ombi hilo, na hayuko tayari kuvunja sheria kwani ajali nyingi za sababishwa na mwendokasi.
Mabasi yakitoka baada ya kusitisha mgomo kufuatia kauli ya Mkuu huyo wa Usalama wa barabarani ambapo aliwataka madereva ambao hawako tayari kufuata sheria za usalama wa barabarani warudishe Leseni na kwamba hayupo tayari kuona maisha ya watu wakiangamia na wengine kuwa walemavu.
 Basi la Mbeya Express liliondoka stendi kuu baada ya kauli ya Mkuu wa usalama barabarani mkoani hapa.
 Mwenyekiti wa Stendi kuu ya mkoa wa Mbeya Bwana Noah Mwakatumbula awaonya madereva watakao kaidi sheria za usalama wa barabarani watapambana na mkono wa sheria na hauyo tayari kuwatetea.

WAFANYABIASHARA WADOGOWADOGO MAARUFU KAMA MACHINGA WAENDELEA KUKOSA HAKI ZA KUENDESHA BIASHARA ZAO.

Kamanga na Matukio | 05:04 | 0 comments
Na mwandishi wetu.
Wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama machinga jijini Mbeya wamelalamikia tamko la halmashauri ya jiji kuwataka kuondoka katika maeneo wanayofanyia biashara pasipo kuwaonesha sehemu nyingine.

Wakiongea na mwandishi wetu baadhi ya wafanyabiashara hao Bwana Baraka Daudi na Bwana Nicholous Msingwa wamesema kuwa halmashauri hiyo haijawashirikisha katika maamuzi waliyoyatoa japokuwa wamefanya uamuzi mzuri lakini wanaomba watengewe eneo kwa ajili ya kuendeshashughuli zao.

Aidha wafanyabiashara hao wanaiomba serikali iwape muda wakuendeleza biashara zao hadi pale watakapotengewa eneo lao ili kuendelea na biashara zao.

Wameongeza kuwa kutengewa eneo maalumu itatoa mchango mkubwa kwao kufanyabiashara kwa uhuru na kwa matumaini ili kuweza kujiongezea kipato na kwamba kutangatanga itachangia kuyumba kiuchumi kwa wengi wao wanategemea biashara hiyo katika kuendesha familia zao.

Hata hivyo wamekuwa wakiendesha biashara zao kwa kuchukua mikopo kutoka taasisi mbalimbali za kifedha  ikiwa ni pamoja na Pride, Saccos, hivyo kuhamishwa huko kwa ghafla kutawaathiri katika urudishaji wa mikopo hiyo.
 
Wamehitimisha kwa kusema utaratibu wao wakibiashara hutegemea kuwakopesha wateja wao hivyo kuwapata sehemu wanazohamishiwa itakuwa vigumu na matokeo yake ni wanahesabu wamepata hasara.

AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA KWA KOSA LA WIZI WA MAGUNIA 84 YA ZAO LA KOKOA

Kamanga na Matukio | 04:45 | 0 comments
Na mwandishi wetu.
Mlinzi wa kampuni ya Leritea amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la wizi wa magunia 84 ya zao la kokoa yenye thamani ya shilingi milioni 15, mali ya Interpres Company Litimed.

Akiongea na mwandishi wa habari hii Hakimu Mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Kyela Bwana Joseph Luambano amesema mtuhumiwa Bwana Piulent Mwamlewa ni mlinzi wa kampuni ya Leritea ambaye alikuwa na wenzake watatu waliochiwa huru baada ya uchunguzi wa mahakama kukamilika na kuonekana hawana hatia.

Aidha amesema kuwa mbinu iliyotumika na mshitakiwa ni kumpiga nondo mlinzi wa kampuni ya Interpres Company Limited(ICL) Bwana Lupakisyo Emanuel na kisha kuchukua mali hizo.

MJI MDOGO WA TUNDUMA HALI SI SHWARI KWA WAFANYABIASHARA.

Kamanga na Matukio | 05:31 | 0 comments
Kufuatia kuchelewesha kwa matokeo ya uchaguzi mkuu nchini Zambia, milipuko ya mabomu imekuwa ikilindima siku ya jana kuanzia majira ya saa 4 asubuhi wilayani Nakonde nchini humo hali iliyopelekea kuwa si shwari katika mji mdogo wa Tunduma kutokana na ukaribu uliopo wa kibiashara.

Kuanzi majira ya 7 mchana maduka yalikuwa yemefungwa huko Tunduma na wengine kuhabisha bidhaa zao kutoka nje ya mji huo wakihofia kuibiwa au kuvuinjwa kwa maduka yao kutokana na ukaribu wa eneo la tukio.

Mtandao huu ulipata kushuhudia milipuko hiyo mfulululizo mpaka majira ya saa 1 usiku ambapo iliwafanya baadhi wa Wanazambia waliokamilisha kupata kibali cha kuvuka mpaka,  kushindwa kushindwa kuvuka mkapa kuelekea nchini mwao.

Hata hivyo mrundikano wa Magari ulikuwepo mpakani hapo na watu kuhofu  kuvuka mpaka kutokana na b=mabasi mawili ya Kampuni ya Falcon na Taqwa kurudishwa kutokana na machafuko, kwa taarifa zilizopo kuwa toka Septembe 17, mwaka huu magari ya abiria nchini zambia yalisitisha kutoa huduma ya usafirishaji kutokana na hali hiyo ya sitofahamu ya uchaguzi uliofanyka siku ya Jumanne wiki hii.

Shuhuda kutoka Tunduma aitwaye Bwana Alex Kajumulo ambaye hufanya shughuli zake mji wa Kapirimposhi ameshindwa kufanyabiashara nchini humo na kuambua kurejea nchini Tanzania kutokana na hali ya machafuko nchini Zambia.

Mvutano mkali upo kati ya Chama cha siasa cha Upinzani ya UPF  kinachongozwa na Bwana Michael Sattah na Chama tawala cha MMD kinachoongozwa na Bwana Rupia Banda. ambapo wapinzani wanadai wameshinda uchaguzi huo na kwamba Serikali inataka kuchakachua matokeo hayo na kusababisha machafuko nchi nzima.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Tunduma Mheshimiwa Frank Mwakajoka amesema hali hii imepelekea wajasiriamali na wafanyabiashara katika kata yake kushindwa kufanya biashara tangu jana, ambapo inawatia hofu kiuchumi kwani Wilaya ya Nakonde na Tunduma zinategemeana kibiashara.

Kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa wa Mbeya ilikutana jana mchana, ili kupanga mikakati ya kuimarisha Ulinzi na usalama mpaka.

AJALI MBAYA YA LORI MJI MDOGO WA MBALIZI WATU WATATU WAFARIKI

Kamanga na Matukio | 03:52 | 0 comments
 Polisi wakiangalia gari aina ya roli lenye namba IT.9518, lililopata ajali baada ya kugongana na gari jingine na hivyo kupinduka na kusababisha vifo vya watu watatu watembea kwa miguu na kuvunja nyumba
Gari lenye T.438 BRT aina ya Landover, mali ya mchungaji Nduka wa kanisa la Uinjilist Mbalizi. Ambalo liligongana na Lori hilo.
Taswira ya mbele ya Lori hilo lililosababisha hasara kumbwa.
Mwanafunzi wa chuo kikuu cha DIT kilichopo Dar es Salaam , Marehemu Dickson Nswila, ambaye alikuwa akielekea kwenye mazoezi ya vitendo TAZARA, jijini Mbeya

Mfanyabiashara wa mitumba, mji mdogo wa Mbalizi Marehemu Charles Mwakanyuma.

Marehemu Mariam Side mwenye umri wa miaka 31,
AJALI mbaya ya lori iliyotokea eneo la Tarafani mji mdogo wa Mbalizi, imesababisha vifo vya watu watatu waliokuwa wakitembea pembezoni mwa barabara ya Mbeya kwenda mji mdogo wa Tunduma, wilayani Mbozi.
 
Ajali hiyo iliyotokea jana saa 2:30 asubuhi, ilihusisha lori hilo , lenye namba IT.9518, lililokuwa likitokea mjini Dar es Salaam , kuelekea nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Kongo (DRC).
 
Muuguzi wa hospitali Teule ya Ifisi, wilaya ya Mbeya vijijini, Rhoda Kasongwa, alisema wamepokea miili ya marehemu watatu akiwemo mwanamke mmoja pamoja na majeruhi mmoja ambaye ni dereva wa lori hilo .
 
Alisema dereva huyo ambaye bado hajatambulika jina lake, wala makazi amepoteza fahamu na anaendelea kupatiwa matibabu, akiwa chumba cha wagonjwa mahuituti (ICU), hospitalini hapo.
 
Aliongeza dereva wa roli, ambaye jina halijatambulika amepoteza fahamu na amelazwa chumba cha wagonjwa mahututi na kuwa ameumia vibaya maeneo ya kichwani pamoja na miguuni, hivyo jitihada zaidi zinafanyika ili kuokoa maisha yake.
 
Aliwataja marehemu kuwa ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha DIT kilichopo Dar es Salaam , Dickson Nswila, ambaye alikuwa akielekea kwenye mazoezi ya vitendo TAZARA, jijini Mbeya na mfanyabiashara wa mitumba, mji mdogo wa Mbalizi Charles Mwakanyuma.
 
Kwa mujibu wa Muuguzi huyo wa hospitali Teule ya Ifisi, mtu wa tatu aliyefariki katika ajali hiyo ni Mariamu Said (31), mkazi wa mji mdogo wa Mbalizi.
 
 
Watu walioshuhudia ajali hiyo walisema lori hilo lililokuwa limepakia shehena ya Chokaa, lilikuwa katika mwendo kasi, na kabla ya kuwagonga na kisha kupinduka, liligonga gari T.438 BRT aina ya Landover, mali ya mchungaji Nduka wa kanisa la Uinjilist Mbalizi.
 
Walisema dereva wa Landlover alikimbizwa hospitali ya Ifisi na aliruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kutibiwa na kuonekana hali yake ni nzuri, kwani alipata michubuko kidogo.
 
Waliongeza kabla ya kuligonga Landrover, lori hilo lilikwepa basi lililokuwa limewabeba wafanyakazi wa hospitali Teule ya Ifisi, ndipo liligonga gema lililopo pembeni  ya barabara, kupaa hewani kisha kwenda kuingia kwenye karakana ya mafundi seremala, iliyopo eneo la Tarafani.
 
Wananchi hao walisema polisi walifika eneo la tukio mapema, na hivyo kuweza kunusuru wananchi wasiendelee kupakua shehena ya Chokaa, ambayo walikuwa wakibeba mifuko na kutokomea nayo majumbani kwao.
 
Aidha, mwanamke mmoja alijitolea kwa kivua kitenge chake, kumfunika dereva aliyekuwa amepoteza fahamu na kisha kusaidia kumpakia kwenye gari ili kumuwahisha  hospitalini.
 
Aidha, kabla ya polisi hawajafika eneo la tukio, baadhi ya watu wasiofahamika walifanikiwa kufungua tenki la mafuta la lori hilo na kisha kutokomea nalo.
 
Baadhi ya wananchi walisema wanasikitishwa na kitendo cha baadhi ya watu waliowahi kufika eneo la tukio, kuanza kugombania mifuko ya Chokaa, badala ya kusaidia kuwaokoa majeruhi na kuondoa miili ya marehemu.
 
Miili ya marehemu wote watatu imehifadhiwa hospitali Teule ya Ifisi, iliyopo wilaya ya Mbeya vijijini.
 
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Anaclet Malindisa, alipotafutwa kwa simu yake ya mkononi, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi.

SERIKALI YAOMBWA KUANZISHA VYUO VYA UDEREVA PIKIPIKI ILI WAWEZE KUZIJUA SHERIA ZA BARABARANI

Kamanga na Matukio | 03:20 | 0 comments
 Na mwandishi wetu.
Wadau wa usafirishaji mkoa wa Mbeya wameiomba Serikali kuanzisha vyuo vya udereva wa pikipiki ili kuwawezesha madereva wa pikipiki na bajaji kuzijua sheria za barabarani.

Ombi hilo limetolewa na wakazi wa mtaa wa Mwanjelwa jijini Mbeya wakati wa mahojiano na mwandishi wetu juu ya namna wanavyoweza kushirikiana na Serikali kupunguza matukio ya ajali za pikipiki.

Wamesema uelewa mdogo wa madereva wa pikipiki kuhusu sheria za barabarani ndio chanzo kikubwa cha ajali za pikipiki na ufumbuzi wa tatizo hilo ni madereva kutokupewa leseni mpaka watakapo kuwa wamepitia vyuo vya udereva wa pikipiki.

Kwa upande wao madereva wa pikipiki Bwana Joseph Mbwilo na Bwana Issa Nziku wamesema ili kukabiliana na tatizo la ajali zitokanazo na uzembe wa baadhi ya madereva wa pikipiki, wamiliki wa pikipiki wanatakiwa kuajiri madereva walio na elimu ya usalama barabarani.

AUA MKEWE KWA JEMBE NAYE AUAWA

Kamanga na Matukio | 05:43 | 0 comments
Na Ezekiel Kamanga.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa Bwana Doto Njige alimuua mkewe kwa kumkata na jembe mara tatu kichwani usiku wa kuamkia Septemba 19 mwaka huu kwa kile kilichodaiwa ni wivu wa kimapenzi.

Mkewe aliyefahamika kwa jina la Selina Cheling(55) alikufa papo hapo baada ya kumkata na jembe ambapo wananchi wa kijiji cha Ubaruku walimkamata Doto Njige na kuanza kumshushia kipigo cha nguvu hali iliyofanya uongozi wa kijijini kuingilia kati na kumnusuru mkazi huyo.

Kumnusuru huko hakukusaidia chochote kwani akiwa njiani kupelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu alifariki dunia kutokana na kuvuja damu nyingi.

Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya limethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo Kaimu Kamanda wa Polisi Anacletus Malindisa amesema polisi inaendelea na msako wa kuwabaini waliohusika na kitendo hicho.

Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi mkoani Mbeya kutojichuklulia sheria mkononi kwani ni hatari na kunaweza kuvuruga amani ya Tanzania.

WANNE WAFIKISHWA MAHAKAMANI, WIZI WA GATE VALVES NA AIR TUBES MALI YA MAMLAKA YA MAJI TAKA NA SAFI MBEYA NA WANANCHI WATAKIWA KUTOA TAARIFA ZAIDI.

Kamanga na Matukio | 05:41 | 0 comments
 Na mwandishi wetu.
Mamlaka ya maji safi na maji taka mkoani Mbeya imepata hasara ya shilingi milioni 35 kutokana na kuibiwa kwa vifaa vya kuunganishia mabomba ya maji ambayo yamefungwa kwenye mradi mpya unaojengwa na kampuni ya Sogea Satom kutoka nchini Ufaransa.

Akiongelea hasara hiyo Afisa habari wa mamlaka hiyo Bi Mery Sayula amesema vifaa vilivyoibiwa ni gate valves na air tubes zenye vipenyo vya milimita 75 hadi 400.

Aidha amesema kuwa hadi sasa watu wanne wamekamatwa na wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Mbeya.

Wahati huohuo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa dhidi ya wezi wa vifaa hivyo, na kuongeza kuwqa zawadi ya shilingi 500,000/= itatolewa kwa atakayefanikisha kukamatwa kwao.
 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger