Pages


KIPINDUPINDU;- Watu 17 wakamatwa kwa kukosa vyoo na uchafu wa mazingira Mkoani Mbeya.

Chimbuko Letu | 08:58 | 0 comments
 Mkuu wa Wilaya ya Kalonga, Nchini Malawi Rosemary Kalonga na Mkuu wa Wilaya ya Kyela Dk Thea Ntara. Na Ezekiel Kamanga. Watu 17 wakazi wa Kijiji cha Lusungo Kata ya Lusungo Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya wamekamatwa kwa kutokuwa na vyoo na uchafu wa mazingira hivyo kuzorotesha juhudi za kupambana na ugonjwa wa kipindupindu Wilayani humo. Ugonjwa huo umedumu kwa kipindi cha miezi mitatu sasa na Kata ya Lusungo na Ndobo ndizo pekee...

Raia wa nchi ya Somalia anashikiliwa na jeshi la polisi Mkoani Mbeya kwa tuhuma za ubakaji.

Chimbuko Letu | 08:54 | 0 comments
Na Ezekiel Kamanga. Raia wa nchi ya Somalia  Mohamed Ahmed (31) anashikiliwa na jeshi la polisi Mkoani Mbeya kwa tuhuma za kumbaka mtoto  mweye umri wa miaka miwili jina limehifadhiwa. Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Ahmed Msangi alisema kuwa  lilitokea jumapili ya pasaka majira ya saa nne asubuhi katika eneo la Kambi katoto wilayani Chunya. Alisema kuwa Mtuhumiwa Ahmed akiwa na nia ovu alimchukua mtoto nyumbani kwao na kisha kwenda kumbaka na kumsababishia maumivu makali sehemu za siri. “Inadaiwa kuwa mtuhumiwa alienda kumchukua mtoto nyumbani kwao na kwenda nae sehemu isiyojulikana kisha kumbaka, bado tunafanya upepelezi...

Halmashauri ya Jiji la Mbeya yaombwa kuweka kipaumbele katika kuboresha huduma za kijamii.

Chimbuko Letu | 08:50 | 0 comments
Na Ezekiel Kamanga. Wananchi wanaotumia kivuko cha Daraja la Makaburi ya Sabasaba Mtaa wa Jakaranda wameiomba halmashauri ya Jiji la Mbeya kuweka kipaumbele katika kuboresha huduma za kijamii  hususani miundombinu ya barabara, vivuko  kwani vingi vimekuwa hatarishi katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha Jijini hapa. Wakizungumza na kituo hiki jana  kwa nyakati tofauti  walisema kuwa kivuko hicho kimekuwa chakavu kwa muda sasa licha ya kutoa taarifa  kwa viongozi wa serikali za mitaa. Athanas Amosy,Mkazi wa Forest alisema ni vema halmashauri ikaliona hili na kulifanyia kazi kwani wananchi wengi  wamekuwa wakitegemea kivuko  hichi...
Pages (14)1234567 Next
 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger