Pages


WALIOGOMA KUHESABIWA WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:52 | 0 comments
 Pichani wananchi waliokataa kuhesabiwa mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Bwana Guram Hussein Kifu. katikati ni Kiongozi wa Mgomo Bwana Ally Mwangoto, kutoka dini ya Kiislamu wanaojiita wenye msimamo mkali wakiwa chini ya ulinzi katika mahabusu ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Ruiwa,Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya,wakisubiri kupelekwa Polisi wilayani humo. Picha na Habari na Ezekiel Kamanga,Mbarali. Licha ya Rais Jakaya Kikwete kuwataka...

UKOSEFU WA WAWEKEZAJI NDIO CHANZO CHA UCHANGISHWAJI WA USHURU MKUBWA - MBEYA.

Kamanga na Matukio | 05:51 | 0 comments
Habari na Eseter Macha, Mbeya...  Imefahamika kuwa ukosefu wa wawekezaji Mkoani Mbeya unachangiwa na ushuru mkubwa unaotozwa na halmashauri ya jiji hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa wafanyabiashara wakubwa kuwekeza katika mikoa mingine na hivyo kutopanda kwa mapato halmashauri. Hayo yamesemwa na hivi karibuni na Mbunge wa viti maalum kupitia chama cha mapinduzi(CCM) Mkoani Mbeya Dk Mary  Mwanjelwa hivi karibuni  katika kikao maalum cha maadili cha baraza la madiwani  (RCC) Kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkapa. Alisema kuwa kuwa kuna haja kubwa ya halmashauri kujipanga kikamilifu na kuhakikisha kodi za wawekezaji wakubwa zinapunguzwa ili kuongeza...

VUGU VUGU LA UCHAGUZI NDANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

Kamanga na Matukio | 05:50 | 0 comments
 Na Esther Macha,Mbeya Wakati vugu vugu la uchaguzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)likiendelea kushika kasi Rais wa Chama wakandarasi Wenyeji Tanzania(TLCO)Bw.Kura Mayuma amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Mkoa wa Chama hicho Mkoani Mbeya. Alisema kuwa lengo ni kushawishi  serikali kukataa  sheria na kanuni kandamizi kwa wananchi ambazo zimetungwa na Bunge n a mabaraza ya madiwani Mkoani hapa. Bw. ...

UPUNGU WA VIFAA VYA MAABARA KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA MBEYA.

Kamanga na Matukio | 05:49 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya. Upungufu wa  vifaa katika  kitengo cha Maabara katika hospitali ya Mkoa wa Mbeya umetajwa kuwa changamoto kubwa  ambayo inapelekea wagonjwa kuwa katika wakati mgumu  wa kupata vipimo muhimu . Hayo yalisemwa jana na Mratibu wa Huduma za Maabara  katika hspitali ya Mkoa wa Mbeya Dkt.Ezekiel Tuya  wakati alipozungumza  na gazeti hili kuhusu matatizo ambayo yanakwamisha shughuli za maabara hosptalini hapo. Alisema ukusefu huo wa vifaa unasababisha kuendelea kudorola kwa huduma , na tatizp kubwa  lingine ni upungufu wa wataalamu katika taaluma ya afya  hasa vitengo vya maabara  katika hospitali hiyo ambapo...

UCHAMBUZI. IMANI POTOFU KWENYE MATUMIZI YA SARAFU KWENYE POMBE ZA KIENYEJI

Kamanga na Matukio | 05:48 | 0 comments
Na Ester Macha. Katika kuhakikisha kuwa kila mwananchi anaweza kuendesha maisha yake ya na familia wananchi wamekuwa wakijitahidi kubuni mbinu mbadala za biashara ili waweze kujikwamua kiuchumi ili waweze kuondokana  na hali duni ya kimaisha . Kundi ambalo limekuwa likijikita zaidi katika harakati za kuendesha maisha wanawake waliopo vijijini na mijini ambao asilimia kubwa wamekuwa walezi wa familia zao. Lakini ni ukweli usiopingika kuwa kundi hili la wanawake linahitajitaji msaada wa hali na mali kwa kubuni mbinu zingine ambazo zitaweza kuwasaidia kuliko hili wanalotumia ambalo ni  hatari kwa afya za binadamu. Hivi karibuni kumeibuka imani potofu kwa wapikaji pombe...

MAKALA JUU YA VITAMBULISHO VYA TAIFA

Kamanga na Matukio | 05:47 | 0 comments
Makala na Ester Macha. UDANGANYIFU  wa vitambulisho vya Taifa  wenye lengo la utambuzi wa watu Nchini umeingia dosari baada ya watendaji wa mitaa na  kata katika maeneo yao kugeuza zoezi hilo kuwa mradi wao binafsi na kusahau dhamana waliyopewa na serikali ya  kuwatumikia wananchi. Kutokana na Unyeti wa zoezi hili kuna umuhimu wahusika wakuu waweze kuchukuliwa hatua mapema kwani Jiji Dar Es Salaam  ndo limeanza ndo wamekuwa wa kwanza kuanza mchakato huo sasa endapo mamlaka ya vitambulisho ikifanya mzaha kuna hatari maeneo mengine yakashindwa kufikia malengo  vizuri kama ilivyotarajiwa zoezi hili. Tunafahamu kuwa zoezi kama hili ni nyeti kwa Taifa lakini...

WADAU WA ELIMU WAIOMBA SERIKALI KUWEKA MJADALA WA KITAIFA JUU YA SHERIA YA ELIMU NA 25 YA MWAKA 1978

Kamanga na Matukio | 05:46 | 0 comments
Habari na Ester Macha, Ileje. Wadau wa elimu  wilayani Ileje mkoanii Mbeya wameiomba serikali kuwepo na mjadala wa kitaifa juu ya sheria ya elimu namba 25 ya mwaka 1978  ambayo inadaiwa kutoweka wazi suala la wanafunzi kupeana ujauzito wakiwa shuleni. Imeelezwa kuwa sheria ya sasa   iliyopo imekuwa ikitoa adhabu kwa watoto  wa kiume pekee  hivyo wamependeza kuwa kuwa sheria  ambayo wataiuomba kurekebishwa  inapaswa kuwawajibisha wote wawili badala ilivyo hivi sasa,mwanafunzi wa kiume pekee anashitakiwa. Tatizo la mimba mashuleni  limeendelea kupamba moto na hivyo kulazimika wadau wa elimu kwa  ushirikiano wa wananchi kuomba  serikali...

KWANINI WAANDISHI WA HABARI WANAWAKE HAWAJIKITI KATIKA UANDISHI WA HABARI WA JINSIA YAO?

Kamanga na Matukio | 05:45 | 0 comments
Habari na Ester Macha,Mbeya. Kutokana na waandishi wa habari wanawake nchini kutojikita zaidi katika uandishi wa habari za wanawake imeelezwa kuwa hali hiyo  imesababisha  habari zinazohusu wanawake kutoripotiwa kwa undani zaidi na badala yake waandishi wa habari wanaume ndio wamekuwa wakiandika habari hizo. Waandishi wa habari wanawake ndo wanatakiwa kuwa nguzo muhimu katika kuandika habari za afya hususani wanawake waliopo vijijini,wengi wanafahamu matatizo ya wanawake hivyo itakuwa rahisi kuripoti habari hizo kwa upana . Mwito huo umetolewa  jana na Mkufunzi wa wa mafunzo ya habari za afya Dkt.Ahmed Twaha  wakati akitoa mada kwa waandishi wa habari...

APPLE LINE BINGWA WA MCHEZO WA VISHALE (DARTS) MKOA WA MBEYA

Kamanga na Matukio | 03:28 | 0 comments
Wachezaji wa Apple line wakifurahia kubeba vikombe vyote vya ushidi wa  Darts mkoa wa mbeya baada ya kuigalagaza timu ya Polisi mkoa wa mbeya huku wakitoka bila kuaga baada ya kushindwa vibaya katika mchezo huo Mwenyekiti wa klabu ya darts ya Apple line Weston Asisya akiwashukuru wachezaji wenzake kwakupata ushindi huo mkubwa pia timu hiyo imewaomba wakazi wa Mbeya kushiriki katika sensa ya watu na makazi inayoanza jumapili ya tarehe...

MATUKIO YA MKUTANO WA HADHARA ULIOJADILI MAUAJI YANAYOHUSISHWA NA IMANI ZA KISHIRIKINA - MBEYA

Kamanga na Matukio | 03:22 | 0 comments
Diwani wa Kata ya Myunga,Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya mheshimiwa Godfrey Siame kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)(kushoto),alipokuwa akimuonesha mpiga picha wetu moja ya kati ya makaburi saba yanayodaiwa kuwa waliozikwa waliuawa kwa imani za kishirikiana kisha kutolewa viungo vyao kama vile meno,sehemu za siri na Moyo pembezoni mwa Mto Momba.Hata hivyo zaidi ya watu watatu wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo hivyo hawajakamatwa...

KAMA WEWE NI MTANZANIA NA MPENDA HAKI SHARE HIZI PICHA KUPINGA UONEVU NA UNYANYASAJI WA HAKI ZA BINADAMU

Kamanga na Matukio | 01:24 | 0 comments
Kwa hisani ya http://dj-sek.blogspot.com...

WANAMKE AJIFUNGUA KICHANGA NA KUKIZIKA

Kamanga na Matukio | 05:00 | 0 comments
Mwanamke mmoja Bi. Tabu Elias mkazi wa Kitongoji Nambalwe Shina la Mwilonga,Kata ya Magamba,Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya,amejifungua mtoto wa kike na kumzika muda mfupi baada ya kujifungua. Tukio hilo limetokea Agosti 22 mwaka huu kijijini hapo majira ya saa 11:30 jioni,ambapo mwanakme huyo alimzika mtoto huyo chumbani katika nyumba anayoishi. Bi Tabu ametenda ukatili huo wakati mumewe Bwana Gilbert Nzowa,alipokuwa kazini na ndipo aliporejea majira ya saa 12 jioni alimkuta mkewe akiwa hana ujauzito na kumuuliza mkewe kulikoni,ndipo alipomueleza kuwa amejifungua mtoto wa kike na kumzika. Taarifa hiyo ilimkasirisha Bwana Gilbert na kuchukua jukumu la kutoa taarifa kwa Katibu wa Shina...

MATUMIZI YA ARV MKOANI MBEYA YAMEKUWA YA HALI YA JUU.

Kamanga na Matukio | 03:32 | 0 comments
Na Bosco Nyambege ,Mbeya. Mwitikio wa watu katika matumizi ya huduma ya ARV Mkoani Mbeya umebainika kuwa ni mkubwa. Hayo ni kwamujibu wa kaimu mratibu wa kitengo cha UKIMWI mkoa wa Mbeya Dkt.Francis Philly alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jumatano hii. Philly  amesema kuwa mwitikio wa wagonjwa wanaotumia dawa za ARV kuwa ni mkubwa kwani takwimu zinaonesha kuwa kuanzia June 2004 hadi June 2012 wagonjwa waliojiandikisha katika huduma ni 106598 ambapo watu wazima ni 92085 na watoto ni 12889. Ameongeza kuwa kati ya hao walioanzishiwa dozi ya ARV ni 52903 ambapo watu wazima ni 40701 na watoto ni 12202 na watu 13163 hawajulikani kama wamekatisha ...

AUAWA KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI - CHUNYA

Kamanga na Matukio | 03:31 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya. Mkazi wa Kijiji cha Mpona,Kata ya Matundasi,Wilayani Chunya Mkoani Mbeya Joseph  Mwazembe(36) ameuawa na wananchi wenye hasira kali kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya ujambazi. Tukio hilo limetokea Agost 21 mwaka huu majira ya saa 2 usiku katika Kijiji cha Mkatang’ombe,Kata ya Totowe wilayani humo ambapo ilielezwa marehemu alikuwa na wenzake wawili walivamia Grocery ya Hassan Michael (36) mfanyabiashara wa Kijiji cha Mpona. Aidha mara baada ya kuvamia walipora simu za mkononi 15 ambazo thamani yake haikuweza kufahamika mara moja na katika eneo la tukio kulikutwa risasi 5 za SMG na SR  na ganda moja  la risasi na panga alilokutwa...

Mwanafunzi afikwa na mauti baada ya kunywa sumu, Ajali ya Barabara yaua Mkoani Mbeya

Kamanga na Matukio | 05:44 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya. Watu wawili wamefariki dunia Mkoani Mbeya katika matukio mawili likiwemo la mwanafunzi kunywa sumu inayosadikika kuwa ni sumu ya panya,baada ya kufokewa na Bibi yake kwa kosa la kuchelewa kurudi nyumbani. Tukio hilo limetokea Agosti 18 mwaka huu majira ya saa mbili usiku Shukrani Ndembo(18) mwanafunzi wa Kidato cha Tatu katika Shule ya Sekondari Isange na Mkazi wa Kitongoji cha Ndamba,Kijiji cha Isange,Wilayani Rungwe amejikuta akipoteza uhai wake baada ya kunya sumu hiyo. Sakata hilo lilianzia pale Bibi wa marehemu alipomtuma binti huyo dukani kununua mahitaji na kisha kuchelewa kurudi nyumbani na baada ya kuulizwa marehemu aliamua kuchukua...

MKURUGENZI AKIRI BARAZA KUFANYA MAKOSA YA KUWAKATA SHILINGI 200/= WAKULIMA - MBOZI

Kamanga na Matukio | 05:43 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya. Wananchi wa Tarafa  ya Itaka inayojumuisha kata ya Bala, Halungu, Itaka na Nambizo, wilayani Mbozi wamekataa kukatwa shilingi 200 toka kwenye mauzo yao ya kahawa kwa ajili ya kuchangia hisa ya uanzishwaji wa benki ya wananchi wa wilaya humo. Katika mkutano wa baraza la madiwani uliofanyika wilayani hapo uliazimia kila mkulima kukatwa shilingi 200 toka katika mauzo yao ya kahawa ambapo madiwani hao baadhi yao walionekena kutofautiana na kauli ya Charles Chenza, ambaye ni mwaandaji wa rasimu ya uanzishwaji wa benki ya wananchi wilaya ya Mbozi ambapo alisema kuwa kila mkulima wa zao hilo atakatwa kiasi hicho cha fedha ili kuchangia...
Pages (14)1234567 Next
 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger