Pages


WANAFUNZI SHULE YA MSINGI KAMBARAGE YA JIJINI MBEYA WAFURAHIA KUHITIMU DARASA LA SABA.

Kamanga na Matukio | 06:10 | 0 comments
Wanafunzi 228 wafanya mtihani kati 236 waliokuwa wamesajiliwa, Nane washindwa kufanya mtihani kutokana na utoro, ambao ni wavulana 6 na wasichana wawili hayo yamethibitishwa na Mwalimu FEBRAM MWANGANYA. 

WAFANYABIASHARA WA MWAMBENE JIJINI MBEYA WAIOMBA SERIKALI KUWATENGEA ENEO MAALUMU LA BIASHARA

Kamanga na Matukio | 05:58 | 0 comments
Na mwandishi wetu.
Wafanyabishara wa eneo la Mwambene kata ya Ilomba jijini Mbeya wameiomba serikali kuwatengea eneo maalum kwa ajili ya soko kutokana na eneo wanalouzia kwa sasa kutokuwa rasmi.

Akiongea na mwandishi wetu mmoja wa wakazi wa eneo hilo bwana Simoni Nyika amesema kuwa anakerwa na kitendo cha wafanyabiashara hao kuuza bidhaa zao katika eneo la barabara kwani kitendo hicho kinahatarisha maisha yao.

Naye mmoja wa wafanyabiashara hao Bi Grace Kisonga amesema kuwa kipindi cha nyuma walitakiwa kuhama na kwenda eneo lililopo mbali kidogo na barabara hiyo lakini imeshindikana kwani eneo hilo linamilikiwa na mtu binafsi.

Ameongeza kuwa kutokana kushindwa kulipia eneo hilo imepelekea wafanyabiashara hao kuendelea kuuza bidhaa kwenye eneo hilo la barabara.

WAKAZI WA MWAKIBETE JIJINI MBEYA WALIA NA WANAOTUPA TAKA ENEO LISILO RASMI.

Kamanga na Matukio | 05:43 | 0 comments
Na mwandishi wetu.
Wakazi wa mtaa wa Nyibuko kata ya Mwakibete wamewalalamikia baadhi ya wakazi wa maeneo ya jirani kwa kitendo cha kutupa taka eneo lisilo rasmi.

Wakiongea na mwandishi wetu kwa nyakati tofauti bwana Abasi Kalinga na Bi Albina Masheta wamesema kuwa licha ya kukatazwa kutupa taka eneo hilo watu hao wanaendelea kutupa taka hizo hasa nyakati za usiku .

Kwa upande wake afisa mtendaji wa mtaa huo ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa sababu maalum amesema kuwa huwa wanafanya mikutano kila wakati kuzungumzia mazingira yao na kwamba waliweka vibao vya matangazo kuwataka watu kuacha kutupa taka katika eneo hilo.

Pia ameongeza kuwa wanampango wa kumtafuta mgabo wa kulinda eneo hilo ili waweze kuwakamata watu hao na kuwafikisha mbele ya sheria.

MAWE YA AJABU YARINDIMA NYUMBA MBILI JIJINI MBEYA POLISI WASHINDWA WA KUMKAMATA

Kamanga na Matukio | 05:38 | 0 comments
Wakazi wawili Mwanyanje kata ya Igawilo jijini Mbeya Bwana SEMENI MSAFIRI na Bwana LEVO MWANGALA  wapo katika wakati mgumu baada ya nyumba yao kupigwa mawe yaajabu na watu wasioonekana.

Tukio hilo limekuwa likitokea majira ya saa kumi na mbili jioni hadi saa 4 usiku na kuanza tena saa kumi na mbili asubuhi mpaka saa moja na nusu asubuhi.

Hayo yamethibitishwa na Mwenyekiti wa mtaa wa Mwanyanje ELIA JEREMA (OBAMA) na amesema tukio hilo limedumu kwa muda wa mwenzi mmoja hadi sasa ambapo alipata taarifa kutoka kwa balozi wa mtaa huo Bwana PETER MWANIBUNGU ambapo kwa pamoja walimwita Chifu mdogo Bwana EDSON MWANYANJE ambaye pia alishindwa kutatua tatizo hilo na kudai kuwa kuna mapepo.

Lakini kwa siku ya jana aliitwa Chifu wa Mkoa Bwana MWASHINGA kutoka eneo la Spweto jijini Mbeya akiwa na machifu wengine na kutfanya kikao eneo la tukio na ndipo hali ikawa mbaya sana na hivyo kusababisha machifu kusambaratika na kutoa tamko kwamba hali ni ngumu baada ya kuanza kupigwa kwa mawe hayo na hivyo waende wakajipange upya hata hivyo mwandishi wa habari hizi aliamua kuvaa elemet/kofia ya pikipiki kujikinga ili kuendelea kupata habari hizi.

" Nimeshuhudia matukio mbalimbali  katika nyumba ya Bwana SEMENI.yakionekana eneo hilo ikiwemo samaki wakavu aina ya magege wakipita angani, vikombe na sahani za udongo zikidondoka sakafuni bila kuvunjika, mafuta ya kupakaa aina ya Carorite, vikombe vya plastiki vitatu, hotpot moja, na mambo mengine yakiambatana na mawe, kama betri na mawe yaliyotengenezwa kwa saruji ambayo bado yalikuwa hayaonekani ambayo yalipelekea kuitwa Jeshi la Polisi Kituo kidogo cha Uyole ambapo walifika eneo hilo majira saa moja na dakika 45" 

Picha za tukio zima tunazo endelea kutembelea mtandao huu. 

AJALI NYINGINE YA MAGARI YA MIZIGO MKOANI MBEYA YATOKEA ENEO LA SENJELE WILAYANI MBOZI

Kamanga na Matukio | 05:17 | 0 comments
 Gari ya mzingo aina ya Scania liliokuwa limebeba tofali kuelekea Jijini Dar es Salaam limefeli mfumo wa breki na hivyo kusababisha kugonga zaidi ya magari matatu na kufunga barabara eneo la Mteremko wa Senjele wilayani Mbozi mkoani Mbeya majira ya Saa 12 jioni.
 Roli kubwa kusholo likiwa limekwama mtaroni wakati wa jitiihada la kulikweba gari lililosababisha ajali hiyo na hivyo kupelekea mpaka sasa kushindwa kutoka na wito kwa madereva kuwa makini na kudhibiti Mwendokasi eneo hilo 
Serikali inapaswa kuboresha miondombinu katika eneo hilo kwa Mkoa wa Mbeya ni moja kati ya mikoa mingine iliyokosa njia mbadala, na hivyo kusababisha foleni kubwa mara baada ya ajali kutokea hali inayopelekea Madereva wa magari makubwa ya mizigo kushindwa kufika kwa wakati muafaka katika Vituo na hivyo kukubwa na tozo la fidia.

MWANDISHI WA HABARI MKOANI MBEYA AINGIZWA MJINI KWA KUTAPELIWA NA VIBAKA/VIKABA JESHI LA POLISI MKOANI MPO!!

Kamanga na Matukio | 05:03 | 0 comments
  Kijana Lusekelo Mwakanje akiwa amekamatwa muda mfupi mara baada ya kufanya utapeli wa kumuuzia Jumba la Simu aina ya Nokia lililotiwa mchanga ndani kwa Pesa za Kitanzania shilingi 25, 000/= Mwandishi wa habari na Mtangazaji wa Ushindi FM Radilo iliyopo kata ya Isyesye jijini Mbeya majira ya saa 11 Jioni eneo la Stendi ya kuelekea Wilaya ya Chunya mkabala na Soko la Sido Mwanjelwa.
 Jumba la Simu maarufu kama Housing ambayo huunzwa shilingi 2,000/= likiwa limejanzwa mchanga ndani, na hivyo kuonesha Taswira kamili ya simu ya mkononi, kwani usipokuwa makini waweza kudhania ni simu iliyokamilika
Taswira kamili ya utapeli huo uliokithiri Jijini Mbeya baada ya kufunguliwa tukashuhudia Mchanga na kuwafanya Abiria wengi kulinzwa na wakati mwingine kutiwa hasara.

Kijana huyo ameachiwa huru na kutuonyesha Mtandao mzima wa matapeli na Makazi yao na hivyo Jeshi la Polisi mkoani Mbeya bila shaka mwatambua hili na ni kazi kwenu sasa kushirikiana nasi bega kwa bega kutokomeza janga hili.

MWANAKONDOO AMESHINDA.

Kamanga na Matukio | 04:56 | 0 comments
Mwalimu Steven Gwasa Mwakatwila akijiandaa kwenda kufundisha neno la Mungu anamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kumuwezesha kupata usafiri wa gari.Amapo mafunzo yake hutoa katika Makanisa nchini Tanzania.

Kwa mafundidho yake tembelea katika website ya http://www.mwakatwila.com

MADEREVA 7 WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA KWA KOSA LA KUVUNJA SHERIA

Kamanga na Matukio | 04:43 | 0 comments
 Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi.
Hapa ni kituo cha magari ya abiria aina ya daladala cha Kabwe kilichopo Mwanjelwa jijini Mbeya na kinadaiwa kuongoza kwa madereva na makondakta kuvunja sheria za usafirishaji wa abiria kwani wamekuwa wakijaza abiria katika magari hayo kupita kiasi.

Na mwandishi wetu.
Kutokana na kukithiri kwa ajali za barabarani Mkoani Mbeya jeshi la polisi Jeshi la polisi mkoani Mbeya linawashikilia madereva saba akiwemo Faraja Emmanuel aliyekutwa akiendesha gari la abiria, licha ya kuzuiwa na Jeshi la Polisi kuendesha aina yoyote ya gari ili kuepuka ajali.

Mratibu mwandamizi wa polisi Anaclet Malindisa amesema kuwa madereva hao wamekamatwa kwa makosa ya kutumia leseni ambazo muda wake umekwisha na kutumia leseni za kuendesha maroli badala yake huendesha magari ya abiria na baadhi yao wamefikishwa mahakamani.

Amewataja madereva waliofikishwa mahakamani kuwa ni Emmanuel Mwakiselise, Iddan Sanga, Igno Mgaya kwa makosa ya kutumia leseni zilizokwisha muda wake na Faratieli Sanga, Michael Mwangoloka wapo rumande kwa kosa hilo hilo.

Wakati huohuo Kelvin Mwakitange amekamatwa kwa kosa la kutumia leseni ya daraja E ambayo hutumika kuendesha malori badala ya magari ya abiria kama alivyofanya.

Mbali na hilo Malindisa amesema Jeshi la polisi mkoani humo limejipanga kupunguza ajali hizo kwa kuweka kanuni madhubuti zitakazowalazimu madereva na abiria kuzifuata na kuimarisha doria katika barabara kuu za jiji sambamba na kutoa elimu kwa madereva na watembea kwa miguu juu ya kanuni za barabara.

Amesema ni kujaza abiria kupita kiasi ni makosa kisheria kwani kitendo hicho huweza kusababisha ajali na kuwataka abiria kudai tiketi pindi wanaposafiri.

Kamanda Malindisa ameongeza kuwa ni haki ya abiria kudai na kurudishiwa nauli yake mara tu gari linapoharibika njiani ili aweze kuendelea na safari yake kupitia gari lingine.

MTAHINIWA MKOANI MBEYA ANG'ATWA NA MBWA, AKOSA MSAADA WA MATIBABU BAADA YA KUKOSA FEDHA.

Kamanga na Matukio | 05:24 | 0 comments
 Mtoto VANESA AMBA mwenye umri wa miaka 13, ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi Ivumbwe wilaya ya Mbeya vijijini ameng'atwa na Mbwa mkono wa kuume/kulia na hivyo kupelekea kukosa msaada wa kupewa matibabu kwa kile kilichodaiwa kuwa alitakiwa kulipa shilingi 10,000/= mara baada ya kufika  katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya.
Leo hii  Septemba 7 mtoto huyo anatakiwa kuanza Mitihani ya kuhitimu elimu ya Shule ya msingi, Na mpaka habari hii inaingia mtandaoni alikuwa hajapatiwa msaada wowote. Mtoto huyu analelewa na Bibi yake Bi GRENDINA FUNGO mwenye umri wa miaka 65 ambaye hajiwezi na hivyo kuomba msaada kwa wasamalia wema kuweza kunusuru maisha yake.

MADEREVA WA DALADALA JIJINI MBEYA WADAI BIASHARA NGUMU

Kamanga na Matukio | 05:06 | 0 comments
Biashara ya usafirishaji wa abiria imekuwa ngumu jijini Mbeaya na badala yake madereka wameendelea kukiuka sheria za usama wa barabarani na hivyo kusababisha kutoa Rushwa ya shilingi elfu moja kwa askari wa usalama wa barabarani hasa katika kituo cha Maghorofani hata hali kadharika katika kituo cha Kabwe Mwanjerwa jijini Mbeya.

Kwa mujibu wa madereva wamedai kuwa wamekuwa wakitumia muda mrefu kutoka vituoni humo kutokana na foleni kubwa inayosababishwa na madereva na makonda wenye uchu wa Pesa kujaza abiria kupita kiasi na hivyo kutumia muda mwingi katika eneo moja. 

MKUU WA MKOA WA MBEYA AWATAKA WUTIMISHI WALIOHUSIKA KATIKA KASHFA YA UKUSANYAJI WA FIDIA PASIPO KUTOA STAKABADHI KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.

Kamanga na Matukio | 04:53 | 0 comments
Na mwandishi wetu.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Bwana John Livingstone Mwakipesile amemwagiza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Rungwe Bwana Noel Mahenga kuwafikisha katika vyombo vya sheria watumishi wa serikali waliohusika na kashfa ya kuwatoza faini ya shilingi 500 na kutowapa stakabadhi wananchi wanaodaiwa kutokuwa na vyoo pamoja na mazingira machafu ya nyumba zao.

Watumishi hao walichukua hatua hiyo walipokwenda kufanya operasheni ya usafi wa mazingira vikiwemo vyoo katika kata hiyo,hata hivyo badala ya kutekeleza kilichowapeleka waligeuza kama mbinu ya kujipatia fedha na mazao ya wakulima walioshindwa kulipa fedha hiyo.

Naye mmoja wa wananchi hao Philipo Mwakatumbula alisema kitendo kinachofanywa na idara hiyo ni kibaya kwani wanateseka kwa kushindwa kulipa shilingi mia tano na kunyang’anywa mazao yao ambayo wanategemea kwa chakula na kujipatia fedha.

WANAFUNZI WANAMCHANGO MKUBWA KATIKA BENKI YA DAMU KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI.

Kamanga na Matukio | 04:50 | 0 comments
Picha hii ni kielelezo cha jinsi ya uchangiaji damu.
Na mwandishi wetu.
Uchangiaji wa damu salama mashuleni mkoani Mbeya umepungua kutokana wanafunzi wanaochanguliwa kujiunga na masomo ya sekondari kuwa na umri mdogo na hivyo walio wengi kukosa kutimiza vigezo vya uchangiaji damu ambapo kigezo mojawapo ni kuanzia umri wa miaka 18.

Akiongea na mwandishi wetu Meneja wa kitengo cha damu salama nyanda za juu kusini Daktari Lelo Bilihima amesema kuwa licha ya kampeni na juhudi zinazofanywa na kitengo hicho kuwa uhitaji wa damu unatakiwa kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na kiasi kilichopo katika hospitali nyingi.

Aidha ameongeza kuwa damu hiyo haiuzwi na kwa yeyote atakayebainika anauza damu hiyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Ameeleza kuwa upungufu mkubwa wa damu katika Benki ya damu ya Kanda ya Nyanda za juu Kusini hutokea mara baada ya shule za sekondari kufungwa ambapo wamekua wakichangia kwa asilimia kubwa upatikanaji wa damu salama. 

Wakati huo huo akizungumzia upande wa wananchi Dkt. Baliyima Lelo amesema kuwa wachangiaji wengine wanaogopa ukubwa wa sindano hivyo kupunguza uchaangiaji wa damu na amewataka wananchi kuondokana na uvumi ulioenea kwa sasa kuwa mchangiaji akichangia mara moja atatakiwa kuchangia tena kwa zaidi ya mara na kusisitiza kuwa jukumu la kuchangia damu ni wajibu wa kila mmoja.

UZINDUZI WA ALBAMU YA PVC YA MJI MDOGO WA TUNDUMA WAFANA

Kamanga na Matukio | 06:17 | 0 comments
 Mchungaji Elias Swatta wa Kanila la EAGT Majengo Mapya Tunduma akiweka wakifu, kuzindua Albamu ya Tatu ya Kwaya ya PVC .
 Hii ni Kwaya PVC wakiwa katika Onesho nawakitoa burudani.
Mwenyekiti wa Kwaya ya  PVC kushoto Bwana Kiswigo
 Hii ni Kwaya ya Beroya Tunduma ambao walialikwa kusindikiza sherehe nzima za uzinduzi huo wa Albamu ya Majirani zao PVC
Kwaya ya Parapanda kutoka jijini Mbeya nao ilialikwa katika uzinduzi huo.

SHULE YA SEKONDARI SWILLA JIJINI MBEYA YALALAMIKIWA JUU YA ADHABU YA VIBOKO.

Kamanga na Matukio | 05:16 | 0 comments
 Katuni hii inaelezea uhalisia wa adhabu ambazo hutolewa Mashuleni hususani Tanzania.
 Adhabu za aina hii bado zaendelea? namwisho wake ni lini?
Na mwandishi wetu. 
Shule ya sekondari Swilla iliyopo jijini Mbeya imelalamikiwa na wanafunzi wa shule hiyo kwa kuwachapa viboko ovyo na kuwajeruhi bila sababu za msingi.

Baadhi ya wanafunzi hao wamesema shule hiyo ina tabia ya kuwapa wanafunzi adhabu katika vipindi vya masomo bila sababu za msingi ikiwemo kuchapwa viboko zaidi ya ishirini na kuwasababishia maumivu makali kwa kuwajeruhi vibaya.

Pia wamesema pindi wazazi wanapochelewa kulipa ada kupitia akaunti ya shule hiyo wanachapwa viboko ovyo bila ya wazazi kujua na wanatishiwa kupewa adhabu kali pindi watakapowajulisha wazazi wao juu ya vitendo wanavyotendewa.

Mmoja wa wanafunzi hao Ezekiel Kimaro amesema pindi wanapojeruhiwa vibaya na walimu hao hupelekwa katika vituo vya afya kutibiwa na hulazimishwa kusema uongo kuwa wameumia ili kuwalinda walimu hao.

Aidha amesema mnamo mwaka jana mwanafunzi wa kidato cha pili alipoteza maisha shuleni hapo baada ya kujeruhiwa vibaya kwa kuchapwa viboko na kukataliwa kupewa matibabu na wazazi wake kwa madai ya kutibiwa na uongozi wa shule hiyo hadi mauti yalipomfika mwanafunzi huyo.

Mwanafunzi huyo amesema kwa mwaka huu zaidi ya wanafunzi ishirini wamehama shule hiyo kwa kuhofia usalama wa maisha yao akiwemo mwanafunzi anayejulikana kwa jina la Roi Assay aliyevunjwa kidole katika mkono wake wa kushoto.

MAENDELEO YA WILAYA KIUCHUMI ,WANANCHI WA WILAYA YA RUNGWE NA VIONGOZI WA WILAYA HIYO WAPEWA PONGEZI

Kamanga na Matukio | 05:10 | 0 comments
Makao Makuu wa Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.
Na Mwandishi wetu.
Viongozi pamoja na wananchi wilayani Rungwe, na viongozi wa wilaya hiyo, wame.pongezwa kwa juhudi wanazozifanya katika kujiletea maendeleo, ikiwemo utekelezaji kwa vitendo sera ya Kilimo Kwanza.

Imeelezwa kumekuwa na jitihada za makusudi zinazofanyika katika ukusanyaji wa mapato ya ndani imeiwezesha halmashauri hiyo kutekeleza vyema mipango yote ya maendeleo iliyopangwa.

Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile, katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani, kilichokutana kujadiri taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Amesema hali ya ukusanyaji wa mapato ndani ya halmashauri hiyo, ambayo imeiwezesha halmashauri kupunguza utegemezi na kuendana na malengo ya milenia 2025.

Alisema niuvyema juhidi hizo zikaendelea kuongezeka k wa halmashauri kubuni vyanzo vingine vya mapato kutokana na hali nzuri ya uchumi wa wilaya kwani bado zipo fursa ambazo zikitumika vyema zitaiwezesha halmashauri kujitegemea kwa asilia kubwa zaidi”
Amesema wilaya ya Rungwe ni sawa na mkate ulionona na inanukia fedha, lakini mapato yanayokusanywa kutokana na vyanzo vyake vya ndani bado ni kidogo kwani wanao uwezo wa kukusanya sh.bilioni 1.6 kwa mwaka.

Mwakipesile alisema kwa hali hiyo Rungwe inao uwezo wa kujitegemea kwa asilimia 6, huku asilimia kubwa ikiwa ni fedha wanazozipata kutoka serikali kuu, hali ambayo haikubaliki hata kidogo na kuongeza kwamba kwa kawaida kufanikiwa ni rahisi, lakini kuendelea kushika nafasi hiyo ya mafanikio ndiyo kazi kubwa, hivyo kumtaka Mkurugenzi mtendaji, wakuu wa idara na wafanyakazi kwa jumla, kufanya kazi kwa bidii.

Alisema suala hilo litafanikiwa kwa wao kujihusisha kikamilifu katika kusimamia sheria, kanuni na miongozo ya serikali kuhusu ukusanyaji wa mapato na matumizi ya fedha za halmashauri.

Hata hivyo Mwakipesile, alisema wilaya ya Rungwe imekuwa ya pili mkoani Mbeya kwa kupokea fedha nyingi katika mwaka wa fedha 2011/2012, kwa kupata shilingi bilioni 31.3 ikitanguliwa na wilaya ya Mbozi.

WILAYA YA RUNGWE YAPATA MWENYEKITI MPYA WA WILAYA HIYO.

Kamanga na Matukio | 05:07 | 0 comments
Marehemu John Mwankenja ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilay ya Rungwe.

Na Mwandishi wetu.
Diwani wa kata ya Lufilyo Meckson Mwakipungu amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya wilaya ya Rungwe baada ya mwenyekiti wa awali John Mwankenja kuuawa na majambazi MEI 17 mwaka huu akiwa nyumbani kwake.

Akitangaza matokeo ya nafasi hiyo ya uwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Rungwe, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo bwana Noel Mahenga amesema Meckson Mwakipungu ameibuka na ushindi wa kura 40 huku mpinzani wake Anyemike Mwasakilali ambaye ni diwani wa kata ya Kawetere kutoka chama cha NCCR MAGEUZI amepata kura tatu.

Matokea ya uchaguzi huo yamepokelewa kwa furaha na mamia ya wakazi wa wilaya ya Rungwe, huku wakidai kuwa Meckson Mwakipungu anao uwezo mkubwa wa kuleta maendeleo kwenye Halmashauri yao.

MWENDOKASI BADO NI TATIZO KWA MADEREVA MKOANI MBEYA HALI INAYOPELEKEA KUSABABISHA AJALI NA HASARA

Kamanga na Matukio | 05:27 | 0 comments
 Gari hili aina ya Tipa mara baada ya kupata ajari namba ya usajili linalodaiwa kuwa ni mali ya Bwana Issa John S.L.P 3500 mkazi wa Mbeya.
Ajali hii imetokea wakati dereva akijaribu kumkwepa Mwendesha baiskeli na kulivaa gari kubwa la mizigo lilokuwa limepaki jirani na Kituo cha mafuta cha ORXY mtaa wa Mama John Jijini Mbeya majira ya Saa 2 na dakika 45 usiku..
 Mwenyekofia ya drafti hapo katikati ni Mwandishi wa Habari na Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha Bomba FM kilichopo Jijini Mbeya Bwana Iman John Mwakapoja akiwa eneo la tukio akiongea na wananchi walioshuhudia tukio hilo eneo la Mama John Jijini Mbeya.
Wananchi wakiwa eneo la tukio wakishuhudia zoezi la uokoaji wa majeruhi zaidi ya watatu wa ajari hiyo 
Tabia ya kutoa namba kwa Wamiliki wa Magari mkoani Mbeya yaendelea kwa sababu ambazo hazieleweki je?, ni kuficha ushahidi.

Mmoja anusurika kufa baada ya kubata kipigo kutoka kwa Wananchi kwa kosa la kutaka kuiba taa za gari, Jeshi la Polosi la wahi kumwokoa. 

BADO KERO YA MAJI MKOANI MBEYA NI SHIDA

Kamanga na Matukio | 05:00 | 0 comments
 Wananchi wa Kata ya Isyesye wamekuwa wakilazimika kuamuza usiku wa manane ili kupata Maji, hali hiyo imekuwa hatari kutokana na wanawake kubakwa.
 Wananchi wakiwa wanasubiri foleni, hali kadharika imekuwa musaada kwa vijana wasiokuwa na kazi kujipatia ajira ya kubeba maji kwa njia ya mikokoteni, ambapo wamekuwa wakibeba ndoo moja kwa shilingi 200/= za kitanzania kulingana na umbali.

WANANDOA WAWILI WAKAZI WA MTAA WA BLOCK T JIJINI MBEYA WASABABISHA KUVURUGIKA IBADA.

Kamanga na Matukio | 06:22 | 0 comments
*Ampiga Mke wake, Mke akimbilia Kanisani.
*Mchungaji aacha Mahubiri na kuamulia Ugomvi,
*Waumini wamfikisha Mume Kituo cha Polisi Mwanjelwa afunguliwa RB na jalada.i.

Imetokea katika Kanisa la Tanzania Assemblies Of God (T.A.G) Mtaa wa Block T jijini Mbeya. Ambapo sakata hilo lilianza nyumbani pale Mme anayejulikana kwa jina la Lusekelo muumini wa Dini ya Kiislamu alipo Mkewe anayefahamika kwa jina la Bahati avae vazi la Khanga ndipo Mwanamke huyo alivyo kaidi na kuvaa Kitenge kitendo kilicho muudhi Mmewe na kuanza kumpiga.

Baada ya kuona kichapo kikizidi Mwanamke huyo aliamua kukimbilia katika Kanisa hilo la Mchungaji Angolwisye Mwasunda akiwa Madhabahuni, hali iliyofanya ibada kuvurugika baada ya Mchungaji na waumini kuamulia ugomvi huondani ya Kanisa hilo takatifu.

Waumini walikuwa na zoezi nzito la kumdhibiti Lusekelo na hivyo kutoa taarifa Kituo kidogo cha Polisi kilichopo Mwanjelwa ambapo alifunguliwa RB hii MWNJ/RB/2630/2011. Haikuishia hapo, Mtuhumiwa aliendelea kuporomosha matusi mazito hali iliyopelekea Mkuu wa kituo cha Polisi hicho kumpeleka mtuhumiwa Lusekelo Kiruo Kikuu cha Ktai kilichopo Jijini Mbeya na kufungualia jalada/faili lenye namba MB/IR/7561/2011 kwa kosa la kufanya fujo kanisani.

MADUKA HAYA NDIO YALIYOVUNJWA ENEO LA INYALA NA KUPELEKEA MWANANCHI WA NNE KUSHIKILIWA NA JESHI LA POLIS KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA MTU MMOJA.I

Kamanga na Matukio | 05:29 | 0 comments
 Duka hili lina milikiwa na Bwana Musa Mwanabeya ambaye ni mmoaja kati ya watu wa nne waliomuuaji kijana moja hakufahamika jina lakini ni mkazi wa Uyole jijini Mbeya.
Hali kadharika na hili linamilikiwa na Bwana Musa Philemon ambaye naye ni Muuaji.
 Na hili linamilikiwa na Bwana Japhet Walenjela ambaye naye ni muuaji
*Watu wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mbeya.
*Hali hiyo ndio iliyopelekea wananchi 11 kati ya 1200 wanashikiliwa na Jeshi la polisi  kufanya maandamano bila kibali siku ya Jumapili asubuhi na Polisi kufanikiwa kuwatawanya watu wengine kwa kutumia Mabomu ya machozi  
 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger